Kama mnajua Sumaye na Lowassa walikuja Chadema kuibomoa, kwanini mnaendelea kumtukana Dkt. Slaa?

Kinana na makamba wamehojiwa?
 
Yule mzee msaliti tu, hadith yake haina tofafuti na hadithi ya Samson na delila,

Yaani mwanaume tena umri wa babu unadangaywa na kademu unakubali
 
Dr. Slaa hajawahi kujiunga tena au kurudi CCM alipotoka CDM. Maneno hayo ameniambia mwenyewe kwa kinywa chake October 2019 nilipokutana naye mahali.

..mienendo na kauli zake zikoje?
 
MLETA UZI NAPENDA KUKU JULISHA KUWA BABU SLAA SIO CHADEMA ORIGINAL. BABU SLAA ALIKUWA CCM ALIHAMIA CHADEMA BAADA YA JINA LAKE KUKATWA KWENYE KURA ZA MAONI. ALIKUWA ANA ONGOZA KWENYE KURA ZA MAONI KUGOMBEA JIMBO LA KARATU. BAADA YA KUKATWA JINA KWA HASIRA AKA HAMIA CHADEMA. BABU SLAA ALIKUJA CHADEMA KWA MASLAHI YAKE BINAFSI. BABU SLAA HANA UZALENDO WOWOTE ULE ZAIDI YA KUJALI TUMBO LAKE JAPO MWENYEWE ANA JIONA YUKO PERFECT KAMA MALAIKA ALIYETOKA MBINGUNI.

BABU SLAA NI MUONGO NA MZANDIKI. KWA HIYO HAKUNA CHA AJABU BABU SLAA KURUDI CCM. HAYO MENGINE NI PROPAGANDA, NA UPOTO SHAJI.KWA LEO NAISHIA HAPA.
 
Sawa...Makubaliano yenu na MEMBE yamefikia wapi Mkuu!?


Typed Using KIDOLE
 
MASIKINI HANA SIASA, ANA NJAA TU. CCM WALIFANYA YAFUATAYO MPAKA SUMAYE AKANYOOKA.
1. MASHAMBA KULE KILOSA WALICHUKUA.
2. SHAMBA LILILOKO BOKO WALICHUKUA. ALIKUWA ANASHINDA BARAZA LA ARDHI PALE WAZO MPAKA ANATIA HURUMA.
KILICHOFUATA KANYOOKA MAZIMA, CHEZEA NJAA WEWE.
 
Shida aliyefanya maamuzi inaaminika huwa hakosei si kwamba hawajui kuwa walipuyanga.

Wanajikakamua tu kumtukana Slaa ila nafsi zinawasuta "kishenzi"!
 

Kama wote watatu wamenunuliwa je?[emoji12].Fikiri nje ya box.Kila mmoja ana bei yake.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shida ya Dkt Slaa ni moja tu. Chama alichokijenga kwa nguvu nyingi alipotofautiana nacho alianza kukibomoa. Ilitosha kujiweka pembeni na kutulia asubiri wakati kuwa shahidi. Hivi vinywa vinaumba mengi. Usisahau lengo kuu la kwanza la chama chote cha siasa ni kushika madaraka ya nchi. Shida ni kuwa ni kwa vipi watayapata hayo madaraka, na hapo ndipo penye mgogoro. Sio kwali kwamba CCM wanapenda kupata madaraka kwa njia za wizi, ila ndio njia pekee iliyo rahisi kwao. Hivyo kumpokea Lowassa au awaye yote haingekuwa shida kama angerahisisha safari ya kuyafikia madaraka ya nchi. Kumbuka hii ni safari ya kwenda Ikulu na siyo safari ya kwenda Mbinguni.
 
Tatizo lako kubwa Mpinzire ni kwamba ama ni mzuka wa utoto au ni ujinga. Utoto ni kwa kutojua historia ya mapambano ya kudai mabadiliko na kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini. Ujinga ni kutojua Dr. Slaa aliingiaje Upinzani huku hakushiriki kabisa katika vita hivyo na kitu gani kilimkimbiza huko kwao CCM hadi akatua Chadema!.

Dr Saa aliikimbia CCM baada ya jina lake kukatwa na Chadema ikampa hifadhi na kumteua agombee katika nafasi ile ile aliyokuwa akiitaka. Hivyo hivyo Lowassa aliikimbia CCM baada ya jina lake kukatwa na Chadema ikampa hifadhi na kumteua agombee katika nafasi ile ile aliyokuwa akiitaka. Je tofauti ya hawa walafi wawili iko wapi?

Yawezekama Chadema ilifanya makosa katika kuwapokea lakini ukweli ni kwamba hawa watu wawili ni ndege wafananao na hivyo huruka pamoja na wamerudi nyumbani kwao. Curses are like young chickens, they will always come back home to roost! Unakumbuka orodha ya mafisadi 17? Kwa ufahamisho, ukiondoa marehemu, wote sasa wamerudi nyumbani.

Walipotapakaa huko na huko, walikuwa wanatupa shida sana katika kuwajadili na hasa sisi tusio na vyama lakini maadamu sasa wote wako pamoja (all bad eggs in one basket) ni wakati murua wa kupambana nao kwani kapu likidondoka mayai yote kwishnei, hakutabakia tena na hivyo safari hii pigo tu moja litatosha.
 
Na kikubwa ni kuwa Dr. Slaa alishiriki katika hatua zoooote za mchakato wa kumpokea Lowasa,ila alizidiwa makarama na Josephine. Na hii nayo ni udhaifu mkubwa kwake kwani hata angekuwa Rais angekuwa anayumbishwa na mama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…