Kama kuna homa mpya na mimi ilinipitia. Ukiona una dalili nilizopata tumia tiba hizi, weka ubahili pembeni

Kama kuna homa mpya na mimi ilinipitia. Ukiona una dalili nilizopata tumia tiba hizi, weka ubahili pembeni

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
October 17 had 27 Mwezi uliopita kuna kipindi nilipitia kipindi kigumu sana.

Kwanza kabisa nilianza kwa kukohoa, nilichukulia kawaida lakini siku ya pili nakohoa sana, asubuhi nilienda kununua good morning haikusaidia chochote

Jioni nimefika nyumbani mara ghafla tu mwili hauna nguvu, vungo havna nguvu, appetite hamu ya kula imepungua, kichwa kinauma na kikohozi kinaendelea, haikuwa hali mpya kwangu nikajua moja kwa moja nina homa pia ni dalili za Homa tulizofundishwa shuleni.

Kwenye akiba ya dawa zilibaki Toffplus na azuma nilizitumia lakini wapi, hapo bado naendelea kutumia goodmorning ya kkohozi bila unafuu wowote.

Siku ya tatu dalili mpya ikaongezeka ya kuhara nikaenda nkajivuta kununua flagil lakini wapi.

Ikabidi jioni niende kununua dawa ya homa Atequick shilingi elfu 10 na mia tano.

Muda mwingi nilitumia kulala.

Siku ya nne nikahisi kwa mbali sana mwili na viungo vimepata nguvu, nikafika muafaka niendelee na dozi, lakini kikohozi bado

Siku ya tano naendelea kutumia atequick, mwili na viungo vinaendelea kupata nafuu japo ni taratibu ila kikohozi kinaendelea nimenunue googd morning ya pili.

Siku ya sita dozi ilikuwa imeisha ya atequick, nilijidanganya nitajiponea kwasababu niliwahi kuumwa homa, dozi moja ilinitosha, nisilojua ni kwamba homa ya sasa ni balaa zaidi.

Hiyo siku ya sita kikohozi kilinikamata vibaya mno, nilikuwa nimelala ghafla nikaamka nikipumua nahisi maumivu mpaka nyuma kwenye mgongo, niliposimama nilihisi nakufa kwa kupumua, yani nikikohoa nahisi mbavu ya kushoto inachomolewa, kwa bahati nzuri nilipata wazo nijifunge taula kifuani nilikaza sana, hapo nilipata nafuu.

Siku ya saba nikaenda kununua dawa ya vidonge ya kikohozi inaitwa Flucamox, hii ndio ilinipa ahueni, Good morning haikufua dafu, nikaongezea na dozi ya atequick

Kikohozi nikaanza kupata nafuu huku atequick ilinisaidia kurudisha nguvu za mwili, kuondoa maumivu ya viungo, kupunguza kichwa kuuma, n.k.

Kufikia siku ya 10 nilikuwa na nafuu, mtihani ulikuwa ni chakula kukosa ladha japo niliweza kula, chakula changu kilikuwa ni chipsi, nyama na kinywaji grand malt.

Niliongeza dozi ya ziada ya atequick niliyotumia siku ya 11

Nilipona kabisa siku ya 12, msoto niliopitia sio wa kitoto

Ushauri:

Wahi hospitalini upimwa, Usikariri kutumia dawa flan kwa homa, Unaweza kupewa tiba bora zaidi

Kama upo mbali na hospitali nunua nunua dozi 2 za siku 6 na dawa ya kifua tumia nunua Flucamox

cc: Nimeponea tundu la sindano kufa. Serikali ichukue hatua, kuna mlipuko unaua kimya kimya
 
Mwezi uliopita kuna kipindi cha siku 10 nilizozihesabu nilipitia kipindi kigumu sana, 2 za mwisho zilinipa tabu kwa maradhi machache.

Kwanza kabisa nilianza kwa kukohoa, nilichukulia kawaida lakini siku inayofuata nakohoa sana, asubuhi nilienda kununua good morning haikusaidia chochote

Jioni nimefika nyumbani mara ghafla tu mwili hauna nguvu, appetite hamu ya kula imepungua, kichwa kinauma na kikohozi kinaendelea.

