Dialogist
JF-Expert Member
- Apr 14, 2014
- 1,167
- 1,872
Wanabodini Mlimakafu??
Mimi ni mpenzi wa siasa za maendeleo zaidi na sio za kiharakati. Wakati huo napenda siasa za kisomi kweli kweli..
Nimekaa nikatafakari baada ya kuisha uchaguzi wa Chadema, nimeona mwaka huu kama hawatapata urais basi watakua na wabunge wengi zaidi bungeni (over 50%) of all...
Hili linachagizwa na mambo kadhaa yafuatayo...
1. Kuongezeka kwa umaarufu wa Chadema kipindi hiki hasa wakati na baada ya uchaguzi, hivyo kupata wafuatiliaji wengi.
2. Ushindi wa Tundu Lissu ambao kwa namna fulani umerudisha chama katika ule mstari wa zamani na hivyo kurejesha matumaini ya watanzania kupata mtu sahihi wa kuwatetea na kuwasemea katika mamlaka mbalimbali. Wengi tumeona wakiwa na shauku ya kujiunga na chama hiki.
3. Kuwepo kwa vijana wengi mtaani ambao hawana ajira na wana elimu na ufahamu wa kutosha juu ya kila jambo linaloendelea nchini. Na hii inachagizwa na ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano. Hivyo Chadema wakichanga karata vizuri wakaandikisha vijana wengi kwenye chama na hatimae kwenye daftari la wapiga kura basi wamelamba dume. Zinangatia vijana wengi ni wa kuanzia 2000 kupanda juu ambao wamekuta chadema ipo on peak na wanamjua Lissu vyema.
4. Kuongezeka kujitambua kwa watu mbalimbali hasa kwa kufahamu na kuelewa madhara ya rushwa. Hivyo wanaweza kuamua kula rushwa lakini wasikuchague.
Rejea uchaguzi wa TLS (fununu) Uchaguzi wa Bavicha na hata huu uchaguzi mkuu wa Chadema (fununu). Hilo kupelekea hata kama tukiingia uchaguzi mkuu, mgombea yoyote akitumia rushwa inaweza kula kwake.
Na sababu nyingine kadha wa kadha..
Welcome on board for discussion.
#TANZANIA KWANZA, TUTAILINDA NA KUITHAMINI