Kama kweli unamchukia Hayati Magufuli fanya haya utuachie tunaompenda

Kama kweli unamchukia Hayati Magufuli fanya haya utuachie tunaompenda

Alijenga kwa pesa zetu!
Kwa Tanzania Rais/kiongozi akitumia pesa zetu kwenye maendeleo hiyo ni big step ni bahati kubwa sana
kwasababu wengi wao wanatumia pesa zetu kunenepesha matumbo yao tu!
Kwahiyo kipindi tunamkejeli kuwa JK alikua fisadi je hakuwa amejenga barabara nchi nzima, hakuwa amejenga terminal 3? Hakuwa ameleta umeme wa gesi au hakuwa amesambaza maji ya ziwa Victoria? Hakuwa amejenga UDOM na mloganzila?

Ubaya wa uongozi hauna uhusiano na miundombinu uliyojenga. Leadership is software rather than hardware
 
Mfano yule chura nimuheshimu kwa lipi hasa? Labda kwa kunipita umri, ana kera sana.
Usipite na gari lako Kijazi interchange.

Kwa wanao toka Mbezi kuelekea kariakoo na Posta pitia njia ya Goba au maji chumvi.

Fanya hivyo boss utakua na amani.

Tuache kudharau viongozi wetu tusitukane tuwaheshimu wote.

Kama unaona unakereka na uongozi wa kiongozi yeyote jenga hoja njoo na data kuliko kutukana viongozi njoo na data
 
Watu kama nyie ndio matatizo ya hili Taifa..., Hakuna Mradi wa JPM wala Samia kwahio yoyote aliyefanya vitu kwa Kodi zetu ni kwamba aliwajibika wala hakuna sababu ya kumsifia na anayelaumu analaumu kwa mapungufu aliyofanya sababu ni haki yake kama mlipa Kodi....

Kwahio muda wa kusifia tungekuwa tunautumia kulaumu wasiofanya huenda wangefanya..., By the way sikubaliani na wanaopambana na marehemu wakati kinachoendelea sasa kinawapita....
 
Bwana Pombe alikuwa ana mapungufu kibao ambayo yalitukera sana, lakini pamoja na hivyo kuna uthubutu alikuwa nao ambao hata watangulizi wenzake na huyu tuliyenae sasa hawana kabisa... nafikiri kwenye awamu yake watu wengi ndio walianza kufuatilia kwa ukaribu nini kinaendelea kwenye rasilimali zetu, huko nyuma ni kama vile wabongo walikuwa wameshaisusa nchi yao na hawataki hata kujua ni nini kinaendelea, ila alipokuja yeye ni kama kuna awareness na shauku fulani hivi aliwatengenezea watanzania ambayo ilikuwa ni hatua nzuri sana kuelekea kwenye uzalendo uliokomaa.

Sema kwa sababu nchi yenyewe imejaa wezi,wala rushwa,mafisadi na wapenda shortcuts kwa hiyo yeye kuchukiwa na watu mpaka sasa hilo ni suala tarajiwa.
 
Usipite na gari lako Kijazi interchange.

Kwa wanao toka Mbezi kuelekea kariakoo na Posta pitia njia ya Goba au maji chumvi.

Fanya hivyo boss utakua na amani.

Tuache kudharau viongozi wetu tusitukane tuwaheshimu wote.

Kama unaona unakereka na uongozi wa kiongozi yeyote jenga hoja njoo na data kuliko kutukana viongozi njoo na data
Hayo yoge unayoyasema ni plans za kikwete. Jpm hakuna alivhojenga hata kimoja labda kuteka na kuua tu
 
Aliyejenga mlima Kilimanjaro, aliyechimba bahari ya Hindi, aliyechimba ziwa Victoria, nyasa na Tanganyika, na kuyakabidhi Kwa wanadamu wa TANGANYIKA, awekwe kundi gani? Acha kusujudia binaadamu, Magufuli hana tofauti yeyote Ile nawewe.
 
Shida nini mkuu siku hizi reasoning yako ina plummet? Ni sawa na kusema kwakuwa Nyerere alipinga wakoloni basi akavunje Reli ya kati, akavunje UDSM, akavunje bandari n.k? Ubaya wa JPM ni leadership style sio barabara.

