Kama mtu chini ya miaka 18 haruhusiwi kupiga kura, basi iwe marufuku watoto wadogo kufundishwa imani za kidini mpaka wafike miaka 21

Mimi naamini Mungu aliyeniumba hana Kabila sasa kwanini nimuombe kwa Lugha ya Kigeni?!

Nitamuomba Mungu kwa Lugha yangu iwe Kiswahili au Kikabila changu.
Kwanza sijui kama kuna imani inasema kwamba ukiomba dua lazima utumie lugha fulani tu na si lugha zengine, mbona tunaona viongozi wa dini wakiomba dua kwa kiswahili wanapokuwa katika shughuli za kiserikali au kisiasa?

Mungu hana kabila kama ulivyosema, sema wewe mtazamo wako kuhusu lugha ndio una shida na ndio maana nikakupa mfano wa kwamba hata hapa Tz kuna mjadala kuhusu lugha ya kufundishia kwa maana wapo wenye kuona kiendelee kutumika kiingereza(lugha ya kigeni) na wapo ambao wanataka kitumike kiswahili.
 
Uko sahihi,tunalazimishwa kuwa uislam na ukirsto ndio dini zenye maana kuzidi za kwetu za asili
Mimi nadhani hizo dini mnazoita za asili ndio zinalazimishwa tena zaidi ya hizi mnazoita za kigeni, kwa sababu zimefungamanishwa na asili na mababu ilivyo ni kama vile ambavyo mtu anatambulika kuwa yeye ni kabila fulani kwa sababu tu ya mzazi wake. Hizo dini za asili hazitoi nafasi ya kuamua uamini au usiamini kwa sababu kwa kutoziamini unaonekana umeacha asili yako na kukana mababu zako hivyo unalazimishwa kwamba walichokuwa wanaamini mababu zetu ndio ilikuwa sahihi kisa mababu zetu.
 
mbona tunaona viongozi wa dini wakiomba dua kwa kiswahili wanapokuwa katika shughuli za kiserikali au kisiasa?
Hizo ni Dua lakini kwenye Sala sijawahi kusikia Kiswahili.
 
We kweli zwazwa, kwa hivyo wafundishwe nini bwege wee
 
Hizo ni Dua lakini kwenye Sala sijawahi kusikia Kiswahili.
Tumetoka kwenye dua na sasa tumeingia kwenye ibada(sala), labda nikuulize kwa jinsi aina ya sala ya waislamu ilivyo wanakusanyika kwa pamoja kuna wakati unakuta ni jamii tofauti tofauti zenye lugha mbalimbali unadhani kikitumika kiswahili kwenye hiyo ibada wote wataelewa hata kama hawakijui kiswahili?
 
Mbona katika Ukristo imewezekana.
 
Mbona katika Ukristo imewezekana.
NIni kimewezekana kwamba wasiojua kiswahili wakienda kwenye makanisa yenye kutumia kiswahili wanaelewa kiswahili?

Kuna ibada makanisani hapa hapa bongo huwa zinafanywa kwa kiingereza. Nilikuwa na rafiki yangu mmoja kutoka Ghana alikuja Tz yeye alikuwa anaenda kanisani ambapo hutumika kiingereza.
 
NIni kimewezekana kwamba wasiojua kiswahili wakienda kwenye makanisa yenye kutumia kiswahili wanaelewa kiswahili?
Kwasababu teyari wanajua Bible Verses na numbers
Mfano Corinthians 13:4–8 👈 teyari inajulikana 13:4-8 kwenye Bibilia ya Kiswahili.
 
Sisi Watanzania tunaelewa zaidi Kiswahili kuliko Lugha za Kigeni.
Ni kweli kabisa mkuu na changamoto iliyochangia kuzaa kizazi kibovu cha kiswahili kinachagizwa na kutokumheshimu baba wa kiswahili bwana shaban robert kama anavyoheshimika shakespear baba wa kingereza
Leo tanzania badala ya mswahili kuheshimika ndio anaonekana mpumbavu
 
Uko sahihi.
 
Una Fuvu gumu sana, Quruani ni ujumbe uwe Kiarabu Kiswahili Kijapani Kingereza nk.nk.
Na ujumbe unawafikia watu na hilo ndio lengo kiarabu hakijakwamisha lengo, wewe unaleta habari za uzalendo kwamba kitumike kiswahili tu kusiwe na Qur'an iliyo katika lugha yake ya asili ya kiarabu tuwe na Qur'an ya kiswahili kisa sie ni wazungumzaji wa kiswahili.
 
Allah ni Mwarabu?! Mimi Imhotep ni Mwafrika nina Lugha yangu ya Kisumbwa na kuna Biblia za Kisumbwa.
 
Allah ni Mwarabu?! Mimi Imhotep ni Mwafrika nina Lugha yangu ya Kisumbwa na kuna Biblia za Kisumbwa.
Duh! Mkuu naona aje mtu kukusaidia kuelewa maana narudia yale yale tu. Hiyo biblia ya kisumbwa ni tafsiri ya biblia kwa kisumbwa kama ambavyo biblia ilivyo tafsriwa kwa lugha zengine pia. Sasa nimekwambia hata Qur'an imetafsiriwa kwa lugha zengine pia ikiwemo na kiswahili.

Sasa tatizo mara utasema hujaona watu wakisoma Qur'an kwa kiswahili mara kusali kwa kiswahili, hauelewi na hauelewi unachozungumzia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…