Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Tumeona tunavyoshindwa kesi; tumeona mashaka ya wananchi kwenye mkataba; tumeona hata mkataba wenyewe tu unaamini kwamba ipo siku utavunjika au kuleta utata na ndio maana umewekewa kifungu cha kutumika kwa mahakama za Afrika kisini na Sheria za Uingereza.
Kama walioandaa akiwemo mwanasheria Mkuu wetu waliamini kwamba upo wakati mkataba huu utaleta utata na tutaenda mahakamani; anapata wapi nguvu ya kumtetea mpinzani wetu?
Je, siku DP world au mwanasiasa mwingine baada ya Mhe. Rais aliyepo atakapokuja kuamua kupitiwa kwa mapungufu ya mkataba na DP world wakakataa mazungumzo wakatupeleka mahakama za Dunia; mwanasheria atapataje nguvu ya kutumia kodi zetu kwenda kutuwakilisha kwenye kesi hizo?
Kwanini mwanasheria mkuu kwenye mikataba asibaki neutral kuepuka kuingizwa kwenye conflicts of interest? Kwanini tunaamini mwanasheria wa serikali anaweza kwenda kwenye vyombo vya habari akamtetea mpinzani wetu?
Hii ya mwanasheria mkuu kuwa upande wa wawekezaji haiwezi kuwa sababu ya serikali kuendelea kushindwa kesi huko nje kila siku na kutakiwa kulipwa fidia lukuki?