Kama kuna aliyewahi pitia haya, anisaidie kimawazo

MGODOLO

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2020
Posts
209
Reaction score
174
Habari zenu ndugu wana JF?

Yamenikuta ndugu yenu, naombeni msaada wa kisheria, hii kesi itanibana wapi?

UZI ULIOPITA KUHUSU SWALA HILI

Kuna uzi nilisha wahi kuutoa hapa Jf (LINK HAPO JUU), Kuhusu binti mmoja niliempa mimba, lakini nilipata matatizo kazini kwangu (Traffic case) (mimi ni dereva) tajiri akagharamia mpaka nikawa huru, hivyo mshahara wangu ukawa unakatwa kwa lengo la kufidia kile kiasi walicho kitoa...

Binti yule alijifungua siku moja baada ya mimi kutoka mahabusu, Sikua na kiasi cha pesa kuhusu uzazi, hivyo nikakopa kwa ndugu jamaa na marafiki,.. Nikabahatika kupata kiasi fulani cha pesa

Uzazi ukaenda salama,... Sasa kazini kwangu nakatwa nusu ya mshahara,.. Na nikichukua kilicho baki, napunguza mkopo niliokopa kwa ndugu jamaa na marafiki, hivyo kiasi ninachobakiwa nacho ni kidogo kiasi kwamba nashindwa kutoa matumizi mazuri kwenye ile familia yangu,.. Na sababu ya familia yangu kuishi kwao ni kukosa mahari ya kuoa.. Sasa kutokana na udogo wa pesa, nikawa nawapatia elfu 40 kwa mwezi, (WAO HULALAMIKA NI KIASI KIDOGO ILIHALI MATATIZO YANGU WANAYAJUA) Mtoto wangu sikuweza kumpelekea nguo, lakini yote ni ukosefu wa pesa. Hivyo nikaendelea kutoa hio 40 kila mwezi. Tena kwa kujibana mno, wakati mwingine naacha kulipa kodi niwatumiwe wao.

Sasa Mwishoni mwa mwezi wa kwanza, Nikaschishwa kazi, na bado deni lao sijamaliza, na hata wale ndugu jamaa na marafiki nilio wakopa madeni yao sijamaliza pia

Tajiri yangu akasema, (KWASABABU BADO NAKUDAI TAKRIBANI LAKI SITA HIVI, NAKUSAMEHE, LAKINI MSHAHARA WAKO WA JANUARI HATUTOKUPA ILI KUPUNGUZA DENI LETU)... Ndugu yenu nilichanganyikiwa kuskia hata mshahara wangu sitapewa, na jinsi JANUARI ILIVYO

Nilitoka kinyonge sana.

Sasa baba yake yule binti, kasikia kua sina kazi,.. Nikaitwa kikao siku ya Alhamisi ya tarehe 09/02/2023,.. Wakaniuliza nina mpango gani na binti yao?.. Mimi nikawajibu, niko tayari kumuoa lakini changamoto ni mahari ambayo mtataka kwasasa sina... (HUYO NI BABA YAKE WA KAMBO) Baba yake huyo akasema Jumapili ya wiki ijayo, ambayo ndio Jumapili ya leo tarehe 19, Kua watakuja wajomba zake binti ufungishwe ndoa, kwahio andaa pesa ya ubani...

Nikaona ni poa na uzuri, mwanamke yupo tayari kuishi maisha yeyote,.. Anajua sina kazi lakini yupo tayari kuolewa, nami naona poa mungu ata bless mbele kwa mbele...

Sasa Jumapili ya leo tarehe 19/02/2023, Wajomba ndani ya nyumba... Nilijiandaa na kama elfu 30,000 (elfu thelathini) kama ya kufungisha ndoa, na ndani nilikua na elfu 50 tu, hivyo nimebakiza elfu 20 ndani, yaani kama ikitokea nimepewa mke,. Tuanze nayo kisha mungu abless mbele kwa mbele

Lakini kikao hicho, dhumuni lao ni lile lilena kutaka mahari kwanza.. Nikawambia, (KWASASA SINA KAZI, HIO MAHARI NITATOA WAPI) Wakasema (YAANI UNA WIKI MBILI TU HUNA KAZI, AFU LEO UNASEMA HUNA PESA.. HAIWEZEKANI, HUYU TUMPELEKE DAWATI, LAZIMA TWENDE USTAWI WA JAMII... WEWE ONDOKA ZAKO, TUTAJUA CHAKUFANYA) nikaondoka kwenye kikao hicho mida ya saa kumi na moja jioni hii,..

