Mambo ya hisa yana complications sana si marahisi kuyaelewa juu juu.
Mfano Hisa zinaweza kugawanya kwenye class, kama Class A NA B
-Class A ikawa na 10 voting rights
-Class B ikawa na 1 voting rights.
Hivyo kukawa na mtu anamiliki asilimia 20 ya Class A shares
Then watu milioni 1 wanamiliki class B asilimia 80 ya hisa.
Ina maana hapo mwenye Asilimia 20 ana kura 200 na asilimia 80 ana kura 80, chochote atakachosema mwenye Kura 200 hata waungane hao milioni 1 hawawezi kukitengua.
Mpaka ujue ni aina gani za hisa wanamiliki huwezi kufanya conclusion.