Naanto Mushi
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 6,236
- 15,677
Nimesikiliza kwa makini sana hotuba za Tundu Lissu akiwa Zanzibar, yaani unaona kabisa madini aliyokuwa anamwaga Tundu Lissu, laiti kama ile platform angekuwa yupo bega kwa bega ana mnadi Maalim Seif kama mgombea wa CHADEMA Zanzibar, mambo yangekuwa tofauti sana.
Sio kwamba napuuza nguvu ya ACT - Wazalendo kama chama cha upinzani chenye nguvu, ila ni kwamba kwenye nyakati ngumu kama hizi za kisiasa ambazo zina watawala wakorofi, ili uweze kupata matokeo, ni lazima uwe upande wa chama cha upinzani chenye historia ya uhodari wa hoja, harakati, na mapambano.
Nikifananisha ACT - Wazalendo na CHADEMA, ni vyama ambavyo vinautofauti mkubwa sana kwenye uhodari wa hoja, harakati, na mapambano. ACT bado nakichukulia kama chama ambacho kipo 'soft sana' na kinachofata misingi ya kujali sana taratibu na sheria. Ni chama ambacho kina uwoga uwoga fulani wa kuwaudhi watawala. Angalia ile kauli ya Bernard Membe ya kwamba eti alitafuta wadhamini kimya kimya ili kutokuingia kwenye mtego wa kuanza kampeni', ni moja wapo ya viashiria kwamba ACT bado kipo soft sana. Kwa mzani huo, sioni ni namna gani msimamo wa chama utaunga mkono mapambano ya Maalim Seif ya kudai haki yake endapo kama ataporwa ushindi kama ilivotokea miaka ya nyuma. Huwa inakuwa ngumu sana, kupambana ikiwa upo kwenye chama chenye falsafa nyepesi kuhusu mapambano na harakati.
Upande wa CHADEMA, wana historia thabiti ya harakati za kupambana, ambazo hata mimi binafsi naamini ndo mwarobaini wa kupambana na CCM, suala la Zanzibar, ukizingatia na historia yake, hakuna namna upinzani watashinda kule bila harakati za mapambano. Kwa historia ya CHADEMA na viongozi wake ambao wanamisimamo imara na wasioyumba, naamini kabisa Maalim Seif angekuwa kwenye chama salama sana kwenye huu uchaguzi ambao kwa huku Tanganyika, CHADEMA wameshajipambanua wazi wazi kwamba hawatakubali kunyongwa ifikapo October 28.
Haya ni mawazo tu, kulingana na upepo unavoenda sio kwamba nakichukia ACT Wazalengo, ila pia ni changamoto kwa ACT Wazalengo, wanatakiwa waamue kuwa maji ya moto kweli, nawaona wapo soft sana na kwa kweli wananiuzi, na wakiendelea kuwa soft hivi, hakuna namna Maalim atachukua nchi endapo ACT itaendelea kuwa na misimamo isiyokuwa ya kiharakati na mapambano kama wenzao CHADEMA.