Kwani Mandela kipindi anakataa makaburu hawakuwa wamejenga barabara nchi nzima? Very poor reasoning.

JPM anapingwa kwa udikteta wake kama ambavyo Hitler licha ya maendeleo makubwa aliyowaachia ujerumani, anakumbukwa kwa udikteta wake.
Katika utawala wa kidikteta wa Hitler zilijengwa autobahn moja ya miundombinu bora sana ya barabara inayompa dereva uhuru wa kuendesha kwa mwendokasi mkubwa.

Ila haimpi sababu ya kufuta udikteta na ukatili aliokuwa nao.

Maana hata miundombinu hakujenga yeye bali wananchi kwa nguvu zao na mateso makali.
 
Magufuli nilimpenda sana, ilivyotangazwa amefariki nilishindwa kula na kulala
Nililia muda wote tangu alipotangazwa amefariki mpaka kuzikwa kwake, na hata leo ninaporudia kuangalia matukio ya msiba wake, wale wajeda na kina mama, wazee kwa vijana walivyokuwa wakishindwa kujizuia, huwa inanitoa machozi

Nilimkubali sana yule mzee, na hakika yangu, haijatokea kiongozi niliyewahi kumkubali na sijui kama atatokea tena kama yule mzee

Ila Mungu ni mwema, asikie kilio cha wote wanaonyanyasika na mabwanyeye ya CCM
 
"Na Mimi nataka niseme Watanzania mtanikumbuka na mtanikumbuka kwa mazuri na si kwa mabaya kwasababu nimesacrifice maisha yangu kwa wananchi masikini"
Umaskini siyo sifa, na ukiona mtu anajivunia watu maskini basi ujuwe ndio mtaji wake umaskini hautakwisha.

Nchi haijengwi na maskini, nenda TRA kaangalie takwimu za walipa kodi ni watu gani.
 
Hiatoria ya mambo aliyofanya Magufuli kwa nchi hii, kujitoa na kujenga miundombinu mingi na ya mhimu, kufufua matumaini ya nchi yetu kuwa na mwelekeo wa kuondokana na umasikini, kulinda rasilimali kwa nguvu zote, kukemea majizi na kila aina ya uovu, kupiga vita rushwa, madawa ya kulevya na ushogha tena hadharani bila kuogopa, kutoipiga lockdown nchi yetu kipindi cha korona

Hiyo tu inatosha kuwa ni historia isiyofutika kwa wepesi masikioni mwa Watanzania wema
 
Usipite na gari lako Kijazi interchange.

Kwa wanao toka Mbezi kuelekea kariakoo na Posta pitia njia ya Goba au maji chumvi.

Fanya hivyo boss utakua na amani.

Tuache kudharau viongozi wetu tusitukane tuwaheshimu wote.

Kama unaona unakereka na uongozi wa kiongozi yeyote jenga hoja njoo na data kuliko kutukana viongozi njoo na data
Wape wape facts
 
Shida nini mkuu siku hizi reasoning yako ina plummet? Ni sawa na kusema kwakuwa Nyerere alipinga wakoloni basi akavunje Reli ya kati, akavunje UDSM, akavunje bandari n.k? Ubaya wa JPM ni leadership style sio barabara.

Kwani Mandela kipindi anakataa makaburu hawakuwa wamejenga barabara nchi nzima? Very poor reasoning.

JPM anapingwa kwa udikteta wake kama ambavyo Hitler licha ya maendeleo makubwa aliyowaachia ujerumani, anakumbukwa kwa udikteta wake.
Akili hii ni ndogo kabisa!

Unaweza kutuambia udikiteta wa Hitila hapa na mapana yake, halafu ukatwambia udikiteta wa Magufuli unahistoria na kukubalika hivi katika nchi ngapi duniani?

Inapotajwa orodha ya madikiteta Duniani, Magufuli yupo au chuki za kijinga tu?

Udikiteta unaozuia maliasili za nchi kuibiwa, huo ni udikiteta mzuri na unafaa sana

Udikiteta unaowaondoa kazini wajinga na waliokuwa wakifanya operations za kichwa badala ya mguu huo ni udikitea bora sana
 
Back
Top Bottom