Kama kuna Mwalimu wa Kiingereza na Kiswahili kwa ngazi ya sekondari anayejua vizuri lugha ya Kichaga naomba tuwasiliane

raslimali

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2014
Posts
1,958
Reaction score
1,744
Habari wakuu.

Kuna jambo nataka kufanya kuhusu lugha ya kichaga.

Naomba kama humu jamvini kuna mwalimu wa sarufi ya Kiswahili na Kiingereza kwa ngazi ya kidato cha nne tuwasiliane tuone tunaanzia wapi. Natanguliza shukrani.

Hata kwa yeyote atakayesoma uzi huu na anamjua mwalimu yeyote tuwasiliane.
 
Mimi sijui kichaga mkuu ila Niko competente
Mkuu nahitqji mtu anayejua grammar vizuri ili tutengeze program za lugha ya kichaga kwa ajili ya utalii na kwa kwa ajili ya vyuo vikuu vya nje kwenye faculties za linguistics na kwa ajili ya mtu yeyote mwenye interest ya kujifunza lugha za makabila ya Tanzania
 
Aika mbe, kotana mbe
 
Africa nzima ina lugha za kikabila zaidi ya 1000 na zote hazina applicability yoyote nje ya umbea. Unategemea mtu gani kutoka nje aje kuwa na interest ya kujifunza lugha za makabila, tena kutoka Africa?
 
Sasa mkuu mbona unatoa code ya idea public
 
Kichaga ni lugha Pana na inatofautiana kutoka eneo Moja na lingine fafanua zaidi
Naelewa vizuri. Mimi nimesoma lugha ya Kijerumani na kuifanyia kazi miaka mingi sana na nimeandika mpa vitabu kwa Kijerumani .Kijerumani pia kina DIALECTS ambazo ukienda kama Bayern (Bavaria) ukakutana na wazee unaweza usielewe wanachoongea. Ila kuna HIGH GERMAN au STANDARD GERMAN inayotumika hata mashuleni ambayo kila mtu ambaye siyo mjerumani anajifunza. Kwenye Kichaga hakuna lugha ambayo tukiongea wote tutaelewana? Maana tukisema watu wajifunze dialects zote itakuwa kazi kweli kweli. Hebu tulifanyie kazi hili.
 
Bahati mbaya hakuna lugha ya kichaga kama ilivyo kwa makabila mengine kama kizaramo au kimakonde
 
Africa nzima ina lugha za kikabila zaidi ya 1000 na zote hazina applicability yoyote nje ya umbea. Unategemea mtu gani kutoka nje aje kuwa na interest ya kujifunza lugha za makabila, tena kutoka Africa?
Ninazo cases nyingi sana za watu wenye interest hizo. Watu wanakuja kufanya research ya lugha za warangi na wahadzabe na wasandawe
 
Anamaanisha lugha ya Kichaga imegawanyika. Kuna kichaga cha Rombo, Maranga, Old Moshi etc. Hizi lugha zote no tofauti na wanaingiliana maneno machache. So unatakiwa kuwa specific unataka awe anajua kichaga cha wapi. Kwa lengo lako hilo nashauri utafute mtu mzima wa makamo anyejua kichaga ashirikiane na huyo mwalimu wa kiingereza/Kiswahili. Maana kwa kiazazi cha kuanzia miaka ya themanini kichaga hatukijui kiundani kivile. Tunajua tu cha kuombea maji.
Naelewa vizuri. Mimi nimesoma lugha ya Kijerumani na kuifanyia kazi miaka mingi sana na nimeandika mpa vitabu kwa Kijerumani .Kijerumani pia kina DIALECTS ambazo ukienda kama Bayern (Bavaria) ukakutana na wazee unaweza usielewe wanachoongea. Ila kuna HIGH GERMAN au STANDARD GERMAN inayotumika hata mashuleni ambayo kila mtu ambaye siyo mjerumani anajifunza. Kwenye Kichaga hakuna lugha ambayo tukiongea wote tutaelewana? Maana tukisema watu wajifunze dialects zote itakuwa kazi kweli kweli. Hebu tulifanyie kazi hili.
 
Anamaanisha lugha ya Kichaga imegawanyika. Kuna kichaga cha Rombo, Maranga, Old Moshi etc. Hizi lugha zote no tofauti na wanaingiliana maneno machache. So unatakiwa kuwa specific unataka awe anajua kichaga cha wapi. Kwa lengo lako hilo nashauri utafute mtu mzima wa makamo anyejua kichaga ashirikiane na huyo mwalimu wa kiingereza/Kiswahili. Maana kwa kiazazi cha kuanzia miaka ya themanini kichaga hatukijui kiundani kivile. Tunajua tu cha kuombea maji.
Shukrani sana wazo lako nimelipokea na nitalifanyia kazi.
 
Hakuna lugha moja ambayo wachaga wote wanaweza kuelewana kwayo.
Kila kipande kina lugha yake,mfano kikibosho sio sawa na kimarangu,kirombo sio sawa na kimachame.
Hivyo hakuna lugha moja rasmi inayoeleweka na wachaga wote
Rombo pia wana lahaja zaidi ya nne tofauti
 
Naelewa vizuri. Mimi nimesoma lugha ya Kijerumani na kuifanyia kazi miaka mingi sana na nimeandika mpa vitabu kwa Kijerumani .Kijerumani pia kina DIALECTS ambazo ukienda kama Bayern (Bavaria) ukakutana na wazee unaweza usielewe wanachoongea. Ila kuna HIGH GERMAN au STANDARD GERMAN inayotumika hata mashuleni ambayo kila mtu ambaye siyo mjerumani anajifunza. Kwenye Kichaga hakuna lugha ambayo tukiongea wote tutaelewana? Maana tukisema watu wajifunze dialects zote itakuwa kazi kweli kweli. Hebu tulifanyie kazi hili.
Kichaga hakuna standard chagga
 
Back
Top Bottom