Kama kweli we ni mhenga nitajie jina la mmojammoja

nakumbuka vurugu za zena na betina enzi hizo duuh ulikuwa ukilikosa gazeti la sani basi unanyongeka sana..maana utasikia kijiweni watu wanavyosimulia yalohili katika gazeti....ndumila kuwili nae na mishe mishe zake daaa

Kuna story yake moja alikuwa anakimbizwa na wananchi basi akiwa katika speed ile ya 150kph yaani mguu moja kisigino kinagusa kisogoni na mguu mwingine goti linagusa kidevuni jamaa alinichekesha sana pale aliposema nimewahi kukwepa matone ya mvua sembuse hayo mapanga?
 
Hii ni picha kutoka hili tolea la sasa lililokua linatolewa hivi majuzi kati alafu likapotea tena ghafla, wachoraji wa hizi picha siyo wale original
 

Dah... Yaan zamani ilikuwa raha sana kusoma gazeti, tena unatunza matoleo yote, unafatilia ndondi za Zena na Betina.. Acha kabisa
 
Kwema shem,habari ya siku nyingi
Namshukuru Mungu nipo vizuri kabisa...

Wewe ni mmoja wa wahenga ? Mimi nilikuwa shabiki wa timu ya kijijini kwetu tukiwakilishwa vilivyo na akina Kobelo,Huhihuhi,Ugimbi,Mzee Meko,komredi Kp na wengineo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…