Kama mtu chini ya miaka 18 haruhusiwi kupiga kura, basi iwe marufuku watoto wadogo kufundishwa imani za kidini mpaka wafike miaka 21

Dini ni utapeli , Wanasema dini ni mfumo Wa maisha wanatakiwa Wajua hata wahadzabe hawana dini lakini wanamfumo wa maisha , Mfumo Wa maisha upo tu na unatokana na tamaduni Mila za watu wa sehemu husika mfano mdogo ni huu kuna watu Wana Kula nguruwe na wengine hawali yote ni kwasababu Imani na tamaduni zao ni tofauti, so suala la mfumo Wa maisha lipo pale pale hata kama hizo dini zisingelikuwepo ,

Ukitaka ujue dini ni utapeli na uchizi Kwa wanao ziamini ni issues ya msalaba wakristo wakati Wana amini ktk misalaba na kuifanya kuwa ndio symbol ya dini yao Wanashindwa kutambua waasisi wa misalaba walikuwa ni waroma walikuwa wanaitumia misalaba kama silaha ya kuwaadhibia watu waliokuwa hawafuati Sheria za utawala wao wa wakati huo hata Ukitazama series ya Spartacus utakutana na hizo script 😁😁😁😁

Turudi sasa Kwa waislam kuna mafundisho ya baadhi ya hadith yanasema kuwa Moja ya miujiza ya mtume alikuwa ana Ongea mpaka na ngamia yaani wanaongea kabisa kama mtu aongevyo na Mtu mwingine πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
Na kuna watu Wana amini huo ujinga

Ili iweze muumini wa hizo dini inatakiwa uwe punguani chizi tena na nusu
 
Je unahisi watoto tulionao wanamjua mungu au wamemkariri mungu au wameaminishwa tu kumjua mungu

Itakuwaje km watoto wataamuriwa kupiga kura kwa kufuata nyao za wazazi wao

hapa sina neno
Kumjua Mungu kwa vitendo kunaenda na ukuaji wa mtoto, mafundisho tuliyopewa enzi zile tukiwa darasa la tatu kuhusu masuala ya Biblia hatukuyaelewa kwa mtazamo tuliokuja kuukuta ukubwani.

Naamini ni kosa kwa watoto wanaoishi chini ya himaya za wazazi kupiga kura, ndio maana ni kuanzia miaka 18 ambapo anachukuliwa na jamii kwamba anaelewa nini kinachoendelea duniani.

Mleta mada nimemuelewa vizuri hii mada yake, hapendi kuuona huu utamaduni wa watoto kupelekwa katika mikutano ya kisiasa kwa kupandishwa kwenye malori.

Kuna mkutano mmoja miaka ya nyuma wa kisiasa ulifanyika mle ndani ya ukumbi wa Karimjee, wakachukuliwa watoto wa shule za msingi za Dar wakajazwa katika viti.

Mkutano umeendelea kwa muda wa saa moja mada zinajadiliwa na zaidi ya nusu ya watoto wakiwa wamesinzia!.

Ni kutowatendea haki watoto kwa kuwaingiza katika siasa za lawama wangali bado hawajui kwa kina kipi kinaendelea duniani.
 
Wewe ndio una confusions sisi wenyewe tunaoamini hatuna hata chembe ya waiwasi.Pole sana though
 
Katika utapeli mkubwa uliowahi kutokea kwenye hii Dunia ni dini.

Dini ni utapeli wa hali ya juu, watu wanatapeliwa kw akuahidiwa maisha hewa ambayo hayapo mahala ambapo hapapo chini ya kiumbe hewa kinachoitwa Mungu.

Ni mambo ya ajabu sana.
Hakika ujinga wa uzeeni lazima utakufa nao tu
 
Hoja unayo lakini kwangu mimi ninayefuata ukristu ntabisha.
1-Yesu alipokuwa na siku chache baada ya kuzaliwa alipelekwa hekaluni kupata baraka za "mchungaji" wa wakati huo.
2-Akiwa na umri mdogo(chini ya miaka 10-12)Yesu alikuwa anahudhuria kwenye masinagogi/mahekalu na kushiriki sala/ibada na jamii yake.
Hiyo ni mifano michache tu ya anayefuatwa alionesha kabla ili wafuasi wake nao wachukue mifano.
 
Sasa swali linakuja, kwanini mtoto anapozaliwa asiachwe mpaka awe mtu mzima awezi kufanya maamuzi sahihi afuate dini gani na dhehebu gani au asifuate dini kabisa?
Hoja yako ni ya kipuuzi ni sawa na wewe ungeachwa mpaka ufike miaka 21 ndio ufundishwe kusoma na kuandika..
Fikiria ugunu wake
 
Me naona zifutwe tu zote kila mtu abaki na Mungu wake moyoni, mambo ua kupigizana yowe uko mabandani kama Kuku mkisema ni ibada ni upotevu wa muda na mali za wananchi.
 
Wewe ukiwa na miaka 21 moja na ukaambiwa mungu ambae hajaumbwa katamka maneno dunia ikatokea then siku zikapita then jua na mwezi then mimea watu etc afu demu akala tunda alilopewa na nyoka anayeongea Mungu akakasirika akawafukuza kwenye bustani baadae bikra alizaa mtoto akaja kutembea kwenye maji, kufufua watu, akafa akafufuka na yeye na kupaa kwenda juu mawinguni (cjui oxygen na pressure mda huo vilikuwaje huko juu) afu "soon" atarudi na farasi wakupaa kuja kuchukua watu wake na kwenda nao kusikojulikana...

Ungeamini?
 
Au una miaka 25 ukaambiwa Kuna mwarabu mmoja zamani alifatwa na malaika akapewa maandishi ya kiarabu ahubirie dunia nzima na watu wasiofata watachomwa moto milele wakishakufa (asa cjui nini kinachomwa moto) ila wakifata wataenda mbingu ya 7 kula bikra 72 na kunywa kwenye mito ya pombe...

We ungeamini?
 
Dini zilitakiwa kufundishwa baada ya mtoto kumaliza shule ya msingi na secondary
 
Sina la kuongeza. Asante sana.
 
Acha kuwafurusha wa kwako ,usiwapangie wazazi wengine
U atakua kizazi kiweje?
 
Ndio ni ujumbe na ndio maana ipo hadi tafsiri ya Qur'an ya kiarabu
Kwamfano Salamu ya Kiislamu ni "Salama alekum"Kiarabu, ambayo maana yake ni "Amani iwe juu yako"Kiswahili,, swali langu ni kwanini mkiwa mnakutana msiwe mnasalimiana Kiswahili tu badala ya Kiarabu vivo hivyo katika Quruani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…