Kuhusu mwanamke anataka kuolewa namimi hata kama sina mahari, ila wazazi wake ndio wanakaza... Sasa najua wakienda huko dawati,.. Lazima wamsokote mtoto wao namna ya kuongea ili wanibane kisheria... Je? Kama itatokea hivyo,.. Mimi nifanyeje ndugu zangu, Mana wajomba wamekua wamoto

Kama kuna aliwahi pitia haya, anisaidie kimawazo, lakini kama kuna mhusika wa ustawi wa jamii pia anipe mawazo, nifanyeje?

Nawasilisha..... Nitangulize shukrani zangu kwenu.
 
Hamna kesi hapo mjomba . kikubwa wewe na mzazi mwenzako mnaelewana. Na huko dawati mbona mambo ndio yatakuwa mepesi zaidi maana wao wanachoangalia ni kuhudumia familia kitu ambacho kwako sijaona kama ni tatizo. masuala ya mahari hayawahusu wao
 
Ishu simple kama hawakuelewi wachukue binti yao mpaka utakapo kaa sawa. Inaonekana pia uliwazoesha vibaya tangu mwanzo kuwaonesha unazo
 
Tulisema ukiona mzazi ambaye ni mama ana sauti usioe au usiolewe.sasa naona mpaka ndugu washaanza kuingilia haya mambo.

Wakitaka kuondoka na binti yao wape si wanatumia fimbo kisa kazi.

Mbona mambo mengine rahisi sana kuna watu wanaomba kupunguziwa matatizo kwa njia kama hizo ukajipange
 
mchukue binti mkafunge ndoa serikalini kimya kimya.. afu tulia
 
pole kwa maswahibu, sasa mahari wanaitaka ya nn hao wajomba kwani wao ndio wanaolewa au wataishi na wewe?? naelewa wewe ni muslim simamia hapo mahari ni haki ya mke, hivo hao hawana haki ya kuidai, na inaswihi kumuoa hata kama huna hayo mahari ila utambue tu hilo ni deni kwako,

Kuhusu ustawi wa jamii waache waende, punguza panic, kua calm, wasikilize hoja zao, wakishikilia wanataka matunzo waambie huna kazi utatoaje matunzo kwa wakati?

Hapo kabla ulikua nayo s ulikua unaudumia bila shida? Mkuu kama huyo binti anakupenda alipaswa yeye kama yeye awaeleze hali halisi unayoipitia sio akueleze wewe, awaeleze wajomba zake yeye ameridhia n anajua huna kazi na hua unahudumia, mke gani anashindwa kukupigia kifua kwao??
 
Ishu simple kama hawakuelewi wachukue binti yao mpaka utakapo kaa sawa. Inaonekana pia uliwazoesha vibaya tangu mwanzo kuwaonesha unazo
Hapana kaka, tena nilikua na matatizo hivyo sikuweza kabisa, soma uzi uliopita mkuu
 
Hamna kesi hapo mjomba . kikubwa wewe na mzazi mwenzako mnaelewana. Na huko dawati mbona mambo ndio yatakuwa mepesi zaidi maana wao wanachoangalia ni kuhudumia familia kitu ambacho kwako sijaona kama ni tatizo. masuala ya mahari hayawahusu wao
Sema wanaweza kumsokota binti yao akaongee hata uongo, ikanibana kisheria
 
Kama nakuona vile anyway huna wazee mnaaoeshimiana hapo mtaani kwako.
Yaani hawa watu ishu sio wazee, ishu wameweka mbele kutaka mahari, Kitu ambacho kwasaaa ni kigumu kwangu kwasababu sina kazi
 
Umaskini ni shida asee. Yani ndugu tena wanaume kabisa wanalazimisha mtoto wao atolewe mahari tena kwa vitisho.

Asee tutafute hela. Hizi tabu zote ni umaskini tu.
 
pole kwa maswahibu, sasa mahari wanaitaka ya nn hao wajomba kwani wao ndio wanaolewa au wataishi na wewe?? naelewa wewe ni muslim simamia hapo mahari ni haki ya mke...
Mke ni kama roboti hana sauti popote, yaani vitakavyokua nayeye hukohuko
 
Habari zenu ndugu wana JF?

YAMENIKUTA NDUGU YENU, NAOMBENI MSAADA WA KISHERIA, HII KESI ITANIBANA WAPI?

UZI ULIOPITA KUHUSU SWALA HILI

Kuna uzi nilisha wahi kuutoa hapa Jf (LINK HAPO JUU), Kuhusu binti mmoja niliempa mimba, lakini nilipata matatizo kazini kwangu (Traffic case) (mimi ni dereva) tajiri akagharamia mpaka nikawa huru, hivyo mshahara wangu ukawa unakatwa kwa lengo la kufidia kile kiasi walicho kitoa...

