dist111
JF-Expert Member
- Nov 29, 2012
- 3,758
- 3,199
Tahadhari: Mawazo haya yanatikana na Imani yangubkubwa katika:
1. Biashara shindani, Yaani bila ushindani, biashara lazima itadorora.
2. Jamii imegawanyika kwenye matabaka mbalimbali, mfano wafanyabiashara, wafanyakazi, n.k.
Nikimaanisha mfanyakazi hataweza kurndesha biashara na kinyume chake
3. Tanzania ninya watanzania na itaendelezwa na watanzania. Lazima wengine wawezeshwe ili wawe chachu ya maendeleo kwa taifa zima.
Baada ya tahadhari hiyo naomba nitoe mfano wa namna ambavyo nadhani biashara ya Mwendokasi ingeweza kufanyika.
Mfano: Kuna siku nikitembelea singida, nikaingia mgahawani kula chakula cha mchana (Sikumbuki Jina) ila niliona Ajabu saana, Yaani wahudumu walikuwa sharp saana, na wateja walikuwa wanagombewa, mwisho nikajua kugundua kuwa ndani ya mgahawa huo (Au bar, I am not sure) kuna majiko mawili ya chakula. Na wahudumu wa pale wanawagombea wateja. Naamini, walikuwa sharp kwa sababu ya ushindani huo uliotengenezwa na mwenye mgahawa. Ikimaanisha lazima wapike chakula kizuri lakini pia lazima wawachangamkie wateja ili na wao waingize siku yao.
Lastly: Hivi ndivo ninaamini ingekuwa biashara sahihi ya Mwendokasi.
1. Kwanza ningewezesha kampuni moja ya mtanzania iweze kumili biashara ya kutoa kadi za malipo kwa abiria. Kila stendi ya Mwendokasi ingekuwa na help desk ya kuservise kadi hizo za usafirshaji. Mbeleni, tutaeleza faida zitazotokana na abiria kuwa na kad ya muda mrefu na namna kampuni hii itavutia abiria kuwa na Kadi hizi pamoja na namna atakavopata faida ya vivutio atakavyoviweka kwenye Kadi hizi za usafiri.
2. Ningetangaza zabuni ya watanzania wenye magari zaidi ya kumi (au wenye uwezo wa kuyanunua), ili washiriki katika kutoa huduma za usafiri wa mabasi ya Mwendokasi. Ningetoa masharti ni Aina gani ya mabasi yanayohitajika, na huduma inahitajika kupatikana katika mabasi hayo. Huduma mojawapo ni kulipia usafiri kwa Kadi, ndani ya gari. Tena kwa kuchanja. Ni Imani wangepatikana (au wangewezeshwa watanzania 20-30 wamiliki mabasi hayo, tena yakifanya biashara ya kushindana kusafirisha abiria basi suala Hili la Mwendokasi lingekuwa limepata ufumbuzi
3. Ningetangaza, zabuni 2 au 3 za garage, ili magari yote ya Mwendokasi yawezepata maintenance katika garage hizo. Hiii itasaidia services za ushindani kwenye Mwendokasi. Uwezeshaji wa ziada utahitajima mbeleni ili garage hizi ziweze kuanza kutengeneza vifaa vidogo vidogo vya magari hayo ya Mwendokasi. Maana hii itasaidia kuharakisha matengenezo ya magari ya kuongeza ubunifu kwenye garage zetu hasa zinazotengeneza magari ya Mwendokasi.
4. Kwa mtiririko huu, naamini kungejitajika additional services kwenye Yale mabanda waliyojenga. Hapa ningeweka vioksi vidogo vya hadhi ya kati na kuvikodisha kwa wajisariamali. Vioksi Hivi vingeuza chakula cha haraka (fast food), vifàa vidogo vidogo vya majumbani, na ahitaji madogo madogo ya majumbani. Biashara hizi zingemfanya mtu awe anawahi kituoni, lakini pia atumie pesa nyingi ndani ya biashara hii ya Mwendokasi, tena kwa kutumia Kadi yake ya malipo ambayo inaweza jazwa pesa kwa huduma za Mobile Money au hata vibanda vidogo vya wakala wa Kadi hizo anayepatikana ndani ya stendi hizo.
Kwa haraka haraka: Naiona biashara hii ikifanya kazi kwa ushindani na abiria wakipata huduma nzuri za usafiri na huduma za ziada kama vyakula na sehemu ya kununua mahitaji madogo madogo ambayo wameyasahau au hayapatikani wanapokwenda.
Faida ya Aina hii ya biashara. Kwa haraka haraka, Aina hii ya uendeshaji wa Mwendokasi ina faida zifuatazo.
1. inarahisisha usafiri
2. Inatengeneza mabilionea wasiopungua 30, katika njian moja tu BRTI, Yaani Posta, Kariakoo, Kimara, Mbezi, Muhimbili), ila matajiri au waajiri wataongezeka namna njia za uendeshaji zinavoongezeka.
3. Swali kubwa litakuwa ni kwa namna gani watapatikana waendeshaji wenye magari makubwa 20-30, Jibu hapa ni rahisi. Kwanza wakuanzia watapatikana, na wasipopatikana watapatikana watu wenye utayari wa kurndesha biashara hii na mabanki yatawakopesha ili waendeshe biashara hii. Imani kubwa kwa mabenki itakuwa, kuwa pesa ya biashara hii IPO kwenye Kadi. Ikimaanisha IPO banki na inahama kutoka kwa mtuamiji mmoja kwenda kwa mwingine, so banki Wana uhakika na pesa Yao na ni rahisi kuwakopesha waendeshaji hao.
4. Pesa zote hizi bado zinabaki nchini, ikimaanisha kwenye ajira, Kodi, faida ya biashara, garage services, fasta food nakadhalika. Mzunguko wa pesa utaingezeka maradufu.
4. Kuchochea ubunifu, kama garage hizi zikimature, zitaanza kutengeneza spare parts, na garage hizi au makampuni mtambuka yatakuwa na ubunifu zaidi. Na hapa ndipo unaposikia makampuni ya kutengeneza magari yaanza kutengeneza magari Yao Tanzania. Kwa maana wapo watu wenye experience ya kutengeneza magari, kutengeneza baadhi ya vifaa vya magari, lakini kubwa kabisa soko la magari lipo kwa maana mzunguko wa pesa umeongezeka na watanzania wengi zaidi Wana extra cash kufanya anasa.
Kwa Leo naomba niishie hapa. Ahsante I sana