Kama kweli mnajiamini mguseni Mtanganyika Dr. Emanuel Nchimbi

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,132
Reaction score
64,416


Salaam Wakuu,

Naomba Dr. Emanuel Nchimbi mumuache afanye kazi. Kwanza udaktari wake wa kusomea so aheshimiwe.

Msimuingize kwenye ugomvi wenu na Ufisadi wenu..

Ameishi kwa heshima kwa kuheshimu wakubwa na Wadogo..

Uroho wenu wa madaraka usiwafanye mumchafue kisa yeye anawalazimisha kutenda mema.

Watanganyika tuko naye bega kwa bega, na tumeona figisu zenu zimeanza..

Dr. Emanuel Nchimbi nakutia moyo. Kaa kimya kama kawaida yako.

Hii Nchi ni ya Wananchi si mali ya mtu mmoja..

Wanaotumwa kukushambulia, wameshindwa kabla ya kuanza..

Fanya kazi zako kwa mjibu wa katiba, usishiriki maovu.

Baada ya kufanya mliyofanya kwa Balozi Humprey Polepole mnafikiri mtaweza fanya kwa Nchimbi pakalike? Vita ya maji maji itapigwa mara ya pili. Jaribuni
 
Baada ya kufanya mliyofannya kwa Balozi Humprey Polepole mnafikiri mtaweza fanya kwa Nchimbi pakalike? Jaribuni
Wameua maelfu watashindwa mmoja?

Mkuu 'figga', hawa siyo watu wa kuwaambia lugha hiyo uliyotumia hapo; haina maana yoyote kwao wakiwa wanajuwa wanao ma-rear Admiral na majenerali na makamishina wa polisi na "Usalama wa waovu" nyuma yao.

Kama Nchimbi kweli analololote la maana; angefanya kazi kubwa huko ndani ya chama chake kilichotekwa toka mikononi mwa hawa waovu.

haya mambo ya kusema tu na kulinda uTanganytika wake huku haonyeshi juhudi zake hata katika chama, haitusaidii sana waTanzania tunaohitaji mabadiliko makubwa ndani ya taifa hili; mabadiliko ambayo CCM hawayataki kwa sababu ya kulinda maslahi yao tu!

huwezi kuwaambia waTanzania wampiganie Nchimbi kwa sababu ya uTanganyika wake tu.
 
CCM wote wameoza hakuna cha Nchimbi wala nani. CHADEMA tusitolewe kwenye reli
 
Kumpinga anayewalazimisha (au anayewataka) CCM wenzake watende haki ni kuwaunga mkono CCM wasiotaka kutenda haki. That’s wrong!
Sijaona chochote anachofanya/alichofanya Nchimbi kuwa tofauti na hao CCM wengine.
hivyo vimanenoneno vya hapa na pale havitoshi kumpambanue yeye na hao CCM wengine..

Akitoka leo na kusimama mbele ya umati wa watu na kuzungumzia maswala muhimu kama katiba na chaguzi huru na za haki, hata mimi leo leo nitaanza kumhesabu katika hilo kundi unalomweka wewe.

hadi hapa sijaona lolote la kumtofautisha na hao wengine.
Yumo kwenye kundi la waovu, na anafaidika na matunda ya uovu ndani ya serikali haramu.
Naye ni sehemu ya tatizo kwa waTanzania kwa sasa hivi.
 
Who cares?

Kwani huyo Nchimbi hakuhusika na mauaji ya Oktoba 29?

Lini amepinga hicho kilichotokea?

Halafu na yeye ni batili tu. Hakuna aliyemchagua awe makamu wa Rais.

Baadhi ya nyie watu hamjielewi kabisa.

Mnawapenda CCM na kuwataka wawatawale au?

Too many imbeciles in this country.
 
Kwani huyo Nchimbi hakuhusika na mauaji ya Oktoba 29?
Hoja ni kupinga kuua watu na kuwapoteza bila kufuata sheria.. Wasimteke, kumuua wala kumpa sumu.. Though Nchimbi hakuwa na Mamlaka yoyote kipindi hicho.. Alikuwa kama wana ccm wengine.

Siwezi kukubali kuona Watanganyika wananyanyaswa au kuuliwa hata kama ni itikadi tofauti.
 
Nchi keshawahi kukemea mauaji yaliyofanywa na bosi wake?
 
Hakuna kitu kitaiua CCM haraka kama Utanganyika vs Uzanzibari. Na hapa ndipo panaogopwa zaidi na Samia.
 
Mungu atasimama penye haki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…