Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bibilia (66 Books)Hicho kitakakatifu kinachotambua kifo cha mpito ni kipi!!? Tusaidie.
Kama mada inavyojieleza,
Nimekua nikisikia na kusoma katika maandiko ya vitabu vitakatifu kwamba kufa ni pumziko la milele, yani ukishakufa ndo basi tena unapotea jumla.
Lakini maandiko hayo hayo yanasema kuna ufufuo siku ya mwisho ambayo itakua na hukumu kutokana na matendo yako.
Parapanda Italia kwenda kumlaki bwana Yesu mawingu, inasemekana wakati parapanda itakapolia itawakuta watu wengine hai kwa maana hawatakua wamekufa na wale waliokufa watafufuliwa.
Je hapa hatuoni kama haki itakua haijatendeka? Kwa maana haiwezekani watu waliokufa miaka milioni 5 iliyopita wafufuliwe na watu waliokufa siku 2 kabla ya parapanda ya ufufuo? Je kuhusu wale ambao parapanda itawakuta bado hai si ndo watakua wamependelewa zaidi?
Ninavyojua neno milele ni kipindi ambacho hakina mwisho kwa maana ukifa ndo unapotea kabisa miaka trilioni kwa trilioni ijayo, sasa hili suala la kufufuliwa linatoka wapi?
Wale wajuvi wa Theolojia naomba mnipe elimu.