Tetesi: Kama mkakati huu wa ACACIA na Barrick ukifanikiwa, watanzania ( wake kwa waume) mmepigwa bao

Tetesi: Kama mkakati huu wa ACACIA na Barrick ukifanikiwa, watanzania ( wake kwa waume) mmepigwa bao

hizi ni hisia tu. hakuna lolote la maana unalolijua.
 
Tahadhari!
Usinihoji kuwa mimi ni nani, lakini kiufupi naipenda Tanzania ingawa yenyewe hainipendi kama ninavyoipenda.

Kama kawaida yangu naendelea kunyetisha na kuwapa habari motomoto zihusianazo na makinikia pamoja na hawa wanaume wezi ( Acacia na Barrick)

Viongozi wa Tanzania waliteleza katika hili na wanaendelea kuteleza na sasa kilichobaki ni kuanguka na kushindwa kuendelea na safari ya kuokoa makinikia na madini ya Watanzania. Kosa la kwanza ni kumpuuza Acacia ambaye ndiye mwizi mkuu na namba Moja. Amepuuzwa na kuchukuliwa kama mtu mdogo sana asiye na madhara katika wizi huu ingawa ndiye mwizi wetu. Kiuhalisia mwizi wetu siyo Barrick ila nguvu zetu zote tumehamishia kwake huku tukiwa na matarajio makubwa!!!! Mwizi tumemuacha, sasa anatamba! Yuko huru! Hata kwenye mazungmzo hayumo na tunaamini hivo kuwa hayumo maana mazungumzo ni kati yetu na Barrick, WATANZANIA MNAJIDANGANYA!!!

Huu ndio mkakati wa Acacia na Barrick na ukifanikiwa watanzania wake kwa waume mnatakuwa mmepigwa bao!

Kama makubaliano kati Barrick na Serikali ya Tanzania hayatakuwa na manufaa kwa Acacia na Barrick, kwa maana ya malipo ambayo yanapaswa kulipwa kwa Tanzania ( ingawa pesa itakayolipwa ni ndogo tofauti na matarajio ya Watanzania) Acacia wataendelea na Kesi yao ambayo wanapanga kuifungua dhidi ya Tanzania. Katika kesi hii ambayo kwa kiasi kikubwa wana uhakika Wa kushinda watadai fidia kubwa mno ambayo ikilipwa itawawezesha kuendesha kampuni yao bila wasiwasi.

HOFU YAO KWA SASA
Hofu yao mpaka sasa ni pale watakapoamua kuishitaki Tanzania basi kuna uwezekano wa kufukuzwa kuendesha shughuli zao hapa nchini. Naam! Hili wamshaliona na wamekubaliana na Barrick namna watakavyoendesha biashara zao hata baada ya kufukuzwa, kwani kama haya yatatatokea Barrick watamiliki hisa zote hata zile zilizokuwa zikimilikwa na Acacia.

Lakini wanaona hawatakuwa na namna ya kurudisha pesa yao zaidi ya kuishitaki Tanzania ambayo mpaka sasa imeshasahau kuwa ndio iliyosaini mikataba na kuiruhusu kampuni ya acacia kuendesha shughuli zao hapa nchini

MPANGO WAO
Barrick wanaweza kulipa hicho kiasi kidogo harafu kwa mkakati mzito acacia watarudisha pesa zaidi ya hizo kwa njia ya mahakama huku wakijifanya kuwa wao hawana habari na mazungumzo yanayoendelea. Ukweli ni kwamba acacia wanahusika chini ya mkakati mzito na Barrick na Leo lao ni kuipiga Tanzania na mpango wao huenda ukafanikiwa.

Mpango wao ukifanikiwa wale mliokuwa mmeshakabidhiwa noa mjiandae kuzirudisha

Ni hayo tu

NIBOZALI WA LUMUMBA
Maaae, me sijapigwa bao
 
Mwenyekiti wa Barrick Gold anaongea

Anasema Mbele bado kuna matumaini makubwa na wana kazi kubwa ya kufanya na maamuzi yote yanatakiwa yapitishwe na bodi ya wakurugenzi iliyopo Uingereza ambao wanamiliki 64% ya Acacia

Mwenyekiti wa Barrick Gold John L. Thornton amesema kulikuwa na kutokukubaliana kati ya Tanzania na kampuni ya Acacia kuhusu masualaya kodi, hata hivyo wamekubali kulipa dola milioni 300 kwa ajili ya kukuza uaminifu

Kutokana na ugumu wa suala lenyewe wamekubaliana kuunda timu ndogo ambayo itashirikisha pande zote mbili kwa ajili ya kuendelea kushughulikia masuala machache yaliyobakia

Michakato yote itaenda kwa misingi ya uwaziili tuweze kuelewa masuala yote kwa uwazi zaidi

Nampenda kumshukuru rais Magufuli kwa kuwa ndio muanzilishi wa mchakato huu na mfumo huu wa biashara ambao utakuwa ni mfano wa kuigwa duniani, nawashukuru sana....amemaliza
 
Jamii Forum where we dare to talk openly..Haya nabii tunasubiri part two. Part one imeisha na yaliyotabiriwa yanaonekana
 
Back
Top Bottom