dubu
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 3,502
- 3,483
Salaam Wakuu,
Mwezi wa nane chama cha Wanasheria Tanganyika (Tanganyika Law Society - TLS) wanafanya Uchaguzi wa kumchagua raisi wao na Viongozi wengine.
Kitu ambacho kimewashangaza wengi, ni kukatwa kwa jina la Wakili Mwabukusi asigombee Urais wa TLS kwasababu eti anawavunjia heshima Viongozi wa Juu wa Serikalini. Hivyo hafai kuwa Raisi wa TLS.
Lakini inadaiwa kwamba Taasisi ya Raisi Tanzania imetia mkono wake kwenye uchaguzi huu kiasi kwamba tangu Uhuru, Raisi hajawahi kufungua Mikutano yao, lakini Safari hii Raisi Samia anategemea kuwa Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa TLS.
Baada ya Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), kumuengua Boniface Mwabukusi katika kinyang’anyiro cha kuwania urais wa chama hicho, wakili huyo ametangaza kusudio la kwenda mahakamani.
Sambamba na hatua hiyo, amewataka wanachama wengine wa TLS kutoshiriki uchaguzi huo, ili kuishinikiza Kamati ya Uchaguzi iwarejeshe wagombea wote iliowaengua.
Je, Mwabukusi ni nani na ana Mahusiano gani na Serikali hadi imuone ni tishio?