Shauri dogo ndani ya shauri lilopo sasa hivi linatokana na utata kuwa je mshitakiwa wa pili Adamoo alitoa maelezo yake kwa mujibu wa sheria?
Kuna tashwishi kuhusiana na maelezo ya mshitakiwa huyu kuwa aliteswa au hakuteswa kwenye kupelekea kuwapo kwa maelezo yake.
Je kulikuwa na shinikizo lolote? Je kulikuwa na matumizi ya nguvu? Je kulikuwa na ushawisi wowote?
Je mshitakiwa alitoa maelezo hayo kwa mujibu wa sheria kama inavyoainishwa?
Kumekuwa na wachambuzi uchwara wanao jaribu kulazimisha shauri la uhaini la miaka ya 1980 kufanana na hili. Wakijaribu kuhalalisha matumizi ya mateso kama njia muafaka mno ya kupata maelezo kamili ya njama nzima kutoka kwa washitakiwa.
Ifahamike kuwa mheshimiwa Jaji yuko katikati ya kutafuta ukweli wa namna ambavyo maelezo ya mshitakiwa wa pili yalipatikana.
Akijiridhisha tu kuwa ilikuwa ni kinyume cha sheria, yaani kama mateso, mashinikizo, ushawisi, ghiliba, nk vilitumika na hata labda bila ya maonyo stahiki kutolewa ili kupata maelezo hayo, basi kwa mujibu wa sheria, Jaji atafanya kazi yake.
Ikumbukwe upande wa mashtaka wanahaha kweri kweri kukanusha kuwa watuhumiwa hawakuteswa. Katika hilo wameleta mashahidi watatu wazito kweri kweri.
Sasa kama kuna wachambuzi uchwara wanaoona mateso ni sawa, hii mbona sasa hiyo itakuwa ndiyo kubwa kuliko?