Kama labda unajiuliza kwanini Kipa Peter Manyika Jr leo anadaka sana jibu ni hili...

Kama labda unajiuliza kwanini Kipa Peter Manyika Jr leo anadaka sana jibu ni hili...

Watu wote wanaomchukia na kumsema vibaya Kocha wa Simba SC Mfaransa Pierre Lechantre hawajui mpira halafu ni ' Wapuuzi ' hakuna mfano. Ndiyo maana kuna muda mwingine huwa naamua tu kunyamaza na kuwaangalia tu Watu ambao hata a,b,c's za mpira hawana na hawajui.

Leo hii kila ' Mpuuzi ' anasema Timu apewe Masoud Irambona Djuma huku wakimsifu kuwa ndiyo anaiwezea Simba na anajua kufundisha. Ili uone kuwa Wapenzi wa mpira wa Simba SC kama si Tanzania kwa ujumla baadhi yao ni ' Wapuuzi ' hawa hawa ambao leo hii wanampigia ' Chapuo ' Djuma apewe Timu ndiyo hawa hawa wakati Simba SC imefanya vibaya katika Kombe la Mapinduzi kule Zanzibar ndiyo walikuwa mitandaoni wakimtaka aondolewe au awe chini ya Kocha Mkuu.

Hivi kwa Mtu anayeujua kweli mpira ' Kindakindaki ' anaweza kuthubutu kumfananisha Lechantre na Djuma? Hivi Djuma ana CV ya hata kuifikia robo ya CV ya Lechantre? Kuna kuna Mwafrika yoyote mfuatiliaji wa Mpira ambaye leo hii hajui uwezo mkubwa alionao Lechantre? Kuna vitu vingine huwa vinatia hasira hadi Mtu unakosa hata uvumilivu.

Wanaojua mpira huangalia Kwanza matokeo ya Uwanjana na aina ya Uchezaji wa Timu huja baadae na wala siyo Kipaumbele sana kwani Timu haiwi Bingwa kwa kucheza ' Sexy Football ' badala yake Watu hutaka matokeo na Vikombe pekee kitu ambacho Simba SC imefanya safari hii.

Upuuzi huu wa kutaka Simba SC icheze mpira wa Kitabuni pekee ndiyo umeigharimu hata Klabu ya Arsenal ambayo kwa mpira wake huo wa ' Kuburudisha ' Watazamaji sasa ina miaka ya Umri aliona mdogo wangu wa Kike wa miaka 22 kama sijakosea bila kuchukua Kombe ya EPL huko Uingereza.

Sioni sababu yoyote ya Kocha Pierre Lechantre ' Kufukuzwa ' Simba SC na badala yake nadhani sasa huyu Kocha apewe Mkataba mrefu ili aitengeneze Simba yetu Kimataifa zaidi. Halafu Kocha Djuma ' aonywe ' haraka aache tabia yake ya kupika ' majungu ' kwa baadhi ya Wachezaji ' Waandamizi ' wa Simba SC ili ' wachomeshe ' akishirikiana na baadhi ya Wanachama wa Simba SC ambao wanampenda Kinafiki ili Timu iharibu halafu Lechantre afukuzwe na akabidhiwe Timu yeye.

Ni hayo tu Mkuu na tupo pamoja.

yametimia lechantre kapigwa chini kimya kimya.....binafsi na wasiwasi sana na hii simba chini ya mo, coz wana maamuzi ya kukurupuka mno kuanzia usajili wao mpk maamuzi yao kiujumla lm viongpzi
 
Back
Top Bottom