N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 8,308
- 12,812
Najua hii ni hoja nzito, lakini hebu tujitafakari.
Tunajivunia kuwa taifa la waumini.
Makanisa na misikiti vimejaa.
Lakini je, maisha yetu yanaendana na yale tunayoyaamini?
Kila siku tunaona na wakati mwingine kushiriki katika:
Cha kushangaza ni kwamba karibu kila anayefanya hayo hujitambulisha kuwa Mkristo au Muislamu.
Ikiwa Mungu angehukumu leo kwa matendo badala ya majina ya dini zetu, je, kweli Watanzania wengi tungekuwa na uhakika wa Pepo?
Au ukweli mchungu ni kwamba wengi wetu tungejikuta upande mwingine wa jehanamu?
Hoja yangu ni kwamba kujitambulisha na dini si tiketi ya Pepo; kinachopimwa ni mwenendo wa maisha.
Kama umetembelea nchi kadhaa duniani utagundua wabongo tuna dhambi nyingi sana hasa hii ya kutokuwa honest/frank/aka unafik/unafiquna/.
Utafiti wangu unaonesha tatizo letu kubwa la dhambi ni:
1. Uzinzi
2. Roho mbaya
2. Uongo na
3. Rushwa
Je, unakubaliana au unapinga?
Kwa nini?
Povu ruksa, wafia dini someni sledi vizuri!!

- Rushwa.
- Uongo na ushahidi wa uongo.
- Wizi wa mali za umma na binafsi.
- Ufisadi.
- Uzinzi na kuvunja ndoa.
- Chuki, fitina na kusengenya.
- Dhuluma dhidi ya wanyonge.
- Kutoruhusu watu wavuke pundamilia.
- Usengenyaji.
- Kutapeli na kula haki za wengine.
- Unafiki—kuonekana watakatifu hadharani lakini kuishi maisha tofauti faraghani (hili kwa utafiti wangu ni tatizo kubwa).
- Nk