Kama Mtaalamu wa Saikolojia ya Mahusiano, Namshauri Haji Manara Apunguze Kasi ya Kuanika Mapenzi yake Hadharani, hasa Faragha yake

Huyo jamaa huenda akili yake haiko sawa, hata kama ni mtu maarufu mjini anachofanya kuweka wazi mapenzi/mahaba yake kwa mkewe huo ni upuuzi na ujinga. Mapenzi yake kwa mkewe abaki naye kwake hatuhitaji atuambie jinsi anavyompenda na kumthamini mkewe hayo ni mambo ya chumbani kwake
 
Sio Haji Manara pekee wenye huo ushamba...

Wapo baadhi ya Wanaume wenzetu wengi wenye hizo tabia.

Mimi bora nionekane simpendi Mke wangu ama naogopa kumpost eti Kwa kuwa nina Wanawake wengine kama ambavyo wajinga hujisemea

Ama labda sijiamini kwa kuwa nimeoa Pisi Kali kama Vijana wa hovyo wanavyosemaga...

Ila sitakuja kufanya huo ushamba wa Kumpost Wife huko mitandaoni.

Msimamo wangu ni ule ule ....

"Wangu Namficha Kwapani"🤗

Namficha song by Harmonize
 
Angekuwa na akiili ujumbe huu ungemfaa..sasa tatizo hizo akili hana. Huenda pia aina hii ya maisha ndiyo inampa kula. Yaani hivi vituko ndo vinampa airtime na aadhamini wanaompa kula, usishangae kesho wakaachana ili kuweka attention zaidi.
 
Yote kwa yote wadada nao wajasiri sana,kumvulia Pichu yule jamaa inataka moyo wa ujasiri
 
Manara anafanya hivyo kibiashara zaidi na ndio maana tunatumia muda mwingi kumfatilia na kumjadili!

Maisha yake ameyafanya biashara hivyo bila kufanya hivyo hela haingii na sio manara mbona karibu wasanii wengi drama zao na vituko ndio biashara inayo wafanya waishi!

Tupunguze na tusipoteze muda kutoa ushauri maana akifata ushauri wako wewe mwalimu basi biashara yake itakuwa imeishia hapo! Manara usichukue huu ushauri.
 
Angekuwa na akiili ujumbe huu ungemfaa..sasa tatizo hizo akili hana. Huenda pia aina hii ya maisha ndiyo inampa kula. Yaani hivi vituko ndo vinampa airtime na aadhamini wanaompa kula, usishangae kesho wakaachana ili kuweka attention zaidi.

Hapo atakuwa anaharibu Wafuasi wake na Watu wa aina yake (wenye ualbino)
 

Hujui Manara ni nani kwa ulimwengu wa watu maalum (special Groups)
 

Kama hawatazidisha mipaka wapo Sahihi
 

Akazidisha ndio tatizo
 
Mkuu live your life. Acha kupangia watu maisha.
 
Kiukweli jamaa anazingua na sidhani kama hili penzi litafika mwaka. Ila why mzee posts zingine umezikubali ila ya kuosha miguu umeikataa? Naomba maelezo kidogo nikuelewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…