Kama labda unajiuliza kwanini Kipa Peter Manyika Jr leo anadaka sana jibu ni hili...

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Ikumbukwe kuwa alipelekwa Singida United na Simba SC kwa mkopo ili akakuze Kiwango chake na kama kikiwa juu kama huko nyuma basi Uongozi utamrudisha Kikosini. Nimetoka kuwasiliana na Mchezaji muhimu sana wa Simba muda si mrefu akiwa huko huko Nakuru ( jina nalihifadhi ) na kuniambia kwamba jana Yeye pamoja na Wenzake ( Wachezaji wa Simba SC ) walimwambia Peter Manyika jr kuwa ahakikishe leo ' anakaza ' mno ili kuweza kuwashawishi Viongozi wa Simba SC ili arudi Kikosini na aweze kusaidiana na Kipa namba moja Aishi Manula.

Na kwa taarifa za hivi punde tu na ambazo tayari nimeshahakikishiwa na chanzo changu kingine kilichopo ndani ya Simba SC kinasema kwamba Kipa Peter Manyik jr anarudi Kundini Simba SC na Kipa Said Nduda ataachwa.

Kama Manyika akirudi Simba SC itakuwa jambo jema kwani atampa changamoto sana Manula na Simba SC haitokuwa na wasiwasi au hofu yoyote na Makipa na Timu itakuwa nzuri zaidi.

Nawasilisha.
 
mechi ngapi ngapi mkuu

Bado 0 kwa 0 Mkuu na Kiwango ambacho anakionyesha leo ' Dogo ' Peter Manyika jr ni kikubwa na cha juu mno. Ameokoa ' michomo ' mingi tena ya wazi wazi na hatari kabisa na hivi punde tu ametoka kuokoa ' Penati ' na mpira wa ' rebound ' na bado mechi baina ya Timu yake ya Singida United na AFC Leopards inaendelea huku sasa ikiwa inaenda dakika ya 78 na sekunde 33.
 
Amejitahidi sana mpaka sasa
Amesave penalt

Na ndiyo maana Simba SC inamrudisha Kundini halafu kumbuka kwamba karibia 95% ya Marafiki zake wote wapo ndani ya Kikosi cha Simba SC hasa wale ambao alianza nao kucheza tokea walipokuwa wote Simba SC ' B ' iliyokuwa chini ya ' Fundi ' wa Kiungo Kocha Seleman Abdallah Matola a.k.a Veron a.k.a Mzambia.
 
Sheikh Yahya amezaliwa tena JF
 
siku moja matola akipewa simba, vikombe kedekede[emoji16]
 
Gor mahia na Simba wakikutana fainali itapendeza zaidi.
 
ndio maana alipigwa 4G na Simba au hakuwa yeye?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…