kama kweli kuna watu wamepewa 10%, ni suala la muda tu majina na viwango walivyopewa vitavuja

kama kweli kuna watu wamepewa 10%, ni suala la muda tu majina na viwango walivyopewa vitavuja

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Hii ndio imani yangu kwasababu sio kila mtu anapenda dhuluma, unyonyaji na wizi wa kiwango hiki. Isitoshe, wako ambao watakuwa hawajapata mgao na hawa hawatakii kimya.

Tusisahau pia vita ya kisiasa baina ya wanasiasa wenyewe wa humu ndani kuelekea 2025, hivyo lazima walipuane na wapinzani ndio watapenyezewe siri wazitoe majukwaani na kwenye mikutano na wanahabari.

Pia, wako washindani wa kibiashara wa kimataifa wa ile kampuni inayolalamikiwa ambao nao wnaweza kuingia kazini kutafuta ukweli.

Mwisho, Mwarabu na watu wa Magharibi, wana uadui wa aina fulani, hivyo Mzungu hatawaacha salama ukizingatia yeyen ndio anamikili teknolojia.

Tuhuma hizi ni kubwa mno kupita hivi hivi, kwahiyo ni swala la muda tu.

Time will tell.
 
Wapotezwe kimya kimya kwa kuisingixia korona au changamoto za upumuaji. Kwani wale jamaa sheria ya jinai wakati wa kutekeleza majukumu si inawalinda?
 
Uziwako umeandikwa ktk hali ya kukata Tamaa na kuonesha kuwa huwezi kujipigania, hadi utegemee batle za kibiashara za mzungu na mwarabu, okay mgao ukaanikwa ilihali mkataba ushasainiwa what will it help??
 
Hiyo list nawahurumia sana Wana wao na Wana wa Wana wao katika Vizazi vijavyo

Ndio Matapeli hupendelea kutumia Nickname eg Musukuma, Kibajaj, Sugu, Jah people, Mwamba, Sauti ya Zege, Kinanasi nk

Nawatakia Dominica Njema!
Lissu ameshawalipua.
Uziwako umeandikwa ktk hali ya kukata Tamaa na kuonesha kuwa huwezi kujipigania, hadi utegemee batle za kibiashara za mzungu na mwarabu, okay mgao ukaanikwa ilihali mkataba ushasainiwa what will it help??
Lissu keshawalipua na huu ni mwanzo tu. Endelea kubeza.
 
Zamani wakati Wilbroad Slaa akiwa mtu na nusu kweli kweli alitoa list of shame pale Mwembeyanga. Sasa hivi zaidi ya wiki tatu sasa tunaambiwa kuna waandishi walipelekwa Dubai lakini majina yao hayatajwa popote.
 
Ni hawa akina Mwijaku bwashee 😄😄
 
Nasubiri wabishe afu wamtake Lissu/ Slaa wathibitishe kwa kuwataja majina mmoja baada ya wingine!
 
Back
Top Bottom