Kama Kweli Wewe ni Shabiki wa Simba, basi kata Tiketi yako mapema, wa kumzuia Elie Mpanzu pale Al Masry, Hii tumevuka

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
473
Reaction score
1,682
Kwa namna mabeki wa Al MAsry wanavyocheza na kwa aina ya uchezaji wa Elia Mpanzu Kibisawala na pacha wake KIbbu Dennis, hakyamungu waarabu kesho kazi ipo.

Na kama hakutakuwa na figisu kutoka kwa jamaa yetu pale uwanjani ambaye anajifanya hana uzalendo basi kesho ni wimbo tu kuanzia nje ya uwanja hadi nyumbani kwetu Tandale.

Yaani kesho ni mwendo wa kuwapelekea moto mwanzo mwisho, hakuna kurudisha mpira nyuma wala nn, tahadhari zote za eneo la hatari wachezaji wetu wajiepushe nazo maana kutakuwa na VAR na waarabu wataomba sana VAR iangalie matukio yao.

Najua kesho jamaa zetu wa Utopolo wataomba tuharibikiwe ili wao wafurahi na tunajua mipango yote wanayoifanya, Ahmed Ally kashasema kama unataka kuharibikiwa basi chezea gemu ya kesho, na kweli kwenye vilinge vyangu nimeona, kila nikipima kwenye vipimo vyangu naiona sumu kali sanaaaa, yaani mambo yaliyoyafanyika kesho hayana kipimo.

Mtu yeyote anayekwambia kesho hakuna furaha achaneni naye, huyo sio mwana simba, huwezi kuwa mwana simba tuko vitani, unaanza kulalamikia na kuponda mikakati na mipango ya kivita, huo ni usaliti.

Mimi pia sikufurahishwa na yaliyotokea kule Misri kufungwa na timu mbovu kabisa, hatukuwa na sababu yoyote ya kuifanya gemu ya kesho kuwa ngumu lakini nimenyuti kwanza, nawatia moyo wachezaji hadi mechi ya kesho iishe ndio nitatoa maoni yangu ya kikatiba.

Shime shime, kata tiketi yako mapema, hii tunavuka.Wa kumzuia Elie Mpanzu Kibisawala sijamuona hiyo kesho.
 
Nafasi ya Mpanzu na Kibu D mechi ya kwanza alicheza nani na nani baada ya wao kutokuwepo?
 
Simba inapaswa kuongeza si chini ya wachezaji watano Msimu ujao.

Quality player wachezaji wa Fainali ya CCL na sio hawa wachwzaji wa Makundi na ndondo.

Ukweli mchungu.
 
Kwa namna mabeki wa Al MAsry wanavyocheza na kwa aina ya uchezaji wa Elia Mpanzu Kibisawala na pacha wake KIbbu Dennis, hakyamungu waarabu kesho kazi ipo.

Na kama hakutakuwa na figisu kutoka kwa jamaa yetu pale uwanjani ambaye anajifanya hana uzalendo basi kesho ni wimbo tu kuanzia nje ya uwanja hadi nyumbani kwetu Tandale.

Yaani kesho ni mwendo wa kuwapelekea moto mwanzo mwisho, hakuna kurudisha mpira nyuma wala nn, tahadhari zote za eneo la hatari wachezaji wetu wajiepushe nazo maana kutakuwa na VAR na waarabu wataomba sana VAR iangalie matukio yao.

Najua kesho jamaa zetu wa Utopolo wataomba tuharibikiwe ili wao wafurahi na tunajua mipango yote wanayoifanya, Ahmed Ally kashasema kama unataka kuharibikiwa basi chezea gemu ya kesho, na kweli kwenye vilinge vyangu nimeona, kila nikipima kwenye vipimo vyangu naiona sumu kali sanaaaa, yaani mambo yaliyoyafanyika kesho hayana kipimo.

Mtu yeyote anayekwambia kesho hakuna furaha achaneni naye, huyo sio mwana simba, huwezi kuwa mwana simba tuko vitani, unaanza kulalamikia na kuponda mikakati na mipango ya kivita, huo ni usaliti.

Mimi pia sikufurahishwa na yaliyotokea kule Misri kufungwa na timu mbovu kabisa, hatukuwa na sababu yoyote ya kuifanya gemu ya kesho kuwa ngumu lakini nimenyuti kwanza, nawatia moyo wachezaji hadi mechi ya kesho iishe ndio nitatoa maoni yangu ya kikatiba.

Shime shime, kata tiketi yako mapema, hii tunavuka.Wa kumzuia Elie Mpanzu Kibisawala sijamuona hiyo kesho.
Kule kwenye ID ile unaanzisha nyuzi za kuponda na kukatisha tamaa wenzako, huku unaanzisha nyuzi za kizalendo.
 
Back
Top Bottom