Kama Ligi ndio ingekuwa inaanza sasa basi Simba ingeshuka daraja

Kama Ligi ndio ingekuwa inaanza sasa basi Simba ingeshuka daraja

Mwenendo wa Timu hii kwa sasa hauridhishi , na kwa kweli ni kama wameamua kwa makusudi kutudhalilisha sisi mashabiki na wanachama wake .

Kila tunapopita tunachekwa na kunyooshewa vidole , huko maofisini hali ni mbaya zaidi , kuna wakati matokeo ya timu yetu yanasababisha baadhi wasiende kazini kwa kuogopa aibu .

Hii hali itavumiliwa hadi lini ?
Mezeni panado tu maisha yaendelee.
 
Nyie makolo jiangalieni na mjitafakari Mkicheza utumbo kama wa leo tar 20 mtachezea saba nadhani mnatufaham
 
Kadeki kwa Sugu mpira na wewe mbali mbali.Eti ligi ingeanza sasa !! Kwani Simba kapoteza pointi ngapi kwenye ligi hivi karibuni mpaka ufikie hiyo conclusion?Au ni mkumbo wa kuandika tu uonekane umeandika?
 
... huko maofisini hali ni mbaya zaidi , kuna wakati matokeo ya timu yetu yanasababisha baadhi wasiende kazini kwa kuogopa aibu
Kama mtu anafikia hatua ya kushindwa kufanya kazi eti kwa sababu timu yake imefungwa au imetoa sare, huo ni ujinga
 
Kuna bazazi kaandika kama ligi ingekuwa inaanza basi Simba angekuwa anashuka daraja!Na huyu ni think tank kabisa wa kujitolea wa Chama fulani.
Sasa ligi inaanza timu itashuka vipi daraja?
Ujinga mwingine ni wa kupewa medali ya ujinga kabisa.
 
Upande huu wa soka usilete chuki za kisiasa , utadhalilika
 
Kadeki kwa Sugu mpira na wewe mbali mbali.Eti ligi ingeanza sasa !! Kwani Simba kapoteza pointi ngapi kwenye ligi hivi karibuni mpaka ufikie hiyo conclusion?Au ni mkumbo wa kuandika tu uonekane umeandika?
Nimekugalagaza kwenye siasa umekuja huku , halafu habari za timu yetu ya simba wewe zinakuhusu nini ?
 
Nimekugalagaza kwenye siasa umekuja huku , halafu habari za timu yetu ya simba wewe zinakuhusu nini ?
Wewe unigalagaze? Kwa upeo upi wa kufikiri?
Uwezo wako wa kufikiri ni mdogo sana usijipe ujiko.Wewe bado sana.
 
Ushauri wa bure kabisa kwa wanasimba.

Timu ichukuliwe kuanza sasa iwe chini ya viongozi wa matawi ya mkoa wa Dar es salaam wakiongozwa na "field marshal" Hassan Dalali mpaka baada ya tarehe 20/04/2024 usiku baada ya hapo timu warudishiwe Mangungu na Try Again. Vinginevyo timu wakiachiwa Mangungu na Try Again basi mjue zile tano huenda zikazaa mapacha. Na ikwezekana Jamhuri Kiwelu apewe kandarasi ya uhamasishaji kwa wachezaji kwa muda huo wote timu itakapokuwa kambini chini ya viongozi wa matawi. Nina hakika likifanyika hili walau Simba itapata matakeo mazuri na hata ikitokea timu imeshindwa haitakuwa kwa magoli mengi kama ilivyokuwa mechi iliyopita

Nimeiangalia Simba leo dhidi ya Ihefu kwa kweli saikolojia ya wachezaji na hata benchi la ufundi haipo sawa. Wachezaji wapo " down" sana. Timu nzima haina morali ya kutafuta ushindi yaani wanacheza kama wamelazimishwa wakati ndio kazi waliyosajiliwa kuifanya. Timu nzima imekata tamaa isipokuwa wachezaji wachahe ndio wanaoonyesha kupambania timu kwa nguvu.

Benchi la ufundi nalo sijui limechanganyikiwa na nini yaani muda mfupi tu Chama ametoa "assist" mbili za hatari moja kwa Miquison aliyopiga shuti kali kipa akaokoa na nyingine akampa Kibu iliyozaa penalti wakamtoa Chama halafu wakamuingiza Onana. Matokea baada ya kuingia Onana ndio basi tena biashara ya kutafuta goli la ushindi ikaishia hapo. Nafikiri imefika mahali sasa benchi la ufundi la Simba lipatiwe mtaalamu wa saikolojia vinginevyo huko mbele ya safari itakuwa shida. Unamtoaje mchezaji ambaye anakutengenezea nafasi zaidi ya tatu za kufunga kila mechi na mara nyingine huwa anaamua mwenyewe mechi hata dakika za mwishoni kabisa halafu unamuingiza bishoo mvaa hereni kwenda kuruka kuruka tu uwanjani na kutembea na mpira badala ya kupeleka mpira mbele kwa kasi timu ipate matokeo. Kwa leo benchi la ufundi lilipuyanga pa kubwa sana.

Ni mtizamo tu.
 
Back
Top Bottom