Kama marefa watachezesha kwa haki ligi kuu msimu ujao, Simba, Yanga, Azam hawawezi kutwaa ubingwa

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Nawaangalia hapa Singida wakicheza na As Vita, aisee jamani jamani, kama ligi haitokuwa na ungese, nna uhakika [emoji817] wakongwe hawawezi kubeba ubingwa. Singida wamekamilika kama ilivyo Simba , yanga, azam, ihefu, Tabora nk.
 
Hiyo mechi ya kifrend tena Moja ndo case study yako duu ao awatoboi ata kwa mtibwa Suger acha kuwalinganisha na madude makubwa ya mpira wa bongo
 
Sijaona la maana walilocheza hao unao waona wakichukua huo ubingwa. Subiri majibu utayaona kwenye ngao ya jamii!!
 
Bingwa ni SIMBA/YANGA.


Hao wengine watapambani kutokushuka daraja. Ligi ya Tanganyika ina wenyewe ambao ni Simba na Yanga, hao wengine ni wapambe tu
 
Singida wamekamilika kama ilivyo Simba , yanga, azam, ihefu, Tabora nk.
Basi iwapo wamekamilika kama hao, wanaweza kwa haki pia wasichukue ubingwa badala yake mmoja wa hao akachukua. Nilidhani wamekamilika kuliko hao
 
Kazi IPO.

Ila nilichokiona kwenye Mchezo WA Bonanza, pamoja na kwamba singida wameshinda ila walizidiwa sana.

Pre season Huwa hatuangalii MAGOLi
Tunaangalia.

: Insurance ya Wachezaji.
: Fitness ya Wachezaji.
: Energy, kasi ,NGUVU.
: Uwezo wa wachezaji kucheza team work.
: Uwezo wa kushika maelekezo nk

SINGIDA WALIZIDIWA MNO KIUCHEZAJI.
TACTICAL ABILITY
 
Bingwa ni SIMBA/YANGA.


Hao wengine watapambani kutokushuka daraja. Ligi ya Tanganyika ina wenyewe ambao ni Simba na Yanga, hao wengine ni wapambe tu
Nataman watanganyika tuamke

KIGOMA ni mashujaa TU
Lindi ni namungo TU
Moro ni mtibw TU
Mbeya ni prison TU
Tanga ni wagosi TU

ILA KWAKUA KILA ANAYEZALIWA NI YANGA AU SIMBA TATIZO LINAANZIA HAPO
 
Reactions: K11
Bingwa ni SIMBA/YANGA.


Hao wengine watapambani kutokushuka daraja. Ligi ya Tanganyika ina wenyewe ambao ni Simba na Yanga, hao wengine ni wapambe tu
Kuna watu wanakasirika, kwa nini unaanza kuiandika Simba, kisha Yanga!?
 
Reactions: K11
tumewaona yanga na Singida wakicheza baada ya sajili zao, Bado hatujawaona Simba Wala Azam wakicheza. Je siku wakicheza wakaonyesha uwezo mkubwa zaidi ya Singida utaanzisha Uzi mwingine.
 
Kama Singida wamekamilika kama ilivyo kwa Yanga, simba na Azam, kwanini sasa hizo timu zisiweze kuchukua ubingwa pia kama wanafanana??
Mimi nilijua Singida kazidi wote
Achana nae mwezi mchanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…