Binti yule alijifungua siku moja baada ya mimi kutoka mahabusu, Sikua na kiasi cha pesa kuhusu uzazi, hivyo nikakopa kwa ndugu jamaa na marafiki,.. Nikabahatika kupata kiasi fulani cha pesa

Uzazi ukaenda salama,... Sasa kazini kwangu nakatwa nusu ya mshahara,.. Na nikichukua kilicho baki, napunguza mkopo niliokopa kwa ndugu jamaa na marafiki, hivyo kiasi ninachobakiwa nacho ni kidogo kiasi kwamba nashindwa kutoa matumizi mazuri kwenye ile familia yangu,.. Na sababu ya familia yangu kuishi kwao ni kukosa mahari ya kuoa.. Sasa kutokana na udogo wa pesa, nikawa nawapatia elfu 40 kwa mwezi, (WAO HULALAMIKA NI KIASI KIDOGO ILIHALI MATATIZO YANGU WANAYAJUA) Mtoto wangu sikuweza kumpelekea nguo, lakini yote ni ukosefu wa pesa. Hivyo nikaendelea kutoa hio 40 kila mwezi. Tena kwa kujibana mno, wakati mwingine naacha kulipa kodi niwatumiwe wao.

Sasa Mwishoni mwa mwezi wa kwanza, Nikaschishwa kazi, na bado deni lao sijamaliza, na hata wale ndugu jamaa na marafiki nilio wakopa madeni yao sijamaliza pia

Tajiri yangu akasema, (KWASABABU BADO NAKUDAI TAKRIBANI LAKI SITA HIVI, NAKUSAMEHE, LAKINI MSHAHARA WAKO WA JANUARI HATUTOKUPA ILI KUPUNGUZA DENI LETU)... Ndugu yenu nilichanganyikiwa kuskia hata mshahara wangu sitapewa, na jinsi JANUARI ILIVYO

Nilitoka kinyonge sana.

Sasa baba yake yule binti, kasikia kua sina kazi,.. Nikaitwa kikao siku ya Alhamisi ya tarehe 09/02/2023,.. Wakaniuliza nina mpango gani na binti yao?.. Mimi nikawajibu, niko tayari kumuoa lakini changamoto ni mahari ambayo mtataka kwasasa sina... (HUYO NI BABA YAKE WA KAMBO) Baba yake huyo akasema Jumapili ya wiki ijayo, ambayo ndio Jumapili ya leo tarehe 19, Kua watakuja wajomba zake binti ufungishwe ndoa, kwahio andaa pesa ya ubani...

Nikaona ni poa na uzuri, mwanamke yupo tayari kuishi maisha yeyote,.. Anajua sina kazi lakini yupo tayari kuolewa, nami naona poa mungu ata bless mbele kwa mbele...

Sasa Jumapili ya leo tarehe 19/02/2023, Wajomba ndani ya nyumba... Nilijiandaa na kama elfu 30,000 (elfu thelathini) kama ya kufungisha ndoa, na ndani nilikua na elfu 50 tu, hivyo nimebakiza elfu 20 ndani, yaani kama ikitokea nimepewa mke,. Tuanze nayo kisha mungu abless mbele kwa mbele

Lakini kikao hicho, dhumuni lao ni lile lilena kutaka mahari kwanza.. Nikawambia, (KWASASA SINA KAZI, HIO MAHARI NITATOA WAPI) Wakasema (YAANI UNA WIKI MBILI TU HUNA KAZI, AFU LEO UNASEMA HUNA PESA.. HAIWEZEKANI, HUYU TUMPELEKE DAWATI, LAZIMA TWENDE USTAWI WA JAMII... WEWE ONDOKA ZAKO, TUTAJUA CHAKUFANYA) nikaondoka kwenye kikao hicho mida ya saa kumi na moja jioni hii,..

Kuhusu mwanamke anataka kuolewa namimi hata kama sina mahari, ila wazazi wake ndio wanakaza... Sasa najua wakienda huko dawati,.. Lazima wamsokote mtoto wao namna ya kuongea ili wanibane kisheria... Je? Kama itatokea hivyo,.. Mimi nifanyeje ndugu zangu, Mana wajomba wamekua wamoto

Kama kuna aliwahi pitia haya, anisaidie kimawazo, lakini kama kuna mhusika wa ustawi wa jamii pia anipe mawazo, nifanyeje?

Nawasilisha..... Nitangulize shukrani zangu kwenu.

Acha uboya. Hapo hamna kesi, tena shikilia huo msimamo wako tu. Mke wanakupa bure maana hawana uhalali wala haki ya kwenda kwenye dawati la jinsia.

Hiyo ni mikwara tu ili utoe mahari wale. Ila wakijichanganya kwenda, uwe muwazi tu kwamba upo tayari kumuoa binti uhudumie mama na mtoto wako kama familia ila huna mahari.

Kesi imeisha.
 
Back
Top Bottom