Mungu hayupo.
Idea ya Mungu kuwapo inapata umaarufu kwa sababu watu wengi wavivu hawataki kufikiri na hawataki kuchukua responsibility, wanataka mungu awepo ili achukue dhamana ya kutatua mambo yote.
Pia watu wengi hawafikirii logically, wanafikiria emotionaly.
Pia watu wengi wanaogopa kusema wanachofikiri na ku question uwepo wa mungu kwa sababu wanaogopa kuonekana wako tofauti.
Pia kusema huamini kuwepo mungu kunaweza kukukosanisha na familia, jamaa, rafiki, kazini etc.
Kitu kukubalika haina maana ni cha kweli. Kuna wakati watu waliamini dunia ni bapa na si tufe. Hilo halikufanya dunia iwe bapa.
Kuna wakati watu waliamini jua linazunguka dunia. Hilo halikufanya jua lizunguke dunia.
Hata kama watu wote wataamini mungu yupo, kama hayupo hayupo tu.
Kama unasema mungu yupo, thibitisha mungu yupo.