Kama ligi kuu ya uingereza ingekuwa darasa la shule ya sekondari

Kama ligi kuu ya uingereza ingekuwa darasa la shule ya sekondari

Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2014
Posts
15,267
Reaction score
29,917
KAMA LIGI KUU YA UINGEREZA INGEKUWA DARASA LA SHULE YA SEKONDARI.

1.Liverpool ni mwanafunzi anejisifia na kuona ana akili kwa kuwa babu yake alifaulu kwa division one japo yeye anapata zero.

2.Manchester city ni mwanafunzi wa kishua ambae wazazi wake wanamnunulia vitabu vingi na vya gharama lakini ni mvivu wa kusoma hii inamfanya afaulu mitihani ya ndani lakini nje ya shule ana fail.

3.Arsenal ni dogo maskini mtulivu darasani anaesongoka sana na huwa anabahatisha kuwa wa kwanza kwenye mitihan ya mid term ila mtihani wa taifa anafeli.

4.Tothenham ni dogo anaefaulu somo moja tu mara nyingi huwa anapishana maksi chache na arsenal.

5.Chelsea ni mwanafunzi wa kishua ila mtemi wa darasa zima haswa kwa wanaoongoza darasani ambae akifeli tu anamlaumu ticha wake mpaka afukuzwe.

6.Everton ni dogo mcharuko na mjanja mjanja anae soma kipindi cha mtihani tu kwa ku paniki.

7.Manchester united ni dogo mwenye akili za kawaida ila muongo muongo anaetegemea chabo na kuiba mitihan tatizo anaemfanya aibe mitihani kesha staafu ndo mana now anapiga F kila pepa japo kanunuliwa vitabu vipya vilivyo nje ya
silabasi.

[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom