Kama mtu chini ya miaka 18 haruhusiwi kupiga kura, basi iwe marufuku watoto wadogo kufundishwa imani za kidini mpaka wafike miaka 21

Kama mtu chini ya miaka 18 haruhusiwi kupiga kura, basi iwe marufuku watoto wadogo kufundishwa imani za kidini mpaka wafike miaka 21

Ni kweli kabisa mkuu. Nawaonea huruma watoto wanavyochapwa bakora huko madrassa. Wawaache wawe wakubwa w.aamue wenyewe.
Kwanini waache dini tu kuwa ndio hadi mtoto akuwe ndio aje kuamua mwenyewe na si kuacha na mambo mengine pia? Kuna mambo mengi sana kutoka kwa wazazi na jamii mtoto hujifunza tokea utotoni.
 
Hata Bible inalugha yake ya Asili lakini leo Wakristo wa Mataifa yote wanasoma Scriptures kwa Lugha zao za Asili.

Kuna Bible za Lugha hadi za Kibantu wakati huko Nigeria kuna Waisilamu waliojaribu kusoma kuruani kwa Lugha ya Kihausa wakapigwa marufuku na Sultan wa Sokoto.
Hizo ni tafsiri, wanachokisoma hapo ni tafsiri na nishakwambia kwamba Qur'an pia imetafsiriwa kwa kiswahili.
 
Moja ya mambo yanayovuruga sana wanadamu ni mambo ya imani ambayo msingi wake ni kuamini bila kuhoji na kuhoji ni sawa na kukufuru(unamezeshwa).

Maajabu zaidi ni kuwa tuna vitabu viwili ambavyo ni Bibilia na Quran, lakini kwasababu watu wamekuja na tafsiri zao za haya maandiko, leo tuna madhehebu kibao kwa kila dini wakati Mungu tunaambiwa ni mmoja.

Matokeo ya hali nii mtu anazaliwa na kukulia katika dhehebu fulani mfano mkatoliki, baadae anahama anakuwa mlokole kwa hoja hawezi kukombolewa kupitia ukatoliki au mtu anzaliwa na kukulia katika ukristo, akikua anaona ukristo sio dini sahihi anahamia kwenye uislamu and vice versa.

Kituko kingine ni mtu kubadili dini kisa kuoa au kuolewa. Huu ndio uthibitisho hizi dini sometimes tunaburuzana tu na wala hatuziheshimu kabisa.

Sasa swali linakuja, kwanini mtoto anapozaliwa asiachwe mpaka awe mtu mzima awezi kufanya maamuzi sahihi afuate dini gani na dhehebu gani au asifuate dini kabisa?

Kama tunaona mtu mwenye umri wa chini ya miaka 18 hawezi kuwa na maamuzi sahihi kwenye sanduku la kura, ni kwanini kwenye mambo sensitive kama haya ya kiimani turuhusu watoto kuburuzwa na wazazi wao kiiamini kwa kutakiwa au kuachwa kufuata dini za wazazi wao?

Mtu anapobadili dini au dhehebu, huwa anatubu kuwa alikuwa amepotoka, na kama hatubu, hiyo dhambi ni nani anastahili kuibeba kama sio mzazi au mlezi?

Tukumbuke baadhi ya hizi dini na madhehebu yametokana tu na mitazamo/tafsiri za wanadamu kama sisi.

Tuwaache watoto mpaka watopofikia utu uzima(walau miaka 21) ndio wachague dini na dhehebu au kutokuwa na dini kabisa wakiona ni sahihi kufanya hivyo.

Tubadilike.
Tafakuri sana. Mtu akifika umri huo na hakjasoma kitu atakuwa ameshapotea.
Sasa mini kama mzee nina wajibu kufunza yale mema ninayo ya Fuata. na atapokuja kuwa mkubwa anayo haki ya kwenda anako taka na kufuata anacho kiona yeye bora.
Anayo haki kukataa yale niliyo mfunza.
Na mie ninayo haki ya kumkubali awe nami au nifukuze awe mbali nami
 
Hata hawa wanaopinga dini nao unakuta wengi walilelewa katika familia na misingi ya dini ila wamekuja kubadilika ukubwani na kufuata wanavyoona wao ni sahihi.
 
Kusomwa Kiswahili.
Bado sijakuelewa kusomwa vp? Kwa sababu tafsiri ya Qur'an ya kiswahili ipo na husomwa maana sio waislamu wote wanajua kiarabu. Au unakusudia kwamba hadi kwenye ibada itumike tafsiri ya kiswahili ya Qur'an?
 
Quruani kusomwa Kiswahili, unashindwaje kuelewa?!
 
Kuabudu kunaanzia utotoni, Baba na Mama wanakwenda kanisani au msikitini na watoto wao ili wamjue Mungu tangu wakiwa wadogo.
Je unahisi watoto tulionao wanamjua mungu au wamemkariri mungu au wameaminishwa tu kumjua mungu
Kupiga kura ni suala la kisiasa, lengo ni yule anayeingia kwenye kachumba na kupiga kura awe anajua ukubwa wa majukumu ya huyo anayempigia kura.
Itakuwaje km watoto wataamuriwa kupiga kura kwa kufuata nyao za wazazi wao
Ngoma ya kitoto haikeshi, kuna msemo mwingine unasema mtoto halali na pesa. Walioibuni hiyo misemo wanaelewa kwa kina mipaka ya shughuli zenye kuwajumuisha watoto inaishia wapi.
hapa sina neno
 
Moja ya mambo yanayovuruga sana wanadamu ni mambo ya imani ambayo msingi wake ni kuamini bila kuhoji na kuhoji ni sawa na kukufuru(unamezeshwa).

