Kama mambo yenyewe ndio haya bora niitwe bahili tu...

Kama mambo yenyewe ndio haya bora niitwe bahili tu...

Nakushauri usiwape hata mia mbovu.

Kuna mwamba sijui anaitwa nani katoa ngoma inaitwa "Siendekezi Ujinga", idownload halafu watumie kwa WhatsApp itawafaa zaidi..
🤣🤣🤣🤣ngoja niwatafute.

Tule bata lakini kwa urefu wa kamba zetu. Hata Mama aliwashauri hivyo baraza lake.🤣
 
Habari za usiku huu ndugu.

Kwenye maisha haya ya kiliberali ili yasonge mbele kila mtu anatakiwa aishi vile anavyotaka. Kimjini mjini wanasema kila mti kimpango wake. Yaani unaishi bila kuuliza uliz maswali ya nani anaishi vipi anakukaje. Sasa jama ndio hivi okay poa tusisimbuane.
Wewe kama kumsaidia msaidie kama hutaki kausha Bata zake hazikuhusu hapa town
 
Watu wanaotumia pesa namna io ni wajinga wajinga tu, namna ya kufaidika nao we kua na ka mtaji kako tu, siku akipata pesa huwa wanakua na papara nazo zikiisha wanaanza kuhangaika.

Hapo akija kwako anaweza kuuzia hata simu ya 3+M kwa laki 5 tu au mali yoyote ile nzuri kwa pesa ya kutupwa hakikisha hukopeshi tu, mpaka aje ashituke umepiga pesa nyingi tu.

Nb, msaidie mwenye shida ambayo hajaisababisha kwa ujinga wake, ingawa sio lazima, ila hao wafujaji faidika nao tu.
sawa
 
Habari za usiku huu ndugu.

Kwenye maisha haya ya kiliberali ili yasonge mbele kila mtu anatakiwa aishi vile anavyotaka. Kimjini mjini wanasema kila mti kimpango wake. Yaani unaishi bila kuuliza uliz maswali ya nani anaishi vipi anakukaje. Sasa jama ndio hivi okay poa tusisimbuane.

Hapa nina funzo kwa vijana, wazee mmeshapitia mengi hata ukijifunza leo haisaidii kitu. Kama kupata umeshapata na kukosa ushakosa. Nimekuwa na marafiki wengi wenye msaada na wale wa kupita tu. Mradi maisha yaende. Baadhi tabia zao zinanikera. Mtu anatafuta pesa zake kwa jasho lake, sawa! Ofcourse huwezi kumpangia mtu atumieje.

Akishakupata pesa yake anakula bata, kesho yuko na demu yule. Keshokutwa yuko Beach Hotel. Inafika jumapili anakupigia simu umtoe buku teni ya umeme. unamshangaa huyu vipi? Pesa zake yeye ale bata ila ya umeme umnunulie wewe? Mwingine naye yeye chapombe tu. Tena mwanamke. Ana kazi ya kupata hela daily lakini anapopata mchongo mzuri basi Bar kali kali zitamkoma.

Wakati sisi na maumivu ya tozo na vyuma kukaza chini ya Mh Rais Mama Samia Suluhu Hassan na ajira ngumu tunabajeti ili siku zisonge. Sasa Kodi yake imeisha ameniganda kama ruba. Sipumui. Si hemi utadhani hiyo nyumba yangu. Ofcourse anajua kama nina hela a uwezo wa kumsaidia ninao lakini nawaza.

Mimi zangu nazipata kama anavyopata yeye. Naweza mahesabu natumia kwa vitu vya msingi. Bata napunguza. Pesa zake ake bata ila kodi ya nyumba nimchangie mimi?

Kama ntaitwa bahili sawa tu na wacha ikae hivyo hivyo. Ila ujinga sitakagi mimi.
Andika vizuri, au kaa utulie then uje utusimulie.😂😂😂
 
Back
Top Bottom