Kama kungekuwa na ligi ya kuachana ningekuwa naongoza kwa kuachwa

Kama kungekuwa na ligi ya kuachana ningekuwa naongoza kwa kuachwa

Status
Not open for further replies.

Digitaldreamer

Senior Member
Joined
Jun 11, 2022
Posts
121
Reaction score
43
Kwa kweli wana JF, mimi nina mikosikatika ishu ya mahusiano.

Mahusiano yangu ya kwanza nilikutana na binti fulani hivi, mzuri sana ni binti la kinyaturu, mwanzoni mambo yalikuwa mazuri kweli, nikasema maisha si ndio haya.

Ni kawa ninaongea naye vizuri kwenye simu, namchatisha sana, kwa kweli nilijiskia amani, huyu anaitwa zuhura.

Baaada ya miezi sita, mambo yakawa yamepamba sana, ukisikia mambo ni [emoji91], ni hatari baaada ya mwezi nikawa nimesafiri mkoa fulani fulani hivi .

Hapo ndo mwanzo wa vituko, mawasiliano yakaanza kudorora ikabidi nimshirikishe my friend ,kuja kukugundua nikachoka mno.

In shortly katika mahusiano yangu ya kwanza, hata nikisikia mtu anataja jina la huyo manzi moyo unapiga paaaaaaaah, muda mwingi nilikuwa na hofu mno, nikijiandaaa kwa chochote, hata wakati wa miadi nilikuwa natetemekaga kweli an.

Nikawa namuomba Mungu kwa sana ,alinde mahusiano yetu, kuja kushangaaa wiki moja baadaye mawasiliano yakawa mabaya nikaona ngoja nikaushe, kwake mimi nilikuwa mgonjwa, nikapiga moyo konde kwa kumuomba samahani, hata kosa lenyewe ,lilikuwa halijulikani,mimi niliomba msamaha ili usukani niushikilie vizuri, muda mfupi baadaye mawasiliano yakawa sawa.

Nilichojifunza kutoka kwa huyu manzi ambapo hata wewe unayesoma huu uzi unatakiwa uwe makini, kuna wanawake ukiingia naye katika mahusiano, maswali hayaishi, unashangaa uko Bize na kazi, hujafanikiwa kumtafuta labda kwa kuonana ana kwa ana au kwenye simu, ukikapata chance kesho yake mtafute anakuja kukuambia mbona umenisusa, nimekutana na wanawake wa namna hii wengi sana.

Upande mwingine anakuwa ana wivu sana, anaanza kupeleleza,ajuwe mahusiano yako yaliopita, unakaaa naye anaaanza kuchomekea vimaswali vya manzi aliyepita, analazamisha kukuona, muda mwingine nampa vitu vizuri mpaka anaaanza kulia.

Daaah nikajiona mimi sasa ndo mwanamme, nilimjali mno, nilijitahidi kumfanya kila nikikutana nae afurahi uwepo wangu, kwa hiyo nilikuwa na amani mno, nikaongeza na percent za uaminifu.

Baada ya miezi kadhaaa mawasiliano yakawa sio mazuri, nikakausha tena miezi kama 4, nikaendelea kutafuta life, muda mwingine nikimpigia hapokei, daaah sijui ndio aliniwekea uchawi gani, mimi kwake nilikuwa nimeoza, huwezi ukaniambia chochote kuhusu yeye, nikarudi tena kuyajenga.

Sasa kinachoniuma ameaniacha kikatili na kaondoka na percent nyingi za upendo, nimetumia miaka kama mitatu hivi katika hii chain ya uhusiano wetu, kuja kukugundua wakati kichwani nawaza ndoa ,yeye anawaza namna ya kunipotezea muda, kuja kugundua kuwa mambo yameeenda vibaya ni too late.

Manzi sjui ndo mnafiki kiasi gani, kwao alikuwa anatoroka kuja kunitafta mimi, na anahakikisha kila siku yuko na mimi, sasa najiuliza kilichomfanya akache ofa yangu ya ndoa ni nini? Au wanawake wengi ndo hawapendi ndoa?

Siku moja nikawa nimempigia nikaongea naye vizuri,nikamuambia namuamini ,tukaaongea namna ya kufanya mahusiano yetu yawe strongly mwisho wa siku nikamsikia anasema ushachelewa ,roho iliniuma sana,nikaona bora nife tuuh.

Nilichokosea katika mahusiano yangu ya kwanza, ni baada ya kuwa na imani sana,kuwa huyu binti alikuwa ananielewa, kumbe yeye alikuwa na mipango yake tofauti, daaah hakuna kinachouma kama kushindwa katika step ya mwisho ya mahusiano .

Nilimpenda kwa asilimia nyingi sana, hiii ni kutokana na kuwa na hamu sana ,kuwa katika ndoa, daaah kumbe nilichokuwa nakipanga kilikuwa ni tofauti,sikuchukua tahadhari yoyote, katika mahusiano yangu, kuna muda kabisa unaona vitimbi vishaaanza ,kichwa changu kilikuwa kimestack wakati ule.

Ile situation ilikuwa ngumu sana katika maisha yangu ,hamu ya kula ikawa imeisha, nikawa ni mwenye hasira sana.

Nimetumia muda mwingi sana kwake, nikajiona niko katika mikono salama,kumbe daaaah kila nikikumbuka, natamani nichukue panga nikafyeke kichwa, wewe mwanamke popote ulipo Mungu anakuona ,kuna siku hutanikumbuka ila utakumbushwa na rafiki yako uwepo wangu.

Nyie acheni tu kama hujawahi kukutana na hali kama hii, mshukuru Mungu ,mimi wakati mwingine natembea naona [emoji93] [emoji93] [emoji93][emoji93] tuuh daaah .

Wana jf mimi sjui ninagundu gani kama kungekuwa na ligi ya kuachana nadhani ningekuwa naongoza kwa kuachwa hawa wanawake hawa [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Nina visa vingi sana vya kuachwa ,yani maumivu juu ya maumivu .

Leo nayo nimewekwa katika list ya kuachwa,Wana jf dua zenu please[emoji120][emoji120][emoji120][emoji24][emoji24][emoji24].

Wanajf nisaidieni hawa wanawake hawapendi ndoa, au ndio nini huwaga natumia rasilimali muda mwingi sana mpaka sielewi nianzie wapi tena je nifanyaje???
 
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]yaani hadi nimekasirika aisee maana nilianza kusoma kwa umakini kutokana na heading lkn content ni mimavi mitupu
Kwenye Heading kaupiga mwingi...we have to give him that...

Hata mm nilijua kitu interesting kutokana na heading😅... kusoma kumbe bure bure
 
Unaachwa sana ndugu. Jichunguze pengine show zako zinaweza kuwa mbovu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom