Kama kweli Waziri Bashe katoa kibali cha kuagiza Sukari kwa kampuni ya simu, hii haitakuwa na tofauti na Ufisadi wa Lowassa Richmond

Sisiemu nyumba ya Kufuga MAJIZIII....
Hapana kuna majizi yanajifichia humo.

Yanaharibu uchumi wa nchi, yanaharibu sifa ya chama.

Wahuni wachache tu ambao kizalendo wanapaswa kufutwa.
 
Nimeona kupitia Jambo TV Mh. Mpina akidai Waziri Bashe ametoa Kibali kwa kampuni ya simu ya Itel yenye mtaji mdogo kuagiza Sukari ya Tsh. Billion 6.6.

Hii inanikumbusha jinsi Hayati Ndesamburo alivyosema Stationary iliyopo pembeni ya hotel yake pale Mnazi mmoja ndio imejigeuza kuwa Richmond na kuingia mkataba na TANESCO.

Scandal ya Richmond ilimstaafisha Waziri Mkuu wa wakati huo enzi za Spika wa Spidi na Viwango Mzee Sitta.

Nawatakieni Dominica njema 😀.
Biashara siyo "Mtaji wa Hela" ila ni "mtaji wa akili" kuna mzungu anakuja na makaratasi tu kuwekeza Tz,vingine vyote vya kuwekeza anavikuta hapa hapa bongo ,ikiwemo mitaji. harafu tunasema serikali imeongeza FDI,kwa sababu makampuni yamesajiriwqa Ulaya
 
Nikiangalia Tanzania ilivyokubwa, ilivyo na mapori yaliyojaa rutuba, nikiangalia vijana wanavyouza pipi mjini unabaki unajishangaa mwenyewe.

Mfano.

Serikali itafute muwekezaji, harafu huyo muwekezaji apew fungu aende kijijini wawakopeshe vijana kwa kilimo cha miwa, harafu kampuni ikainunue hiyo miwa harafu wakate deni lao, sidhani kama watu wangepoteza muda kwa kuuza karanga mjini
 
Hapana kuna majizi yanajifichia humo.

Yanaharibu uchumi wa nchi, yanaharibu sifa ya chama.

Wahuni wachache tu ambao kizalendo wanapaswa kufutwa.

Wahuni wapo ccm, watoto wa mjini wapo ccm, mafisadi wapo ccm

kwa kashfa hii huyo waziri bado tu hajajiuru? Ukiona hvyo ni mchongo ht ikulu wanajua na wana maslahi yao
 
Bashe mfuasi na mwanafunzi wa Lowasa kwenye Kila kitu , hakika ameiva kwenye Ufisadi
 
Il
Nimeona kupitia Jambo TV Mh. Mpina akidai Waziri Bashe ametoa Kibali kwa kampuni ya simu ya Itel yenye mtaji mdogo kuagiza Sukari ya Tsh. Billion 6.6.

Hii inanikumbusha jinsi Hayati Ndesamburo alivyosema Stationary iliyopo pembeni ya hotel yake pale Mnazi mmoja ndio imejigeuza kuwa Richmond na kuingia mkataba na TANESCO.

Scandal ya Richmond ilimstaafisha Waziri Mkuu wa wakati huo enzi za Spika wa Spidi na Viwango Mzee Sitta.

Nawatakieni Dominica njema 😀.

=====

Pia soma: Luhaga Mpina amshukia Waziri Bashe, adai amelidanganya Bunge, awataja Magufuli, Rais Samia
ULe mradi wa bbt tangu mwanzo ulionyesha kuwa hakuna accountability kwenye kulinda maslahi ya umma
 
Nikiangalia Tanzania ilivyokubwa, ilivyo na mapori yaliyojaa rutuba, nikiangalia vijana wanavyouza pipi mjini unabaki unajishangaa mwenyewe.

Mfano.