Nilitumia Toffplus na azuma lakini wapi, hapo bado naendelea kutumia goodmorning

Kesho yake dalili mpya ikaongezeka ya kuhara nikaenda kununua flagil lakini wapi

Ikabidi jioni niende kununua dawa ya homa Ateqquick shilingi elfu 10 na mia tano

Kwa mara ya kwanza dawa hii ndio ilinipa unafuu, kumbuka hapo nipo siku ya tatu

Kula ilikuwa shida sana, chakula hakina ladha, chakula nikila hakiingii nahisi kutapika,

muda mwingi nilitumia kulala,

siku ya nne na ya tano naendelea kutumia atequick, mwili kidogo unaanza kupata nguvu ila kikohozi kimepamba moto

Siku ya sita dozi ilikuwa imeisha ya atequick nilihisi nitajiponea kwasababu nilianza kupata nafuu,

hio siku kikohozi kilinikama vibaya mno, nilikuwa nimelala ghafla nikaamka nikipumua nahisi maumivu mpaka nyuma kwenye mgongo, niliposimama nilihisi nakufa, yani nikikohoa nahisi mbavu ya kushoto inachomolewa, kwa bahati nzuri nilipata wazo nijifunge taula kifuani nilikaza sana, hapo nilipata nafuu.

Siku ya saba nikaenda kununua dawa ya vidonge ya kikohozi inaitwa Flucamox, hii ndio ilinipa ahueni, Good morning haikufua dafu, nikongezea na vidonge dozi ya atequick

Kikohozi nikaanza kupata nafuu, atequick ilinisaidia kurudisha nguvu za mwili, kuondoa maumivu ya viungo, kupunguza kichwa kuuma, n.k.

Kufikia siku ya 10 nilikuwa na nafuu, mtihani ulikuwa ni chakula kukosa ladha japo niliweza kula, wali sokuweza kula, ugali ndio kabisa, chakula changu kilikuwa ni chipsi, nyama na kinywaji grand malt,

Niliongeza dozi ya ziada ya atequick niliyotumia siku ya 11,

Nilipona kabisa siku ya 12, msoto niliopitia sio wa kitoto

Ushauri:

Tumia dawa ya Atequick, nunua dozi 2 utazotumia siku 6, tumia hizo kwanza kama hazitatosha ukaongeze, usiruke dozi

Dawa ya kifua tumia Flucamox
Ushauri mbaya sana huu. Nakushauri nenda hospitali kapime ujue tatizo kabla ya kuanza kutumia sumu(dawa) hovyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo ni malaria na ni kawaida, mafua, kichwa, ladha ya chakula na zaman hata kutapika haswa!

Mmekuwa walaini sana siku hizi! Unataka serikali ifanyeje? Pambana Mzee, hii ndo Dunia!

Unafikiri Kwa Nini mtoto akizaliwa tu analia? Kaingia kwenye Dunia ya tabu na ziki za kutosha, pigana, pigana, pigana
 
Mtu mwenye uelewa wa kutumia jf ukashindwa kwenda hospitali kujua unaumwa nini. Kweli Tanzania nchi ngumu
Tulishafundishwa kwenye Biology Dalili za homa, Elimu nayo inasaidia,

Tofauti ni kwamba homa hii ni kali zaidi
 
Usitupe lawama mkuu
Nimeulizwa swali tu, kwenye maelezo yake sijaona anywhere alipotaja aina ya ugonjwa zaidi ya kuzitaja dalili/symptoms, siku 12 zote akiwa kitandani, ni hatari sana kujinunulia dawa bila kujua unacho umwa, kuharisha sio mara zote ni bacteria, sometimes inaweza kua malaria. Kukohoa ni dalili ya ugonjwa, sasa kununua tu dawa while hujui unaumwa nini is like kujipa sumu tu. Tupo dunia ya kisasa sana, tusibahatishe katika kujitibu; twendeni hospital. Ushauri tu
 
Mzee hizo dawa ulizopiga mixer ni hatari ukizipiga tu zenyewe bila kuumwa unaweza kuumwa, hizo ni dalili za corona ungejifukiza na kupiga nyungu matokeo yangekuwa chanya zaidi
1000014637.jpg
 
Mwezi uliopita kuna kipindi cha siku 10 nilizozihesabu nilipitia kipindi kigumu sana, 2 za mwisho zilinipa tabu kwa maradhi machache.

