Kama kuna member humu anaweza kuniamini nakunikopesha angalau milioni 1

flulanga

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2016
Posts
4,860
Reaction score
6,390
Ndugu zangu ninakijiwe kinachoniingizia sio chini ya laki 3 kwamwezi, ila nimejiongeza nataka nifungue kijiwe kingine kama hichohicho ili niweke mtu ili niwe navijiwe viwili angalau kwamwezi niwe naingiza kuanzia laki 5. Changamoto yangu nimepeleza mtaji, maandalizi mengine yapo fresh ila sasa pesa ya kuwekeza hapo ndio shida inapoanzia, nikisema nivute subira ili nidundulize ili nipate huo mtaji naona tachelewa sana maana hiyo laki 3 ninayoingiza ndio naitegemea kuendeshea maisha yangu yakila siku.

Kama kuna member humu anaweza kuniamini nakunikopesha angalau milioni 1 ili niwekeze katika biashara yangu alafu nikae nayo ndani yamiezi 4, malipo nitalipa kwaawamu 4 kila mwezi nitalipa laki 2 nanusu. Najua wapo watu humu wenye moyo huo namungu amewajaaria huo uwezo.

NB: sipendelei riba kwasababu nidhambi. Uaminifu niasilimia zote.
 
Acha masihara mzee, mtu akupe milion yake ukae nayo miezi minne bila dhamana yoyote wala riba??
 
Kuna mikopo inatolewa kila kata kwa ajili ya vijana. Jiungeni watano, kaombeni mkopo mfanye kazi
Mkuu ishajaribu kwenda manispaa nakuonana namuhusika wamikopo kwavijana nakinamama aliniambia kama wewe hivyo ila changamoto nilivyoona nijiinsi yakuwapata hao vijana wenye malengo nawenye biashara ambao tungejiunga nakuomba mkopo, kiukwel niliwakosa, Jamii iliyonizunguka wengi wavijana hawana muamko wakupambambana, n
 
Kuna mikopo inatolewa kila kata kwa ajili ya vijana. Jiungeni watano, kaombeni mkopo mfanye kazi
Mkuu hiyo ni hatari maana watu wamesha lipa madeni ya watu mpaka wamechoka labda mjiunge mumchukulie m1 mnaeamini atarudisha ila awapooze mikopo ya vikundi noma
 
Unafanya biashara gani?
 
Wewe tapel mkubwa. Huna kijiwe wala nini. Yaani uingize laki 3 kila mwezi halafu ushindwe kupata pesa kuongezea mtaji wako. Haupo serious kweli wewe.
 
Wewe tapel mkubwa. Huna kijiwe wala nini. Yaani uingize laki 3 kila mwezi halafu ushindwe kupata pesa kuongezea mtaji wako. Haupo serious kweli wewe.
Naamini ujasoma uzi wangu vizuri ila umekurupuka tu mkuu, nimesema naingiza laki 3 nikweli ila nikasema hiyo laki 3 ndio naitegemea kuendeshea maisha yangu yakila siku
 
Sijawai hona, eti riba dhambi, kauli hiyo inabidi aitoe mtoa pesa sio wewe muhitaji msaada.

Riba kweli dhambi ila hili inabidi alielewe mwenye pesa, mimi nakopa sana kwa riba bila riba nitapata wapi hiyo pesa mambo yanaferi au nife njaa.
 
Huyu anataka azamie south[emoji23][emoji23] kaja na kigezo cha riba ili aonekane ni mwaminifu aliyeshika dini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…