thomasankara
Member
- Jun 7, 2026
- 22
- 33
Tumshukuru Magufuli kwa kutimiza kuhamisha makao makuu ya Taifa Dodoma kufuatana na uamuzi wa baba wa taifa zaidi ya miaka 50 iliyopita. Karibu Marais wote waliyofuata hasa waswahili wa pwani hawakulipendelea suala la kuhamisha makao makuu kwenda dodoma.
Baada ya Nyerere, Mwinyi hakutoa kipaombele kabisa kuhamia Dodoma. Kikwete yeye alijikuta akisema wazi wapwani hawataki kuhamisha mji mkuu. Mama samia mswahili wa pwani bahati yake mbaya kakuta mji mkuu ushahamishwa lakini kila dalili inaonyesha anafurukuta kuhujumu.
Mwenyewe hakai wala kufanyia kazi Dodoma. Kila shughuli ya Rais anafanyia Dar es salaam. Iwe ni kupokea mabalozi, kuapisha viongozi, kutangaza teuzi, kupokea marais wageni nchini iwe kukutana baraza la mawaziri yote anafanyia Dar es salaam.
Leo hii naandika anapokea Rais wa Namibia Dar. Hivi sasa zinapigwa nyimbo za taifa ikulu ya Dar. Bila rais kupenda makao yake makuu nani atapenda. Mawaziri makatibu wote saa zote wako Dar es salaam kumfuata Rais wa Jamhuri. Je mabalozi watahamia dodoma?
Je ubalozi zitajengwa dodoma? Balozi bila shaka hazitahamia Dodoma. Hakuna hata ubalozi mmoja umehamia dodoma hadi sasa. Wanapewa viwanja ila huko mbeleni sijui itakuaje.
Kuna mengi ningesema ila ngoja niendelee kukodoa macho tu.