Kama kwa beki zile walifunga ingekuaje leo?

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Kwa beki katili na makini kama kina Sol Campel,Vidic,Ferdinand,Paulo Maldin,Nesta,Zambrota,Chivu,Puyol,Robert Carlos etc ila bado washambuliaji wa kipindi kile Kina Van Neestrol,Rau,Dwight Yorke,Andy Cole,Ronaldo De lima na wengineo walifunga magoli mengi tu.

Ingekuaje kama Washambuliaji hawa wangekua zama hizi za beki jamii ya kina Pique,Umtiti,Smaling,Jones,Cahil,Varane,Ramos,Boateng etc wangeweza kuwika au beki hizi zingeweza kuwazuia?
 
Zilipendwa...... za zamani sana
 
Christian Chief kwanza hakuwa beki. LAKINI hata hivyo, sayansi ya mpira kwa sasa ipo juu sana.

Unaweza ona timu inamiliki mpira 81% lakini inashindwa kupenya na kupata goli. Huu ni ufundi mkubwa japo unaweza kuishia kulalamika kuwa kapaki basi!!!

Mbinu za saaiv ni za kisayansi mno
 
Wasingeonekana kwa mabeki wa sasa, mana mchezo wao ulikuwa wa kawaida tu___kwa lugha nyingine tunasema "wanakabika"

Jitu kama Messi ndio tunasema "ni ngumu kumkaba kwa beki yeyote yule,, hata waje mabeki 10 like nesta na hawataweza kumkaba jini huyu"

Asante sana Messi.
 
Kuna ukweli hapa mkuu mabeki na viungo wakabaji wa zamani walikuwa waakabaji kweli tofauti na siku hizi wengi wana ruka ruka tu.

Vuta picha Messi angekabwa na mtu kama Edger Davis au Patrick Viera kama tungeona hata hizo goli 50 wanazofunga ndani ya msimu mmoja.

Nakumbuka Cristiano Ronaldo aliwahi kukabwa na Cafu mpaka akahama namba na mwisho wa siku akafanyiwa sub kabisa.


Inashangaza sana kuona siku hizi eti beki kama Gerald Pique nae anaingia kwenye kikosi bora cha FIFA. Hakuna mabeki kabisa siku hizi
 
Mkuu game hii naikumbuka hakuwa Cafu nakumbuka alikuwa Genero Gattuso 'katili' (if mistaken on the name spelling correct me). Jamaa alitembea na Ronaldo hadi kahama namba na baadae kutolewa kabisaaa!
 
Mkuu game hii naikumbuka hakuwa Cafu nakumbuka alikuwa Genero Gattuso 'katili' (if mistaken on the name spelling correct me). Jamaa alitembea na Ronaldo hadi kahama namba na baadae kutolewa kabisaaa!
Yeah... Kabisa mkuu, unajua Man u alikutana na AC Millan mara mbili ndani ya misimu miwili na zote man u alitupwa nje.

Sasa ile mara ya kwanza kitu kama 2005 aliyemkaba sana Ronaldo alikuwa ni Cafu baada ya Ferguson kumtoa kushoto sababu ya Maldin. Sasa walivyokutna tena mara ya pili ndio alikuwa ana tembea na Genaro Gattuso na alikuwa anaonekana kwenye kupiga faulo tu.
 
Mpira umebadilika sana sasa hivi watu wanacheza kwa nafasi na timu nzima inashiriki kukaba na ku recover mpira ndo maana mabeki wenye nguvu wanaweza kutokuwa na umuhimu badala yake wakatakiwa mabeki ambao ni flexible sana kama kina Ramos ,Thiago silva, Dani alves , philipo lahm n.k

Zamani hakukuwa na kitu kama false nine lakini kutokana na mabadiliko haya washambuliaji hawakai mbele sana kufukuzana na mabeki bali wanawinda nafasi ndo kitu cha msingi.

Haya yamefanyika baada ya wadau wa mpira kuusoma mpira kwa mda mrefu na kuja na njia mbadala. Kama unaikumbuka barca ya Guardiola utakuwa unanielewa , hii timu ilihenyesha dunia kwa mpira wao na ilikuwa mfano wa kuigwa.
 

Yeah man. Kumbuka pia Messi kaitoa mbali mno barca.bila ya Messi Gadiola asingeonekana.

Messi ni professor
Gadiola ni mwanafunzi.
 
Pumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…