Kwanza kabisa nilianza kwa kukohoa, nilichukulia kawaida lakini siku ya pili nakohoa sana, asubuhi nilienda kununua good morning haikusaidia chochote

Jioni nimefika nyumbani mara ghafla tu mwili hauna nguvu, appetite hamu ya kula imepungua, kichwa kinauma na kikohozi kinaendelea.

Nilitumia Toffplus na azuma lakini wapi, hapo bado naendelea kutumia goodmorning ya kkohozi bila unafuu wowote.

sku ya tatu dalili mpya ikaongezeka ya kuhara nikaenda nkajivuta kununua flagil lakini wapi

Kula ilikuwa shida sana, chakula hakina ladha, chakula nikila hakiingii nahisi kutapika,

Ikabidi jioni niende kununua dawa ya homa Atequick shilingi elfu 10 na mia tano

muda mwingi nilitumia kulala,

Nikafikia maamuzi nina homa, hivyo nitumie atequick kama nilivyozoea

Siku ya nne nikahisi kwa mbali sana mwili na viungo vimepata nguvu, nikafika muafaka niendelee na dozi, lakini kikohozi bado

siku ya tano naendelea kutumia atequick, mwili na viungo vinaendelea kupata nafuu japo ni taratibu ila kikohozi kinaendelea nimenunue googd morning ya pili.

Siku ya sita dozi ilikuwa imeisha ya atequick, nilijidanganya nitajiponea kwasababu niliwahi kuumwa homa, dozi moja ilinitosha, nisilojua ni kwamba homa ya sasa ni balaa zaidi.

hio siku ya sita kikohozi kilinikamata vibaya mno, nilikuwa nimelala ghafla nikaamka nikipumua nahisi maumivu mpaka nyuma kwenye mgongo, niliposimama nilihisi nakufa kwa kupumua, yani nikikohoa nahisi mbavu ya kushoto inachomolewa, kwa bahati nzuri nilipata wazo nijifunge taula kifuani nilikaza sana, hapo nilipata nafuu.

Siku ya saba nikaenda kununua dawa ya vidonge ya kikohozi inaitwa Flucamox, hii ndio ilinipa ahueni, Good morning haikufua dafu, nikaongezea na dozi ya atequick

Kikohozi nikaanza kupata nafuu huku atequick ilinisaidia kurudisha nguvu za mwili, kuondoa maumivu ya viungo, kupunguza kichwa kuuma, n.k.

Kufikia siku ya 10 nilikuwa na nafuu, mtihani ulikuwa ni chakula kukosa ladha japo niliweza kula, chakula changu kilikuwa ni chipsi, nyama na kinywaji grand malt.

Niliongeza dozi ya ziada ya atequick niliyotumia siku ya 11,

Nilipona kabisa siku ya 12, msoto niliopitia sio wa kitoto

Ushauri:

Wahi hospitalini upimwa, usijitibu kwa kubahatisha kama mimi

Kama upo mbali na hospitali nunua nunua dozi 2 za siku 6 na dawa ya kifua tumia nunua Flucamox
Pole sana kwa uliyoyapitia.

Katika kujitibu ulitumia dawa nyingi (antibiotics) ambazo haikuwa lazima kuzitumia pengine ulitumia kwa sababu hukujua hasa unatibu kitu gani! Sasa matumizi haya holela ya dawa za antibiotics ndiyo inayochangia usugu wa dawa hizo ktk kuua bacteria tatizo ambalo tunalishuhudia kwa sasa. Mfano kuna tafti zinaonyesha magonjwa ya zinaa (Gonorrhea nk) zinaelekea kutotibika kutokana na usugu wa wadudu wake kwa dawa zinazotumika kutibu.

Ungeenda kuonana na daktari tatizo lako umeelezea vizuri hizo dalili kwa hiyo liko wazi na ungepatiwa dawa sahihi na kuepuka hayo matumizi holela ya antibiotics.

