Kama mdau toa ushauri kwa Serikali juu ya usafiri kwa wanafunzi

Future president

Senior Member
Joined
Dec 30, 2013
Posts
144
Reaction score
39
Kila asubuhi na jioni nashuhudia udhalilishwaji wa viongozi wa baadae yaani wanafunzi wa leo jinsi wanavyohanya na usafiri wa mabasi pindi wanapoenda au kurudi mashuleni.
Wanakuwa ni watu wa kuviziana na makondakta milangoni hata kufikia hatua ya kupigana kabisa, hembu kama mdau wa forum hii ya kuelimisha ambayo hata viongozi wanaipitia na pia wamo humu humu toa maoni yako kwa Serikali nini kifanyike, labda hawafahamu.
 
Ifanyike sensa ndogo ya wanafunzi, kujua idadi ya wanafunzi kila wilaya au kata kwa mfano. Kisha yawekwe mabasi makubwa kama ya UDA kwa kila route.

Mabasi hayo yawekwe kulingana na idadi ya shule na wanafunzi katika eneo husika, for instance, kwa shule zilizopo k/koo, wanafunzi wengi huenda Mbagala, Gongo la Mboto na Tabata, hapo wanaweza kuweka mabasi mawili yapitayo Nyerere Road kuelekea G/Mboto na lingine Kilwa Road kuelekea Mbagala. Watawasaidia wanafunzi wengi.

Kisha waweke basi moja litakalokwenda hadi Ubungo kwa kupitia barabara itakayofaa. Maeneo yapo mengi, nadhani point imeeleweka, wanaweza kupanga route za namna hiyo.

Wanafunzi watalipa nauli ya kawaida wanayolipa sasa ili kusaidia suala la maintenance ya mabasi, kama kutakua na pungufu serikali itachangia percent itakayobaki.

Kama hili litafanyika, idadi kubwa ya wanafunzi itapungua katika vituo vya mabasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…