Kama Mohamed Dewji tajiri mkubwa vile alitekwa, wewe ulikuwa na kinga gani kwa bwana yule?

Kama Mohamed Dewji tajiri mkubwa vile alitekwa, wewe ulikuwa na kinga gani kwa bwana yule?

deblabant

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2022
Posts
2,650
Reaction score
4,065
Tukiwaambia nchi hii tumepitia kipindi kigumu sana muwe mnaelewa jamani! Maana kuna watu kabisa uwezo wao wa kufikiri ni mdogo sana.

During that regime kila mwekezaji alikuwa anaogopa na wengine walifirisiwa kabisa ama moja kwa moja au kwa kuchukua pesa kwenye akaunti zao, mfano Nimrodi mkono ambaye alipararaize kabisa akawa hatoki ndani tena pale masaki. Sasa nani angeweza kuja kuwekeza Tanzania kipindi hicho kama matajiri wanatekwa kirahisi rahisi tu wakati ndio mlipaji mkubwa wa Kodi.

Ambaye kidogo alikuwa safe ni kapuku ambaye alikuwa hana threat yoyote kwa yule bwana. Ndio maana ukazalishwa msemo kwamba ni Rais wa wanyonge kwa sababu tu makapuku hawana effect kwake na kwenye Urai wake. Japo baadae ingekuwa disaster mana machinga halipi Kodi au Kodi yao ni ndogo kabisa.

Imagine kila mtu hasa tajiri alikimbia nchi, kama akina M owe nk. Sasa hii nchi ingesonga mbele kwa miujiza gani bila ya kuwa na potential investors ambao wanalipa Kodi? Imagine Marekani waanze kuwateka akina Elon Musk, Bilgate nk, si ndio utakuwa mwisho wa wa economic giantism ya Marekani!
 
Dah! Pole sana Senior Member. Naona Mods wamekupiga na kitu kizito kichwani.
 
Mo alijiteka, kama wengine wa CHADEMA ambao walijitengenezea mazingira kwa uharakati wao
 
Na mo nimstaalabu tu maana hakusema kiasi cha mabilioni alichosaini kitoke kwenye account yake ndipo aliachiwa.
 
Sukumagang hawawezi kukuelewa! Hata Rostam alisimamisha uwekezaji mpaka JPM alivyojirudi.
 
Kipindi cha utawala wa jamaa, wachuuzi wadogo wadogo walifurika kila mtaa na barabara za majijini na mijini. Biashara ndogo ndogo zilikuwa shaghala-baghala, na tena zilifanyika kila sehemu bila uthibiti wowote.

Hao ndio walikuwa mtaji wa kisiasa wa Mzee, kwa kuwa hawakuwa na kitisho chochote kile kwake. Lakini kwa upande wa matajiri alijiapiza kuwa watalimia meno na wataishi kama mashetani.

Akaanza kuwatenda kutokana na aina ya majina ya chuki aliyowapa. Alitumia kanuni ya kuwa, ukitaka kumuua mbwa lazima umpe jina baya!

Wale alioamini ni wenye pembe moja alijitwalia sehemu ya fedha zao kwa nguvu kutoka katika akaunti zao na wengine kupunguza mishahara yao. Wale wa pembe mbili alifilisi biashara zao, wale wa pembe tatu na zaidi aliwafungulia kesi za uhujumu uchumi, na kuwasweka ndani.

Aliwashutumu wengine kuwa wanaleta taharuki katika utawala wake! Kumbe yeye mwenyewe alikuwa ni chanzo cha taharuki, na pia ni taharuki yenyewe!
 
Back
Top Bottom