Kama kufa ni kwa milele sasa suala la siku ya mwisho na ufufuo linatoka wapi?

Mambo ya sir God wee acha tuu. [emoji847][emoji847][emoji847][emoji847][emoji847]
 
Haya mambo ukifikiria sana utachanganyikiwa! Ni bora kuyaacha kama yalivyo na kusubiri tu siku yako ya kifo
 

Amani iwe juu yako.

Kufa haimaanishi kupotea tena au pumziko la milele kinachofanyika ni al faraq baina ya mwili na roho. Mwili ndiyo hilo gamba/ jumba na roho ndiyo wewe kwa maana hiyo nafsi yako yaani ndiyo wewe. Kuhusu parapanda zipo za namna mbili ya kwanza ndiyo itakayotoa ishara kwamba dunia, sayari nyengine na ulimwengu kwa ujumla umefika kikomo. Si mbingu wala ardhi zote zitaharibiwa na vilivyomo ndani yake vitakufa.

Parapanda ya pili ndiyo ya ufufuo ya wote waliyokufa mwanzo na waliyokufa parapanda ya kwanza ikipigwa. Lengo la kufa wote ya parapanda ya kwanza ni ile kuithibitisha hali yake kwamba Mungu hafi, yeye ni wa mwanzo tumemkuta na yeye ndiyo wa mwisho tutamkuta. Vilevile kuitimiza ile ahadi yake ya "Kila nafsi itaonja umauti"

Swali lako linalosema wapo waliyokufa takribani miaka millioni 5 na wengine siku 2 kabla ya parapanda, haki iko wapi ikiwa watafufuliwa siku 1? Katika hili inakubidi ujuwe Dhana nzima ya kuumbwa. Na tunayajibu haya kwa sababu swali lako limejikita kiimani ya mambo ya Mungu. Kwa nini niko hapa kwenye sayari? Imekuaje nimefika hapa kwenye hii sayari? Ndiyo maswali wengi wao tunajiuliza. Jibu ni moja tu lazima atakuwepo yule ambaye aliyenifanya niwepo na kama amenifanya niwe hapa bila shaka kuna lengo maalum analitaka mimi nilikamilishe. Nalo ni lipi? Ni kumuabudu kwa tafsiri nyengine apate kuona yupi atakayemshukuru na yupi atakayempa mgongo. Akatupa dira na akatueleza kupitia kwa mitume yake hasi na chanya na makazi yake ni wapi ukiwa mkazi wa hasi na yapi ukiwa mkazi wa chanya. Kwa hiyo kinachomata hapa si huyu alifariki kwa kipindi kirefu kilichopita huyu kafa mwishoni mwa uhai wa ulimwengu, la hasha, kinachomata hapa ni kuangalia wewe ni mkazi wa wapi ni wa hasi au wa chanya. Na hilo ndilo lenye manufaa makubwa zaidi.

Kuhusu suala la kufufuliwa mwanadamu huwa anastaajabu sana wengine hufikia pahala hupinga kabisa. Ilete dhana ya kuunda na dhana ya ku'huisha kitu, kisha jiulize katika hayo ugumu wake upo wapi? Kama umemuamini Mungu amini pia na aliyoyanena. Kufa ni haki, kufufuliwa ni haki. Na ni kweli kuna maisha ya milele, kwa nini kwa sababu ndivyo mwenyewe alivyosema na kuamini ndiyo maana ya imani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…