Kama mtu chini ya miaka 18 haruhusiwi kupiga kura, basi iwe marufuku watoto wadogo kufundishwa imani za kidini mpaka wafike miaka 21

Hoja ipo ila haiwezekani kwa maana imani ni jambo la miiko ya jamii husika, sasa kiuhalisia hakuna jamii isiyo na miiko
 
Mtazamo wako ni wa secularist. Ukweli ni kuwa bila masuala ya Dini ulimwengu ungeshafutiliwa mbali. Dini inasaidia watu kuwa na hofu ya kutenda maovu. Kipindi cha Nuhu watu hawakuwa na dini ona kilichotokea! Watu waliishi kama wanyama. Zinaa, dhuluma, mauaji nk ilikuwa ni kawaida tu.
 
Maana au tafsiri nzuri haviakisi uzuri wa kitu, acha hiyo maana ya mfumo wa maisha, kuna dini ya Mungu, ummat wa mtu fulani n.k yote yana sura nzuri lakini mwenendo, mafundisho, matendo kwa maana ya uhalisia wa ndani hakuna kitu
 
Ni kweli kabisa mkuu. Nawaonea huruma watoto wanavyochapwa bakora huko madrassa. Wawaache wawe wakubwa w.aamue wenyewe.
 
Nafikiri hata elimu ya sekula pia tusubiri mpaka afike 24 years maana kumlazimisha mtoto kujifunza mahesabu , sijui mafizikia tunawaharibu sana sana sana mbaya zaidi wanatiwa stiki wakiwa hawawezi kunyoosha miandiko au wakifeli au wakichelewa kushika namba .

Au unaonaje mtoa mada elimu zote za imani na sekula zitolewe kwa wao wakishakuwa vijana wakubwa miaka 24 na kuendelea tena kwa maamuzi yao wenyewe .
 
Maana au tafsiri nzuri haviakisi uzuri wa kitu, acha hiyo maana ya mfumo wa maisha, kuna dini ya Mungu, ummat wa mtu fulani n.k yote yana sura nzuri lakini mwenendo, mafundisho, matendo kwa maana ya uhalisia wa ndani hakuna kitu
Msingi wa mfumo sahihi wa maisha ni watu wake kujipanga kwa sifa na matendo ya uadilifu na kufanya wema ya kiislam ambayo ndani yake hakuna kitu
Au vitendo vibaya

Thibitisha
 
Msingi wa mfumo sahihi wa maisha ni watu wake kujipanga kwa sifa na matendo ya uadilifu na kufanya wema ya kiislam ambayo ndani yake hakuna kitu
Au vitendo vibaya

Thibitisha
Uthibitisho msikilize huyo Sheikhe hapo
Pia kuna nchi hizi za Kiisla ambazo zimepiga marufuku kuoa mwanamke zaidi ya mmoja,
Turkey, Tunisia, Albania, Kosovo na Central Asian countries
 
Uthibitisho msikilize huyo Sheikhe hapo
Pia kuna nchi hizi za Kiisla ambazo zimepiga marufuku kuoa mwanamke zaidi ya mmoja,
Turkey, Tunisia, Albania, Kosovo na Central Asian countries
Shekhe gn nimsikikize.

Lkn ipi

Hakuna nchi ya kiislam.

Kuna nchi zenye waislam wengi.

Tofautisha
 
Kupiga kura na kuabudu ni vitu viwili tofauti kabisa, mnapokosa hoja za kuandika mnakuja na vitu vya ajabu sana.
 

Mleta uzi ni mkristo au alikuwa mkristo (abishe tuone). Wengi wa hawa wazee wa "hizi dini zifutwe" na wanaoigiza u atheist humu wengi wao ni wakristo waliochanganyikiwa. Wana mashaka na dini yao wanaishia kusema "dini zote hazifai". Wanataka kupoteza na watu wengine wote.
 
Naunga mkono 99%
 
Kweli mkuu msingi wa dini lazima ujengwe kuanzia utotoni akishakuwa mkubwa ana machaguzi yake binafsi ila kama mzazi ulishapambana kwa uwezo wako uliojaaaliwa .
 
Mkuu hata bibilia haikuandikwa kwa kiswahili bali imetafsiriwa kitu ambacho hata Qur'an pia imetafsiriwa kwa kiswahili na lugha zengine.
 
Huko China, ukristo na uislamu unachukua sehemu ndogo tu ya jamii ya wachina wengi wao wana dini tofauti kabisa.

Dini ya mwafrika mpaka leo sijui ni ipi iliyosalia .Yaani sisi ni wa kupandikizwa tu imani za watu wengine!!!
Kwani mkuu kila jamii ina dini kasoro sisi waafrika au waafrika ndio tunaona tumeletewa dini pekee yetu?
 
Tusaidie tofauti iliyopo kati ya kupiga kura na kuabudu
Kuabudu kunaanzia utotoni, Baba na Mama wanakwenda kanisani au msikitini na watoto wao ili wamjue Mungu tangu wakiwa wadogo.

Kupiga kura ni suala la kisiasa, lengo ni yule anayeingia kwenye kachumba na kupiga kura awe anajua ukubwa wa majukumu ya huyo anayempigia kura.

Ngoma ya kitoto haikeshi, kuna msemo mwingine unasema mtoto halali na pesa. Walioibuni hiyo misemo wanaelewa kwa kina mipaka ya shughuli zenye kuwajumuisha watoto inaishia wapi.
 
Hiyo ndio lugha yake
Hata Bible inalugha yake ya Asili lakini leo Wakristo wa Mataifa yote wanasoma Scriptures kwa Lugha zao za Asili.

Kuna Bible za Lugha hadi za Kibantu wakati huko Nigeria kuna Waisilamu waliojaribu kusoma kuruani kwa Lugha ya Kihausa wakapigwa marufuku na Sultan wa Sokoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…