GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Ikumbukwe kuwa alipelekwa Singida United na Simba SC kwa mkopo ili akakuze Kiwango chake na kama kikiwa juu kama huko nyuma basi Uongozi utamrudisha Kikosini. Nimetoka kuwasiliana na Mchezaji muhimu sana wa Simba muda si mrefu akiwa huko huko Nakuru ( jina nalihifadhi ) na kuniambia kwamba jana Yeye pamoja na Wenzake ( Wachezaji wa Simba SC ) walimwambia Peter Manyika jr kuwa ahakikishe leo ' anakaza ' mno ili kuweza kuwashawishi Viongozi wa Simba SC ili arudi Kikosini na aweze kusaidiana na Kipa namba moja Aishi Manula.
Na kwa taarifa za hivi punde tu na ambazo tayari nimeshahakikishiwa na chanzo changu kingine kilichopo ndani ya Simba SC kinasema kwamba Kipa Peter Manyik jr anarudi Kundini Simba SC na Kipa Said Nduda ataachwa.
Kama Manyika akirudi Simba SC itakuwa jambo jema kwani atampa changamoto sana Manula na Simba SC haitokuwa na wasiwasi au hofu yoyote na Makipa na Timu itakuwa nzuri zaidi.
Nawasilisha.