Kama moyo chukua!

Kama moyo chukua!

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
32,529
Reaction score
76,691
Sasa ni zamu ya moyo wangu,maana figo na mapafu ulishaviteka!

Penzi lako ni kama hewa safi ya oxygen, inayopita katika viunga vya mwili na kuupa uhai uliotukuka!

Ucheshi na ukarimu wako ni tuzo tosha katika maisha yangu, hata kilio chako kimekuwa ni ngazi ya kukomaa kwa mapenzi yetu!

Tone la wivu wako kwangu ni kama ukuta wa babeli, siponyoki na wala sichoropoki. Naahidi kukulinda, kukutunza na kukupenda kwa maana naijua kiu yako kwangu.

Hata seli za mwili wangu husheherekea pindi zisikiapo sauti yako tamu. Moyo wangu nao hudunda kwa kufuata mapigo ya moyo wako, kwani mioyo hii miwili hutambuana kama watambuanavyo wapemba kwa vilemba!

Sina mengi laaziz ila usije kuongeza kizizi.😉
 
Ingia studio mzee, songi likitoka nitakupigia promo
Wasanii wa namna hiyo wengi walipotea kwenye game

Kuna mmoja aliachana na demu wake sasa zile depression zikamfanya atoe ngoma ya heartbroken ikabamba sana mtaani

Siku maumivu ya kuachwa yameisha na kipaji kikaishia hapo, kila akitoa ngoma inaishia kuskika geto kwake.
 
Wasanii wa namna hiyo wengi walipotea kwenye game

Kuna mmoja aliachana na demu wake sasa zile depression zikamfanya atoe nhoma ya heartbroken ikabamba sana mtaani

Siku maumivu ya kuachwa yameisha na kipaji kikaishia hapo, kila akitoa ngoma inaishia kuskika geto kwake.
Uzuri huu si wimbo!
 
[emoji23][emoji23]
 
Moyo auchukueeeeeeee eeehhh...
Ila akili zako akuachieeeee
Wewe usije okota makopooo.
Akili baki nazo mwache achukue moyoo.

Haya nimeongezea chorus
 
Jamani komenti ziwe fupifupi si mnajua moyo nishakabidhi..🤣
 
Back
Top Bottom