Kwa hiyo ni muhimu kuonana na daktari ili akuandikie dawa sahihi na kwa kufanya hivyo tutalinda dawa (antibiotics) hizi dhidi ya usugu unaokuja kwa kasi.
 
Tulishafundishwa kwenye Biology Dalili za homa, Elimu nayo inasaidia,

Tofauti ni kwamba homa hii ni kali zaidi
Homa sio ugonjwa ni dalili ya ugonjwa. Sasa wewe hukujua unaumwa nini ukanywa dawa
 
Mkuu kuna wengine tuna perception mbaya zidi hospitals, sometimes mtu hana hima anakwepa direct charges,

Mwingine ndo hivo kakua kwa mitishamba

Mfano mimi mwakajana Dec nimeugua ulcers nikaenda hosp nikazuiliwa vyakula vyny gesi na vyenye acidic nature Sasa hapo mkuu ni almost 80% ya vyakula niliacha

Dawa nilizokua natumia omoprazole(the spelling not sure)
Nikawa sion vizuri kichwa kinauma
Ikabidi Niache dozi nikabadili mazingira vile vidonda vilipotea tu
(most nlikua nakula mnafu na mchicha)

So siku hzi ni kama vinarud especially siku nitapowaza sana.so nawaza zile medicine alizoniandikia zilikuwa na salama almost vidonge 18per day

Pole sana kwa uliyoyapitia.

Katika kujitibu ulitumia dawa nyingi (antibiotics) ambazo haikuwa lazima kuzitumia pengine ulitumia kwa sababu hukujua hasa unatibu kitu gani! Sasa matumizi haya holela ya dawa za antibiotics ndiyo inayochangia usugu wa dawa hizo ktk kuua bacteria tatizo ambalo tunalishuhudia kwa sasa. Mfano kuna tafti zinaonyesha magonjwa ya zinaa (Gonorrhea nk) zinaelekea kutotibika kutokana na usugu wa wadudu wake kwa dawa zinazotumika kutibu.

Ungeenda kuonana na daktari tatizo lako umeelezea vizuri hizo dalili kwa hiyo liko wazi na ungepatiwa dawa sahihi na kuepuka hayo matumizi holela ya antibiotics.

Kwa hiyo ni muhimu kuonana na daktari ili akuandikie dawa sahihi na kwa kufanya hivyo tutalinda dawa (antibiotics) hizi dhidi ya usugu unaokuja kwa kasi.
 
Mkuu kuna wengine tuna perception mbaya zidi hospitals, sometimes mtu hana hima anakwepa direct charges,

Mwingine ndo hivo kakua kwa mitishamba

Mfano mimi mwakajana Dec nimeugua ulcers nikaenda hosp nikazuiliwa vyakula vyny gesi na vyenye acidic nature Sasa hapo mkuu ni almost 80% ya vyakula niliacha

Dawa nilizokua natumia omoprazole(the spelling not sure)
Nikawa sion vizuri kichwa kinauma
Ikabidi Niache dozi nikabadili mazingira vile vidonda vilipotea tu
(most nlikua nakula mnafu na mchicha)

So siku hzi ni kama vinarud especially siku nitapowaza sana.so nawaza zile medicine alizoniandikia zilikuwa na salama almost vidonge 18per day
Pole,
Ulikuwa unameza vidonge 18 per day au 8 per day?

Huwa tunashauri kama kuna hali au dalili utaona baada ya kuanza kutumia dawa ulizopewa hospital ni vyema ukarudi au ukawasiliana na daktari wako ili kujua kama ni kutokana na dozi au la,
 
Naungana na mdau, wadau walioshauri angepima kwanza.

Hapo tunaona hata suala lake la kurudia dozi za maralia tena kali mara mbilimbili ni dalili kuwa hatibu ugonjwa husika.

Angepima kama ni homa ya typhoid/homa a matumbo ama nn. Tena kama hint tu taifodi ikiwepo inacomplicate uponaji wa maralia. Saaa ni vema kupima na kutibu vyote kikamilifu
 
Tusipende sana kununua dawa bila prescription, bila kupima na kujua tatizo. Kuna baadhi wamepata magonjwa ya kudumu kwa kutumia dawa bila vipimo.
 
Back
Top Bottom