Kama Mtanzania, propaganda ni kitu cha kawaida sana

DaudiAiko

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2012
Posts
372
Reaction score
310
Wanabodi,

Kweli tumetimiza mwaka mmoja tangu Rais Samia aingie madarakani. Shangwe na vigelegele kila tunapo kumbushwa kuhusu miradi inayo endelea kusimamiwa na Rais. Mema yamefanyika, tuendelee kusubiria mambo mengine makubwa kutoka kwa serikali ya awamu ya sita.

Katika haya yote, kitu ambacho kinatupita wengi ni jinsi ambavyo serikali inatumia kila fursa kufanya "branding" ya yale yote yanayo fanyika serikalini na zaidi, kuhakikisha kwamba Jina la Rais Samia Suluhu Hassan linakubalika kila mahali nchini na kwa watanzania wote. Zoezi hili linafanywa kimkakati sana haswa na vyombo vya habari vikishirikiana na viongozi mbalimbali.

Serikali inajihusisha sana na suala hili na kwasababu hiyo, lazima kuna madhumuni ya hali kuwa kama ilivyo. Labda ni njia ya kuwa na "Control" kwa kuhakikisha kwamba serikali ina "impact" sana maoni ambayo watanzania wanaweza kuwa nayo kuhusu utendaji kazi wa serikali yao. Labda ni njia ya kumjengea Rais Samia mahusiano mazuri na watanzania na hivyo kuhakikisha kipindi chepesi zaidi katika uchaguzi mkuu ujao. Labda serikali ina amini kwamba kuna hatari kwa wananchi kupata taarifa ambazo hazija chujwa kikamilifu.

Yote haya yanaonyesha nguvu ambayo serikali inayo katika kufanya kitu chochote au kuchochea maoni yoyote kutoka kwa wananchi. Hii inaitwa propaganda.

Propaganda inaweza kufanywa kwa njia nyingi tofauti. Inaweza ikawa hotuba, chapisho kwenye gazeti, filamu au hata muziki, ambapo yote hufanywa ku "Influence" maoni na fikra za wananchi. Vile vile propaganda ni chombo ambacho kipo na ni cha umuhimu kwa kila serikali katika kulinda amani na kuendesha shughuli zake. Cha muhimu kuliko vyote ni kutumia chombo hiki vizuri...
 
Naona kama mwaka huu propaganda za kumbrand rais zimezidi kiasi. Inawezekana mama ana wasiwasi kuwa hakubaliki hivyo anatumia wapambe kumfanyia propaganda za kumbrandi, au wapambe wanafanya kumbrand kwa kujipenedeza, ila in any case ni too much. Nimeishi chini ya awamu zote tangu uhuru, nadhani hii inaongoza kwa propaganda za aina hiyo.

Kipindi cha Nyerere pia kulikuwa na propaganda sana, lakini zilikuwa siyo za kum-brand Nyerere kwa vile yeye mwenyewe tayari alikuwa ni brand kubwa, ila kulikuwa na propaganda sana za kuhamasisha siasa ya ujamaa.

Baada ya hapo propaganda zilikuwa za kawaida tu za kuhamasisha sera fulani, ila sasa hivi kumekuwa na wimbi kubwa sana la propaganda za kum-brand rais kutoka kila kona ya serikali na kila kona ya CCM. Eti waziri anaita waandishi wa habari kuwaambia mafanikio yaliyofanywa na rais kwa kipindi cha mwaka mmoja; kioja sana.
 
Hata huu moto uliounguza magodoro nawahakikishia ndugu zangu muheshimiwa Rais,mama yetu Samia Suluhu Hassan atapambana nao hadi mwisho.😂😂😂😂😂😂
 
Eti waziri anaita waandishi wa habari kuwaambia mafanikio yaliyofanywa na rais kwa kipindi cha mwaka mmoja; kioja sana.

Hakuna hata kitu kimoja cha maana alichokifanya. Sana sana ameirudisha nchi nyuma sana.

Teuzi za hovyo, zisizofuata vigezo,weledi, common sense, usimamizi na usimamiaji hakuna.

Matatizo ya umeme,maji, nidhamu serikalini, rushwa iliyokithiri,wizi na ujambazi kuongezeka, uonevo wa polisi umeongezeka sana, kuwatimua wachapa kazi wengi na kuwarudisha wezi wote serikalini.

Mafanikio ni kuwakamua Watanzania na tozo, kodi, bei kubwa za mafuta, ujenzi, chakula, kutimua machinga, kutembeza bakuli,kukopa hovyo kwa vitu visivyo na tija, kupeleka pesa, ajira nyingi nyumbani bila uwiano sahihi, au kutenda haki kwa Watanganyika.
 
Serikali haina dira, mwelekeo, sera,maono, seriousness anasema kazi iendelee huku akizipinga na kuzihujumu hizo kazi kwa kuteua watu wasiofaa,wasio na maadili, wahuni kila sehemu muhimu, ya kimkakati kwenye uchumi namaisha ya Watanzania.

Ngorongoro inaenda kuuzwa, Bandari ya Dar na Bagamoyo kutafutiwa ubia kwa mikataba ya siri na watu wanaojali pesa kuliko maslahi mapana ya Watanzania.

Basically ameshindwa kwa karibu kila kitu na kila anachokigusa anaharibu zaidi.
 
serikali inatumia kila fursa kufanya "branding" ya yale yote yanayo fanyika serikalini na zaidi, kuhakikisha kwamba Jina la Rais Samia Suluhu Hassan linakubalika kila mahali nchini na kwa watanzania wote. Zoezi hili linafanywa kimkakati sana haswa na vyombo vya habari vikishirikiana na viongozi mbalimbali.

Serikali inajihusisha sana na suala hili na kwasababu hiyo, lazima kuna madhumuni ya hali kuwa kama ilivyo. Labda ni njia ya kuwa na "Control" kwa kuhakikisha kwamba serikali ina "impact" sana maoni ambayo watanzania wanaweza kuwa nayo kuhusu utendaji kazi wa serikali yao. Labda ni njia ya kumjengea Rais Samia mahusiano mazuri na watanzania na hivyo kuhakikisha kipindi chepesi zaidi katika uchaguzi mkuu ujao. Labda serikali ina amini kwamba kuna hatari kwa wananchi kupata taarifa ambazo hazija chujwa kikamilifu.

Yote haya yanaonyesha nguvu ambayo serikali inayo katika kufanya kitu chochote au kuchochea maoni yoyote kutoka kwa wananchi. Hii inaitwa propaganda.

Propaganda inaweza kufanywa kwa njia nyingi tofauti. Inaweza ikawa hotuba, chapisho kwenye gazeti, filamu au hata muziki, ambapo yote hufanywa ku "Influence" maoni na fikra za wananchi. Vile vile propaganda ni chombo ambacho kipo na ni cha umuhimu kwa kila serikali katika kulinda amani na kuendesha shughuli zake. Cha muhimu kuliko vyote ni kutumia chombo hiki vizuri...

Propaganda, uchawa, haviwezi kuondoa uhalisia unaonekana na kila mwenye macho.
 
Sio kweli, enzi za jiwe ndipo propaganda zilianza na kutamaliki. Kwenye vyombo vya habari, vya dola, vyuo, wanamuziki, comedians, timu za mpira n.k ilikuwa lazima jina lake litajwe hata katika mambo ambayo hakuhitajika kutajwa kabisa. Sasa ni muendelezo tu wa legacy.

Back
Top Bottom