Tatizo lako kubwa
Mpinzire ni kwamba ama ni mzuka wa utoto au ni ujinga. Utoto ni kwa kutojua historia ya mapambano ya kudai mabadiliko na kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini. Ujinga ni kutojua Dr. Slaa aliingiaje Upinzani huku hakushiriki kabisa katika vita hivyo na alikuwa anakimbia nini huko kwao CCM!.
Dr Saa aliikimbia CCM baada ya jina lake kukatwa na Chadema ikampa hifadhi na kumteua agombee katika nafasi ile ile aliyokuwa akiitaka. Hivyo hivyo Lowassa aliikimbia CCM baada ya jina lake kukatwa na Chadema ikampa hifadhi na kumteua agombee katika nafasi ile ile aliyokuwa akiitaka. Je tofauti ya hawa walafi wawili iko wapi?
Yawezekama Chadema ilifanya makosa katika kuwapokea lakini ukweli ni kwamba hawa watu wawili ni ndege wafananao na hivyo huruka pamoja na wamerudi nyumbani kwao. Curses are like young chickens, they will always come back home to roost!Unakumbuka orodha ya mafisadi 17. Kwa ufahamisho, ukiondoa marehemu, wote wamerudi nyumbani.