Kama mama mwenyewe amekiri msuli wake ulikuwa mdogo, Tusimuonee Gambo

Kama mama mwenyewe amekiri msuli wake ulikuwa mdogo, Tusimuonee Gambo

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
4,016
Reaction score
6,759
Tumeshuhudia hii miezi miwili kukiwa na kauli kadha wa kadha zenye kukinzana na matendo mbalimbali yaliyofanywa na awamu ya 5 chini ya Shujaa toka kwa wateule wake wa kipindi hicho. Moja ya wateule hao ni aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Arusha, ambaye kwa sasa ni mbunge wa jimbo la Arusha mjini Mh. Mrisho Gambo (Mb).

Nisingependa kuzirudia kauli hizo lakini recently ni hii inayohusu unyang`anyi kwenye maduka ya kubadilishia fedha za kigeni. Naona kundi kubwa la wapingaji wa awamu ya Shujaa wakiwashambulia wateule hawa waliopita bila kusahau ya kuwa Executive power ilikuwa kubwa sana na ya kutisha kias cha kwamba kama jambo hulielewi ni bora kuufyata.

Sasa tunaona Mh. Gambo na wengineo wakikiri waziwazi kuwa walikabwa pumzi nasi tukiwashambulia kwa kasi bila kujali kuwa nafasi zao zilikuwa ni ndogo sana ukitokea juu. Tumejione wenyewe kuwa hata VP wa wakati huo amekiri waziwazi kuwa kuna sehemu alijaribu kuingilia au kuulizia akaona "Msuli wake mdogo".

Mtazame PM naye alikuwa pozo wakati hata alipojaribu kudeal na Mk. wa Bandari ni dhahiri alikuwa na msuli mdogo. Hivyo tukianza kuwashambulia wateule wa awamu Iliyokwendazake itabidi tupite kwa PM,Kwa mama na wengineo akiwemo IGP ambaye mimi naamini anaijua kazi yake vizuri kama asipoingiliwa halafu ndo tuwalaumu dagaa kama akina Mrisho.

Cha msingi ni kuanza kuevaluate na nadhani watafahamika wengi ambao walikuwa wanapenda na kufurahia, lakin pia tumuunge mkono Mama yetu ambaye labda aliteleza au naye msuli ulikuwa mdogo lakin anaonekana wazi hakuwa akifurahia fomesheni ile ya kukaba sana. Tujenge imani nao tuje kuwalaumu kwa maendo yao sasa wakati wapo huru kucheza tikitaka kila mmoja na nafasi yake.
Tukiruka na Gambo, Itabidi turuke na wengi.

KWA KIFUPI SYSTEM ILICORRUPT .
 
Si ni katiba imetoa mamlaka hayo? Imesema Rais ndiye atakua na kauli ya mwisho kwa chochote kile, imesema pia atashauriwa ila siyo lazima afuate ushauri.

Imesema pia atamchagua yeyote kushika nafasi yoyote bila kujali merits zozote. Sasa katika sheria unakuta muongozo unasema mteuliwa inabidi awe na elimu hii hapa na uzoefu huu hapa.

Ila aliyeteuliwa anaonekana kabisa hana vigezo na hauwezi fungua kesi kwakua katiba ishasema atamchagua yeyote. Hata katika maagizo na maamuzi imesemwa wazi yeye ndiye mwenye kauli ya mwisho kwahiyo ikatokea Rais hana hekima lazima aonekane miyeyusho.

Am simply saying marehemu aliact kwakua katiba inatoa hiyo ruhusa.
 
Hiyo ng'ombe inataka kujisafisha na uuaji aliokua anafanya na sabaya kwa kumsingizia mwendazake! Sisi sio wa kuzugwa na mdoli km ga mboo! Mlipewa nafasi mkaichezea hamtaaminika tena kamwe!
 
Siku hizi kuna waTanzania wanajaribu kuonesha na kutoa ushahidi umuhimu wa kuwa na mfumo utakao mbana yeyote aliye pewa mamlaka ya kuongoza nchi kufuata miongozo mikuu badala ya utashi wake pekee.

Ni jambo jema sana. Labda ipo siku itawezekana. Lakini kwasasa ni kama kuna walishika mpini na walioshika makali.

Wapo watetezi eti kwamba mtu ni muhimu kuliko mfumo thabiti unaowezeshwa na katiba.

Ndio maana utasikia watu wanasema kiongozi fulani kaletwa na Mungu, nchi yetu imebarikiwa, ona hivi ona vile.

Yapasa tuwe na mifumo inayo mbana yeyote akienda kinyume na matakwa ya wananchi au kikatiba anaondolewa alipo au hata kujiuzuru mwenyewe.

Tanzania watapita marais wengi tu, habari ya kubahatisha fulani alitumwa na Mungu ina maana wengine walitumwa na nani?

Safari itakua ndefu kufikia ukamilifu lakini papo pa kuanzia. Tuwe na katiba itakayo toa fursa ya kumbana raia yeyote yule awe namba wani au ile ya mwisho kabisa.
 
Kama hayati alikuwa mchafu na hawa wasaidizi hawawezi kuukwepa uchafu kama alikuwa Msafi hawawezi kuukwepa Usafi.

Kuna wakurugenzi wa mamlaka nyingi tu walipewa uhuru wa kufanya kazi kitaalam na tija ikaonekana, hutakaa uwasikie wakijaribu kujikomba kwa Madame Rais ili wawe sehemu ya uongozi wake.

Hawa wanaojaribu kutaka waonekane wasafi ni wachafu hata kwa Kiongozi wanayejaribu kujivuta kwake.
 
Kama gamba kweli analaani kitendo kile cha maduka ya pesa basi aachilie ngazi mana inasemekana katika ubunge pia amebebwa
 
IGP ambaye mimi naamini anaijua kazi yake vizuri kama asipoingiliwa halafu ndo tuwalaumu dagaa kama akina Mrisho.
Ujambazi umerejea kwa kasi sijui ile statement ya Mwendazake "I wish I could be ..." ndiyo ilisitisha ujambazi au IGP kazembea
 
Back
Top Bottom