Kama Mkristu Mkatoliki Naomba Unishauri!

Nenda katika parokia iliyopo karibu nawe..kaonane na katekista..hapo utaambiwa usome mafundisho ya ukatakumeni nahisi hua ni miezi mitatu hivi sina uhakika sana...baada ya kumaliza mafundisho utapokea ivyo unavyovihitaji

Au kama vipi okoka kabisa nenda kabatizwe upya kwenye maji mengi..kule hakuna komunio wala kipaimara

Sikushauri kuhama dini
 
Ukatoliki haukufikishi mbunguni ndugu mtafute YESU KRISTO ndio jibu la yote. Haujachelewa
 
Padre gani unamawazo finyu kiasi hiki. Hilo nalo ni tatizo kweli la mtu mzima kuja kulialia huku JF ambako wapagani hulala na kuamkia?!
 
Hayo matatizo yako yangeweza kutatuliwa
1. Padre angeweza kuandika barua katika parokia uliyobatizwa akawapa jina na tarehe yako ya ubatizo. Kumbukumbu za ubatizo ziko kwenye registrar. Ungetumiwa nakala ya cheti chako.

2. Kwakuwa ulifanys mafundisho unge batizwa na kuleta komunuio siku moja.

Mtafute padre kwenye parokia yako muongelee hili tatizo
 
Padre gani unamawazo finyu kiasi hiki. Hilo nalo ni tatizo kweli la mtu mzima kuja kulialia huku JF ambako wapagani hulala na kuamkia?!
Asante Kwa Busara Zako..
 
Asantee Saana!
 
Pole kwa unayoyapitia, kwa ushauli wangu usiangaike kuhama dhehebu au dini.
kila tunachokipitia kwenye maisha huwa kina makusudi yake akuna bahatimbaya kwenye maisha.
Mungu ameyaruhusu hayo unayoyapitia kwa makusudi, labda kwa sasa ni vigumu kuyaelewa labda mbeleeni ikimpendeza Mungu atakusaidia kuyaelewa. Katika kanisa kunataratibu zake awawezi kumpokea mtu kiolela jaribu kwenda kuongea na parokia ambayo ulibatizwa watafatilia na kujiakikishia kuwa huu mkweri watakupa cheti au kufanya utaratibu ubatizwe upya. Ikishindikana kwenda kwenye hiyo parokia tafuta parokia ya karibu ulipo waeleze na watakusaidia.

- Usijari ndugu kuwa na nia na Mungu atakusaidia maana Mungu hujua yote yaliyo ndani yetu na kama anataka uwe padri utakuwa tu.
kwa kukupa moyo jaribu kusoma maisha ya mtakatifu Agustin alikuwa anafujo za kila namna na alikuwa na mtoto lakini kwa neemaa za Mungu alikuja kuongoka na kuja kuwa padri, askofu na mwalimu wa kanisa.
- Mtakatifu Rita wa kashia aliolewa kwa sababu wazazi walitaka hivyo lakini moyoni alitaka kuwa Sister na Mungu alimjalia kulingana na hitaji la moyo wake.

Angalizo
- usije ukafanya ujanja ujanja wa kukomunika pasipo kustahili kwa imani yetu unapokea hukumu maana Mungu zihakiwi
Ekaristi ni sacrament is not something human invert for religion purpose . Ekaristi zimewekwa na Yesu mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…