The Dictator
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 4,475
- 12,281
Kwa nini?
1. Anahitaji mazoezi mengi sana. Si kutembezwa dakika 20 tu ukaona inatosha. Mara nyingi huhitaji saa 1–2 au zaidi za mazoezi makali na shughuli za akili kila siku.
2. Ni mbwa wa kazi-kazi. Alizalishwa kwa kazi za polisi, jeshi, ulinzi na uokoaji. Bila kazi au mafunzo, anaweza kutafuta "kazi" yake mwenyewe, kama kuharibu vitu au kufukuza watu na wanyama ilimradi awe bize.
3. Ana akili nyingi na hujifunza haraka. Hiyo ni faida kubwa, lakini pia huimaanishi hawezi kujifunza tabia mbaya haraka vilevile pale usipomfundisha vizuri kuhusu jambo jema na baya.
4. Ana nguvu na kasi kubwa. Akiwa hajafundishwa, anaweza kuwa mgumu kumdhibiti hata kwa mtu mzima mwenye nguvu zake. Ni mmoja kati ya breeds zenye hekaheka na nguvu haswa...
5. Anaweza kuwa na msongo wa mawazo au tabia za uharibifu wa mali ikiwa atabaki peke yake kwa muda mrefu au akikosa shughuli.
kufuga Belgian Malinois kunaweza kuongeza matatizo badala ya kuyapunguza.
Hata hivyo kwa upande mwingine, ukiwa na muda wa mafunzo ya kila siku, mazoezi, na uzoefu wa kushughulika na mbwa wenye nguvu, Belgian Malinois anaweza kuwa mwaminifu sana, mlinzi bora, na mshirika wa kazi mwenye uwezo mkubwa.