Serikali itafute muwekezaji, harafu huyo muwekezaji apew fungu aende kijijini wawakopeshe vijana kwa kilimo cha miwa, harafu kampuni ikainunue hiyo miwa harafu wakate deni lao, sidhani kama watu wangepoteza muda kwa kuuza karanga mjini
Kilimo siyo rahisi hivyo. Na vijana wajua kilimo hakilipi ndo maana wamekomaa kukaa mijini. Kilimo kinatakiwa kuendeshwa na wakulima wakubwa wachache tu; Serikali ikwapa ruzuku ya kutosha ili bei ya chakula isipande sana. Then, kundi kubwa libaki mijini kwa ajili ya kuchaka mazao ya kilimo, kiyasambaza na kuyachuuza. watu wengi kuwa kweli kilimo ni dalili ya umaskini uliokirithiri wa nchi.
 
KUsema ati

Samia hajui na dili ya Trillion, ni uongo, Samia anajua ila wapiga dili ndiyo wameshindwa kuifanya ili ifichike; haya mambo ya kusema Rais huwa hajui ni uongo. Sukari imeangusha wengi sana sasa useme bashe alifanya bila idhini ya juu ni uongo. Hata uagizji kwa hizo gharama kwa aanchi masikini kama Tanzania waziri wa fedha na Rais wanatakiwa wajue. Sukari inanunuliwa kwa dollar.
Na hii inatuumiza sana kiuchumi ,kuanzia maisha ya mtu mmojammoja Hadi kwenye level ya nchi nzima ,hivi TISS mbona wanafumbia macho hili swala hata makanisa na misikiti kwanini wasihubiri hii kitu mbona nchi inaingizwa mkenge hivihivi
 
Hapana kuna majizi yanajifichia humo.

Yanaharibu uchumi wa nchi, yanaharibu sifa ya chama.

Wahuni wachache tu ambao kizalendo wanapaswa kufutwa.
Unaamini miamala ya mabilioni inaweza kufanywa serikalini bila Hazina, BOT na Ikulu kuwa na taarifa rasmi? Seriously?
 
Kilimo siyo rahisi hivyo. Na vijana wajua kilimo hakilipi ndo maana wamekomaa kukaa mijini. Kilimo kinatakiwa kuendeshwa na wakulima wakubwa wachache tu; Serikali ikwapa ruzuku ya kutosha ili bei ya chakula isipande sana. Then, kundi kubwa libaki mijini kwa ajili ya kuchaka mazao ya kilimo, kiyasambaza na kuyachuuza. watu wengi kuwa kweli kilimo ni dalili ya umaskini uliokirithiri wa nchi.
Sawa. Kungekuwa na uwekezaji mwingi kwenye kilimo cha mashamba makubwa (estates) na kampuni za kilimo kuundwa kungekuwa hata na ajira nyingi za maana kuliko hizi biashara za kipuuzi zilizoenea mijini.

Nchi finyu kama Israel zina-import vibarua wa mashamba. Pia wengi wanaokimbilia Ulaya na US wanaenda kwenye kazi kwenye estates za kilimo.

Tungefanya hapa kwetu, kwa ardhi kubwa na mito tuliyo nayo, tungeimarisha sana uchumi. Tuna mifano ya estates chache zinazoajiri wafanyakazi wa aina mbalimbali hapa kwetu. Kuna moja inamilikiwa na mzungu kule Iringa. Hakuna namna wasomi wa Tanzania waweze kukusanya mtaji na kufanya uwekezaji wa kilimo cha estates?

Serikali makini inatarajiwa ku-promote za shughuli aina hiyo badala ya hizi porojo zinazoendelea kutaka vijana graduates waanzishe vigenge vya kuuza nyanya au wawe bodaboda, n.k. Eti ndio fursa hizo: “wasibweteke na kuchagua kazi”! Kuna kitu hakiko sawa kabisa katika uongozi wa nchi hii.
 
