Fascinating
Senior Member
- May 14, 2025
- 146
- 351
Naanza kuamini, kama mechi za mpira wa miguu zingekuwa zinamalizika dakika ya 85, Afrika ingekuwa imefanikiwa sana kwenye kombe hili la Dunia, na mashabiki wetu wasingekuwa na presha ya kupanda kila kukicha. Lakini kwa bahati mbaya, FIFA wana dakika zote 90 na hicho kipindi cha lala salama ndipo ndoto za soka la Afrika zinapozikwa rasmi.
Ukiangalia mechi za hivi karibuni ambapo timu zetu zilipoteza mchezo dhidi ya mataifa ya Ulaya, huwezi kujizuia kufikiri kuwa kuna mambo ya Kiswahili: Team za Afrika tumerogwa au ni nini?
Haiwezekani! Inakuwaje kisayansi, mbinu, au hata kiroho kwa timu tatu kubwa za Afrika kukatika pumzi na kuruhusu goli kwenye dakika ile ile ya 86?
Inashindikana Vipi Kujishikiria Dakika 4 Plus Za Nyongeza?
Hivi huwa tunapatwa na nini hasa muda ukigonga dakika ya 85:00? Je, kuna meseji ya siri inayotumwa kwa mabeki wote inayosema, "Haya jamani, kazi imeisha, tuanze kufikiria kubadilishana jezi"?
Tunaweza kulaumu ukosefu wa umakini, au tunaweza kusingizia hali ya hewa ya Ulaya, lakini hii inafanana sana. Kufungwa kirahisi hivi ukiwa umeshikilia droo au ushindi zikiwa zimebaki dakika nne tu za kawaida pamoja na nyongeza ni mchezo wa hatari ambao timu za Afrika zinatakiwa kuuacha mara moja.
Wakati mwingine timu ya Afrika ikicheza na timu ya Ulaya, kocha anatakiwa kuifuta kabisa namba 86 kwenye vyumba vya kubadilishia nguo. Turuke moja kwa moja kutoka 85 hadi 87. Labda hapo, vijana wetu watajifunza jinsi ya kujishikiria na kumaliza mechi kwa ushindi!

- Jinamizi la Viking Haaland: Ivory Coast walikuwa wamejikilia muda wote dhidi ya Norway, lakini ghafla Erling Haaland akapenya na kufunga goli dakika ya 86.
- Janga la Kane: DR Congo walipambana kiume, lakini Harry Kane akaona dakika ya 86 ndiyo muda muafaka wa kuharibu usiku wa mamilioni ya Wakongomani.
- Lukaku, Daah kama ameua ndugu zake: Simba wa Teranga wa Senegal, ambao kila mtu aliwasifu nidhamu yao walimwacha Romelu Lukaku akate mitaa hadi akapachika goli la ushindi dakika ya 86 na kufungua njia ya Belgium kupata ushindi wa 3-2
Ni Mbinu Mbovu au Ushirikina?Inasikitisha sana. Ni kama vile akili ya ukabaji inazimika ghafla. Tunahimili mbinu zote za makocha wa Ulaya kwa dakika 85, alafu tunalegea pale ambapo mstari wa mwisho unapoonekana.