Maajabu zaidi ni kuwa tuna vitabu viwili ambavyo ni Bibilia na Quran, lakini kwasababu watu wamekuja na tafsiri zao za haya maandiko, leo tuna madhehebu kibao kwa kila dini wakati Mungu tunaambiwa ni mmoja.

Matokeo ya hali nii mtu anazaliwa na kukulia katika dhehebu fulani mfano mkatoliki, baadae anahama anakuwa mlokole kwa hoja hawezi kukombolewa kupitia ukatoliki au mtu anzaliwa na kukulia katika ukristo, akikua anaona ukristo sio dini sahihi anahamia kwenye uislamu and vice versa.

Kituko kingine ni mtu kubadili dini kisa kuoa au kuolewa. Huu ndio uthibitisho hizi dini sometimes tunaburuzana tu na wala hatuziheshimu kabisa.

Sasa swali linakuja, kwanini mtoto anapozaliwa asiachwe mpaka awe mtu mzima awezi kufanya maamuzi sahihi afuate dini gani na dhehebu gani au asifuate dini kabisa?

Kama tunaona mtu mwenye umri wa chini ya miaka 18 hawezi kuwa na maamuzi sahihi kwenye sanduku la kura, ni kwanini kwenye mambo sensitive kama haya ya kiimani turuhusu watoto kuburuzwa na wazazi wao kiiamini kwa kutakiwa au kuachwa kufuata dini za wazazi wao?

Mtu anapobadili dini au dhehebu, huwa anatubu kuwa alikuwa amepotoka, na kama hatubu, hiyo dhambi ni nani anastahili kuibeba kama sio mzazi au mlezi?

Tukumbuke baadhi ya hizi dini na madhehebu yametokana tu na mitazamo/tafsiri za wanadamu kama sisi.

Tuwaache watoto mpaka watopofikia utu uzima(walau miaka 21) ndio wachague dini na dhehebu au kutokuwa na dini kabisa wakiona ni sahihi kufanya hivyo.

Tubadilike.
Hujielewi na wala hujui unachowasilisha,unachosha watu kusoma ugolo wako.Elewa nn maana ya tofauti Alafu ndio ulete mada hapa.maana hapa tunajifunza mambo mengi ikiwa ni kutoka na kwako pia.
 
Kimsingi hakuna mtu 'anaburuzwa' katika mambo ya imani; ni wewe tu kufuata mkumbo wa wazazi. Lakini mtu anapokuwa mtu mzima anayo hiyari kuchagua dini/imani anayoyotaka hata kama ikiwa kinyume na wazazi. Huku 'kwetu' tunaamini mwanamke hana kabila wala dini, maana akiolewa anafuata mkumbo wa mume wake (labda hata kinyume chache siku hizi inawezekana).
Ukiendekeza wazazi wanaweza kukulazimisha kusomea udaktari wakati hata hujui "mucus" ni nini; kumbe kidato cha tatu uli-escape kusoma biology..!
 
Quruani yenyewe isomwe Kiswahili nikupe mfano kuna Biblia za Kiarabu huko Lebanon zinasomwa Kiarabu.
Mkuu nimeeleza kwamba Biblia hizi tunazoona zimeandikwa kiingereza,kiarabu au kiswahili ni tafsiri za biblia. Na Qur'an nayo ipo tafsiri ya kiingereza,kiswahili,kifaransa n.k

Kwa uelewa wangu ukiniambia watu wanasoma biblia kwa kiswahili au kiarabu nachoelewa ni kwamba wanasoma tafsiri ya biblia ya kiswahili au kiarabu,na ndio maana kuna matoleo mengi tu ya tafsiri ya biblia.

Ndio maana nakuuliza unakusudia watu wasome tafsiri ya Qur'an ya kiswahili badala ya kusoma Qur'an kwa lugha yake ya asili?
 
Tatizo mleta mada yeye kaona dini tu ila dini ni moja tu ya mambo ambayo yapo kwenye jamii zetu kama yalivyo mambo mengine na mtoto hawezi kukwepa hayo mambo.
 
Mkuu nimeeleza kwamba Biblia hizi tunazoona zimeandikwa kiingereza,kiarabu au kiswahili ni tafsiri za biblia. Na Qur'an nayo ipo tafsiri ya kiingereza,kiswahili,kifaransa n.k
Quruani ni ujumbe sio lugha unaweza kusoma Quruani Kiswahili
 
Quruani ni ujumbe sio lugha unaweza kusoma Quruani Kiswahili
Ndio ni ujumbe na ndio maana ipo hadi tafsiri ya Qur'an ya kiarabu, kwa maana hiyo tafsiri ya Qur'an sio kwamba ni kutafsiri huo ujumbe kwa sababu tu upo kwenye lugha ya kiarabu bali ni kutafsiri maana ya ujumbe wenyewe iwe kwa kiarabu chenyewe au kwa lugha zengine.

Sasa sijaelewa point yako hasa ni ipi kwa kutaka isomwe Qur'an kwa kiswahili?
 
Back
Top Bottom