Nimeona kupitia Jambo TV Mh. Mpina akidai Waziri Bashe ametoa Kibali kwa kampuni ya simu ya Itel yenye mtaji mdogo kuagiza Sukari ya Tsh. Billion 6.6.

Hii inanikumbusha jinsi Hayati Ndesamburo alivyosema Stationary iliyopo pembeni ya hotel yake pale Mnazi mmoja ndio imejigeuza kuwa Richmond na kuingia mkataba na TANESCO.

Scandal ya Richmond ilimstaafisha Waziri Mkuu wa wakati huo enzi za Spika wa Spidi na Viwango Mzee Sitta.

Nawatakieni Dominica njema [emoji3].

=====

Pia soma: Luhaga Mpina amshukia Waziri Bashe, adai amelidanganya Bunge, awataja Magufuli, Rais Samia
Soma vizuri bwashee sio bilioni sita tu ni mabilioni ya sh

"3.3.1 ITEL EAST AFRICA LIMITED ambaye Bodi ya Sukari ilimuandikia barua yenye Kumb. Ref. No. SBT/DGO/09/VOL.II/2-10 ya tarehe 2 Januari 2024 iliyosainiwa na Lusomyo Buzingo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Bodi wa Sukari ikiitarifu kampuni hiyo kuwa Serikali imeidhinisha kuingiza tani 50,000 za sukari (Kiambatisho Na. 14).

Lakini tarehe 9 Januari 2024 na tarehe 30 Januari 2024 Kampuni ya ITEL ilipewa vibali vya kuingiza tani 60,000 za sukari zaidi ya kiwango ya kiwango kilichoidhinishwa kwenye barua rejea kibali SR Na. 8652445335 na 944600548 (Kiambatisho Na. 15)

Pia vibali alivyopewa ITEL ni zaidi ya viwanda vyote vitano ambavyo jumla vimepewa tani 50,000 tu kwa maana ya tani 10,000 kila kiwanda.

Baada ya kufanya upekuzi wa BRELA tarehe 10 Juni 2024 (Kiambatisho"
 
Sawa. Kungekuwa na uwekezaji mwingi kwenye kilimo cha mashamba makubwa (estates) na kampuni za kilimo kuundwa kungekuwa hata na ajira nyingi za maana kuliko hizi biashara za kipuuzi zilizoenea mijini.

Nchi finyu kama Israel zina-import vibarua wa mashamba. Pia wengi wanaokimbilia Ulaya na US wanaenda kwenye kazi kwenye estates za kilimo.

Tungefanya hapa kwetu, kwa ardhi kubwa na mito tuliyo nayo, tungeimarisha sana uchumi. Tuna mifano ya estates chache zinazoajiri wafanyakazi wa aina mbalimbali hapa kwetu. Kuna moja inamilikiwa na mzungu kule Iringa. Hakuna namna wasomi wa Tanzania waweze kukusanya mtaji na kufanya uwekezaji wa kilimo cha estates?

Serikali makini inatarajiwa ku-promote za shughuli aina hiyo badala ya hizi porojo zinazoendelea kutaka vijana graduates waanzishe vigenge vya kuuza nyanya au wawe bodaboda, n.k. Eti ndio fursa hizo: “wasibweteke na kuchagua kazi”! Kuna kitu hakiko sawa kabisa katika uongozi wa nchi hii.
Hii nchi ngumu. Ni hadi hapo Mfumo wa uatawala utakapobadilika. Lakini kwa Serikali ya Chama kile kile tangu uhuru tusitegemee makubwa hata baada ya miaka 50 ijayo.
 
Wagalatia mtahangaika sanaaaaa
Mama ni mpaka 23000000 hukoooooo,
Tunajua hata iweje hamuwezi kumsifu wa huku, ila wa kule hata liboronge vipi bado mtasifia
Ila safari hii tunapiga kazi tu na hayo maneno yenu semeniiii, mkichoka mtalala
 
Back
Top Bottom