permanides
JF-Expert Member
- May 18, 2013
- 11,682
- 14,241
Kuamini Urusi anaweza kuishinda NATO kwenye vita ni matumizi mabaya ya akili. Russia ni overrated, Ukraine angekuwa na mfumo mzuri wa air defense ni wazi Russia asingetoboa. Kwa namna Urusi alivyopanga majeshi yake tena kwa kushirikiana na Belarus niliamini ingekuwa vita ya siku 2. Ingawa Urusi anaweza kuangusha majengo na kuteka miji, vita inahamia mtaani, na hii ndio vita ngumu zaidi.Kama mpaka sasa Jeshi la Ukraine limeweza kuwapa upinzani wa kiwango hiki, ni wazi Jeshi la Russia sio strong kama linavyoelezewa na ni wazi lisingeweza kuhimili majeshi ya NATO kama tu Jeshi la Ukraine linawatoa jasho mpaka muda huu.
Kwa sifa tunazosikia kuhusu Jeshi la Russia, nilitarajia mpaka muda huu mji mkuu wa Ukraine uwe chini ya Majeshi ya Russia lakini mpaka sasa bado.
Soon tutaanza kusikia madai kuwa Jeshi la Ukraine linapata support kutoka kwa wamarekani na washiriki wake.
Ama kweli actions speak louder than words.