Mtaniwia radhi kidogo. Hawa vijana wa CCM ni mzigo wa hovyo kabisa kwa taifa kwani wana endekeza upumbavu na ujinga.
Hivi wanashindwa kuelewa tofauti ya Chama cha siasa na Taifa (nchi)? Sasa kama watu hao wana akili za namna hiyo wanastahili hata kujadiliana nao jambo lolote kwa ujinga walio nao?
Chama cha siasa mfano CCM au Chadema ni kundi linaloendeshwa kwa hiari kwa misingi ya kiitikadi wanayokubaliana wanachama wake na katiba wanayojiwekea. Huitaki unajiondoa na kujiunga kwingine.
Taifa ndio haki yako ya msingi na ndio sehemu ya uhai wako uliyopangiwa na Mungu na unapaswa kuitetea na kuilinda ili iwe imekubalika na wengi.
Sasa ukiona mjinga wa UVCCM anataka kilinganisha uendeshaji wa Chama na Taifa ni wa kumpuuza maana ni mjinga huyo! Na sio ajabu ndio hao wanadanganywa na mwenyekiti wao kuwa eti nchi hii ina akiba ya fedha za kigeni Bilioni 6,230 $ na wao kama mazuzu wanamshangilia.
Oneni vijana wengine wenye akili wanamhoji mama yenu kuwa kama ni hivyo kwa nini tuwe na madeni? Si alipe tuu yote kwa mkupuo mmoja yaishe? Jee sisi kumbe ni matajiri kuliko hata China?
Wakiona katiba ya Chadema nzuri waje wajiunge, kama mbovu wakae huko huko Mbogamboga ujingani Street.
Katiba Mpya hiyo ni sasa na #HATUPOI