Mzee Wasira alibainisha hivi karibuni, kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinao wanachama hai wasiopungua milioni kumi na tatu.
Sote tunajuwa hakuna nchi yoyote duniani inayoruhusu chaguzi zake kuwa huru wapiga kura halali wanaojitokeza kupiga kura idadi yao haiwezi kuzidi asili mia 75; kwa hiyo tuseme kwa wana CCM; ambao kweli wamechangamshwa na viongozi wao kupiga kura, wasingeweza kupungua milioni kumi hivi; na hizi zingekuwa ni kura za Samia Suluhu Hassan zenye uhakika kabisa, kutokana na sifa nyingi anazo pewa ndani ya chama.
Hizi ni kura nyingi sana kwa kuanzia, kwa kiongozi yeyote.
Sina uhakika na hili, na sikutaka kutafuta takwimu sahihi; lakini kwa kukadiria tu wapiga kura waliojiandikisha kwenye daftari la wapiga kura haizidi 35 milioni. Wengi wa hawa, ni vijana wanaotafuta vitambulisho tu vya "mpiga kura".
Kwa hiyo tukadirie kuwa wapiga kura halisi wenye sifa za kupiga kura watakuwa ni kama milioni 30 hivi. Katika hawa, ondoa zile kura milioni 10 za wana CCM, ambazo tayari zimo kapuni mwa Samia Suluhu Hassan.
Utabaki na kura milioni 20, nazo ukipunguza wale wasiojitokeza kabisa siku ya kupiga kura, unabaki na kura milioni 15 ambazo zinagombewa na vyama vyote vitakavyo shiriki uchaguzi.
Hata kama CHADEMA wangeamua kushiriki kwenye uchaguzi wasingeweza kupata kura zote hizi za watu milioni 15!
Sasa naomba tuachane na hizo hesabu, ambazo kiuhalisia siyo lengo la mada hii.
Samia Suluhu Hassan, na viongozi wenzie ndani ya CCM, na kwenye serikali yao wanapogomea kufanya marekebisho machache tu, ili uchaguzi uwe angalau wa kuaminika kuwa wa HAKI, hofu yao hasa inatokana na nini? Hawawaamini wanachama wao kuwapigia kura?
Wanaokaza shingo, kwa kiburi tu, wakijuwa kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kusababisha waTanzania kuumizwa na kupoteza maisha; kwa kiburi tu cha kukataa kufanya marekebisho rahisi kabisa; historia itawahukumu vipi kwa ukosefu wa uzalendo wao kwa nchi wanayoiongoza wao?
Yaani ni bora Samia na watu wake wavuruge uchaguzi ili ajihakikishie ushindi kwa kura za wizi kuliko halali, na yote yatakayotokana na wizi huo; kuliko kukubali kufanya marekebisho uchaguzi ufanyike kwa amani!
Kuna nini kisicho eleweka kinacho wafanya wawe na roho ngumu kiasi hiki?
Inawezekana wao wanaujuwa ukweli halisi kuliko tunaoujuwa sisi. Kwamba, hata hao wana CCM wenyewe kura zao ziko kwingine, siyo kwao.